Clouds Fm wamshukia Mnyika, wampuuza kwa kuchanganya mambo

Mwenye CV ya Ephraim Kibonde (kama anayo) naomba atuwekee hapa, inawezekana siyo tatizo lake ni vyeti.

Nilivyokuwa namsikiliza kwenye hiyo radio kabla sijaihama alikuwa anajiita yeye ni mwana sheria. Labda humu kuna member amesoma naye. Pia kwenye hiyo CV ongezea ni MC shughuri mbalimbali.

JF kumekuwa na kilio kikubwa cha magazeti kuandika uzushi na udaku, lakini kwenye radio hawagusii kabisa!!! Sasa hii Clauds Fm urushaji wa habari zao ni utata mtupu.
 
These are street boys, unethical & rumour hunters. As a member of JF, you, even, don't have a right to quote them. Try quoting intellectuals not every famous human.

Kama wanatusoma watarekebisha midomo;

"One must be a little foolish, if one does not want to be even more stupid." -Michel de Montaigne

Wamezoea kujikomba na sasa naamini hawana tena tabia wanayoijua.

 
These are street boys, unethical & rumour hunters. As a member of JF, you, even, don’t have a right to quote them. Try quoting intellectuals not every famous human.

Kama wanatusoma watarekebisha midomo;

“One must be a little foolish, if one does not want to be even more stupid." -Michel de Montaigne

Wamezoea kujikomba na sasa naamini hawana tena tabia wanayoijua.

 

mimi nawaita vibendera hawa jamaa wa clouds....surely I have lost interest na wao!!! hawajielewi kabisaaaaaaaa, ni upuuuuzi mtupu
 
Hawa jamaa wa clouds FM wana matatizo sana na hasa hicho kipindi cha Jahazi wanatumia lugha ya matusi na maneno ya mitaani as if inasikilizwa na wahuni wa mitaani, ilhali watu wenye heshima zetu nasi tunasilkiliza ili tupate habari, lakini matokeo yake tunakereka.
 
Huyu Kibonde ni kibonde hasa kama jina lake, yeye kama mtangazaji anatakiwa awe neutral as posible siyo kuleta ushabiki wa kitoto, sasa hivi kwenye ardhi Tanzania huko Biharamulo/Kigoma kuna msitu umejaa wakimbizi kila siku wanateka magari, kuibia wananchi na kubaka, serikali inajua na kibonde anajua, Lakini siku waje watu wa UN