Clouds FM wamburuza mahakamani Lady JayDee, kesi yapigwa kalenda hadi Mei 27...

Clouds FM wamburuza mahakamani Lady JayDee, kesi yapigwa kalenda hadi Mei 27...

Part 2? Wao Clouds wamejuaje kuwa kuna part 2 na contents zake? Na kwani mahakama ishatoa gag order mara hii hadi imzuie asiiweke hadharani hiyo unayoiita part 2? Kama ishatoa hiyo gag order, imeitoa lini ilhali huyo binti leo ndo kaenda huko mahakamani?

Majomba Jide alishasema kwenye media part II itatoka Tarehe 15 na Clouds wanajua. Alisema immediately baada ya interview ya Ruge. Na Jide alisema more facts will come on 15th. Gang order no body knows kwani content za hati ya mashtaka no body knows na wala hatujui mahakama itachukua muda gani kusikiliza.


Wewe...kwani kesi imesikilizwa leo? Kama imesikilizwa, matokeo yake yamekuwaje?

Alipewa wito wa kuitwa mahakamani na leo atapewa hati ya mashtaka.


That will shall we see. But I'm all for them to duke it out the courtroom.

You got a right to talk Dude!

Labda kweli ndo maana anahaha ku manufacture beef ili auze album na maonyesho yake. Si umesikia anachaji 50K kwenye hicho ki concert chake mbuzi hapo Nyumbani lounge...so I can't put anything past that.

50K VIP pamoja na misosi na albam (CD). Ile Mutu size kubwa kishanunua, ile Mukulu Mukulu (You know what I mean). 20K ni Standard.

Shida iliyopo Clouds same day wanasupport show ya Skyband na New Maisha Club Rachel na kina dogo wengine wamepangiwa show. So kuna hatari binti asiapate watu wengi ingawa anajitahidi kupiga promotion ya nguvu.

She is just a has been who is seeking relevance again. She ain't got it no more.

You could be right. We will see her Plan B, C and D

Unavyomfanya aonekane kama yeye yuko squeaky clean ilhali hayuko makes me SMFH!!

Wote Jide na Clouds wababe. So let us see what will happen finally.

Cha msingi ni yeye huyo binti kukubali hali halisi kwamba hawezi kuwa juu kwenye medani za burudani milele na milele. Na aache kuropoka na kuzushia watu.

Kakataa kukubali na yuko radhi ashindwe. Anadai No Retreat No Surrender!
 
ana bahati sana JD,amwulize Sugu,aliwekwa ndani siku ya uzinduzi wa project ya maralia no more.ashukuru mungu hajaitwa siku ya uzinduzi wa shoo yake.
haya yana mwisho,hakuna jambo lisilo na mwisho.
 
MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo.

Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu.

Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.

Source:Global publishers

Unajuwa siku zote haziwezi kufanana. Wakati akina Sugu na wenzake Vinega wakilalamika watu walidhani utani na sasa hii inaonyesha ni jinsi gani hawa majangili wa mziki wanavyowahujumu wasanii. Clouds wameona wadau wengi wapo upande wa Jide na ndo sasa wameamua kwenda mahakamani ili wamkomoe. Mbona sugu hawakumpeleka mahakamani na alikuwa anawachana live? hao jamaa ni matajiri lakni bado wanawivu sana. Sasa je kama hii ndo ni tabia yao tusitegemee wafanyakazi walio chini yao kuendelea kimaisha kuzidi wao. Hawa wanajivunia chombo chao hiki iko siku naye Jide atafungua redio yake. Tunamuombea Mungu ashinde kesi hii na majambazi hawa wamziki waumbuke na redio yao.
 
Binafsi nasikiliza clouds mostly (rarely naskiza radio). Lakini hainizuii kuona kuwa mnachofanya sio sawa. Mimi ni mnazi wa jay dee na still pamoja na bifu lenu na yeye naskiliza tu clouds kwa sababu kuna baadhi ya vitu napenda kuvisikia. Kwa hiyo kufanya kwenu vizuri kwenye matangazo kunaweza kuwa sawa tu na kushinda kwa ccm kwenye chaguzi. Na sio kitu cah kujivunia.

Naskia p-funk nae kawananga. Sijui mtapeleka wangapi mahakamani. Ruge alitamka kuwa hajaliongelea suala lake na jide kwa sababu halina maslahi ya kitaifa. Na kudai yapo mengi ya kujadili zaidi yake. What is not happening?
Clouds kwa asilimia kubwa sana inaendeshwa na pesa za matangazo ya biashara, kwa mujibu wa Ruge.

Sasa mbona matangazo ya biashara hayajapungua? Manake kama Clouds ingekuwa ni mbaya hivyo kama ambavyo nyie manazi wa CHADEMA mnavyodai humu kusingewa na hata tangazo moja la biashara kwenye hicho kituo.

Acheni propaganda zenu za kinazi hapa.
 
Majomba Jide alishasema kwenye media part II itatoka Tarehe 15 na Clouds wanajua. Alisema immediately baada ya interview ya Ruge. Na Jide alisema more facts will come on 15th. Gang order no body knows kwani content za hati ya mashtaka no body knows na wala hatujui mahakama itachukua muda gani kusikiliza.

Sasa huyo Jide ni komandoo gani anaye-telegraph next move yake? Komandoo wa wapi huyo? Mimi nilidhani komandoo atakuwa na stealthy moves kama za crocodile kumbe wapi, hamna kitu kabisa.

50K VIP pamoja na misosi na albam (CD). Ile Mutu size kubwa kishanunua, ile Mukulu Mukulu (You know what I mean). 20K ni Standard.

Hahahaaa hii tayari najua. Nachosubiri ni pichaz za wabebs wa ukwee pamoja na za cigar mdomoni na poz la kufa mtu.
 
MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo.

Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu.

Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.

Source:Global publishers

mkuu tuwekane sawa huwa ni hati ya madai kwa kesi za madai na hati ya mashtaka kwa kesi za jinai.
 
tats how u can easily give yo insights cz hujui nn hasa kimemfanya mpaka Jide akawa mbogo!
wasanii wangapi tunawajua wanakaliwa na clouds,wanatumika vzr sana kwa show na kuambulia laki 1 na still hawawez kuongea?
tuache kutumia lugha nyepes kusema jide anatafuta wateja wa albamu yake kwa kununua bifu,kwa njaa ipi kali kumfanya awe hvo?
 
Hawa wakina ruge cjui nawaona ni wase**** kwelikweli
ni mijitu feki kabisa sasa hata kusaga na wewe umeanza kuingilia na kusapoti ujinga wa manamba wako ruge!?
 
Source inapokuwa Global publisher huwa napata shida kuamini

Na hii vipi? hebu isome mpaka mwisho kisha urudi tena:

MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo. ...



Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. ...




Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu.




Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo...

Jaydee ambaye alikuwa Baraza la Sanaa ambapo alikuwa akiongea katika jukwaa la wasanii, alipata ujumbe wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa hati hiyo ambayo mwenyewe alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka kwanza awasiliane na mwanasheria wake.

Kikubwa ambacho aliweza kusema kwa waandishi waliokuwa wameongozana naye ni kwamba, kesi itaanza kuunguruma tar 27 mahakamani hapo.

Kati ya vielelezo alivyopewa na mahakama ambavyo alivionesha kwa baadhi ya waandishi ni pamoja na nakala za magazeti na nakala za Post za blog yake pamoja na tweets!

Taarifa za mwanadada huyo kufikishwa mahakamani hapo, ziliibuka chinichini kwenye mitandao ya kijamii, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo baadaye Lady Jaydee alihoji kuwa pengine yeye ndiye anayestahili ‘kukinukisha’ kwa kuwapeleka mahakamani wasanii walio chini ya Tanzania House of Talent (THT), Estarlina Sanga ‘Linah’ na Elias Barnaba ambao anadai aliwalipa kianzio cha shoo yake ya Mei 31, mwaka huu kisha kumchomolea dakika za mwisho

source-MPEKUZI Blog (mpekuzi.com)


 
Kumbe Clouds nao vilaza ya nn chuki binafsi tu suala hapa ni kutaka kumkomoa Jidy hawana lolote
 
Binafsi nasikiliza clouds mostly (rarely naskiza radio). Lakini hainizuii kuona kuwa mnachofanya sio sawa.

Tunachofanya mimi na nani? Mimi ni Ngabu na niko peke yangu. Usinihusishe na wengine ambao hawanihusu. Kama vile ambavyo wewe unavyoona mitazamo yako ndo nami hivyo hivyo. Naona huyo binti kachemka, anatafuta bifu kinguvu ili afufue career yake ambayo iko mahututi.

Mimi ni mnazi wa jay dee na still pamoja na bifu lenu na yeye naskiliza tu clouds kwa sababu kuna baadhi ya vitu napenda kuvisikia.

Well, good for you. You can like or love whatever or whomever.

Kwa hiyo kufanya kwenu vizuri kwenye matangazo kunaweza kuwa sawa tu na kushinda kwa ccm kwenye chaguzi. Na sio kitu cah kujivunia.

Matangazo ya biashara na CCM kushinda chaguzi havina uhusiano hata kidogo. Umechemka. Jipange upya.

Naskia p-funk nae kawananga.

So? He's just another has-been anyway. And who listens to him? You and yo'mama?

Sijui mtapeleka wangapi mahakamani. Ruge alitamka kuwa hajaliongelea suala lake na jide kwa sababu halina maslahi ya kitaifa. Na kudai yapo mengi ya kujadili zaidi yake. What is not happening?

Nimekwambia usinihusishe na wengine. "Mtapeleka" kwani mimi nina ubia na Clouds?
 
Sina bifu naye. Ni kwamba tu naona kanunua bifu ili kupromoti album yake mpya.

Sasa ili apate free publicity akaamua ku pick fight na Goliath, so to speak.

Kwa vile Clouds ni chama kubwa nadhani calculations zake ni kwamba umma utamuonea huruma, utakuwa upande wake, na kununua album yake mpya.

Her beef ain't genuine. It's phoney baloney coconut bacon.

Hivi mtu akitoa mwazzo tofauti na mtizamo wa mtu ni kuwa na bifu?jana niliongea against JD nikaambiwa eti nina roho ya korosho, wewe leo wanasema una bifu na Jide....kila mtu ana namna yake ya kuona mambo, sio lazima tuwe sawa bana...khaaa....

Jide ni kama yuko frustrated flani sasa anatafuta pa kufia......ukichunguza kwa makini madai yake hayana mshiko na huwezi kuainisha nini hasa analalamikia kutwa kucha. Kama sio kuchafua watu why toka mwanzo asiende mahakamani kuwashitaki hao ruge na jose kwamba wamemfanyia A,B,C badala yake anatumia blog na twits zake kuongea pumba zake?
 
Majomba Jide alishasema kwenye media part II itatoka Tarehe 15 na Clouds wanajua. Alisema immediately baada ya interview ya Ruge. Na Jide alisema more facts will come on 15th. Gang order no body knows kwani content za hati ya mashtaka no body knows na wala hatujui mahakama itachukua muda gani

mkuu Allien kutokana na habari nilizo zipata ni kwamba Ruge na joseph wamefungua case ya madai, wakidai kuchafuliwa na jyde na ina onekana wazi haya madai hayakusomwa leo pale na yatasomwa mei 27.
Na kinacho ni furahisha hapa walishindwa ku apply for restrain order ambayo ingemfunga mdomo jyde na ina onekana case yenyewe ndio itaanza kusikilizwa mei 27 na ndio siku atasomewa mashitaka.
 
Last edited by a moderator:
Naona huyo binti kachemka, anatafuta bifu kinguvu ili afufue career yake ambayo iko mahututi.

Hapa ndipo penye shida, si afe kivyake vyake why abebeshe watu lawama za kifo chake? ukweli jide hana jipya kwenye sanaa yake, na sanaa yake kwa mfwatiliaji mzuri haikui ...iko pale pale (monotonous) sasa anataka kuwabebesha watu mizigo ya lawama kwamba wao ndio wanaomuua kisanii....AJIPANGE UPYA HII SINGO YA KUTOKA KIRUGE NA KIJOSE HAITAHITI
 
Hivi mtu akitoa mwazzo tofauti na mtizamo wa mtu ni kuwa na bifu?jana niliongea against JD nikaambiwa eti nina roho ya korosho, wewe leo wanasema una bifu na Jide....kila mtu ana namna yake ya kuona mambo, sio lazima tuwe sawa bana...khaaa....

Sasa hata wewe shangaa!

Jide ni kama yuko frustrated flani sasa anatafuta pa kufia......ukichunguza kwa makini madai yake hayana mshiko na huwezi kuainisha nini hasa analalamikia kutwa kucha. Kama sio kuchafua watu why toka mwanzo asiende mahakamani kuwashitaki hao ruge na jose kwamba wamemfanyia A,B,C badala yake anatumia blog na twits zake kuongea pumba zake?

Mimi mpaka sasa specifically sijui anacholalamikia ni nini. Afadhali hata Sugu alikuwa analalamikia kuhusu mradi sijui wa vyandarua au sijui malaria nini nini sijui.

Lakini huyu binti mimi sijajua hasa anacholalamikia ni kipi mahsusi. Analialia tu huko kwenye twitter na facebook na kwenye kiblogu chake.

Na kama kweli angekuwa na hoja madhubuti pamoja na ushahidi wa mabaya aliyofanyiwa basi angefuata legal recourse ili kama akishinda apewe fidia. Lakini hapana, hakuthubutu kufanya hivyo. Kwa nini? Kwa sababu hata yeye mwenyewe hajui anachokilalamikia. Kachanganyikiwa tu.
 
Back
Top Bottom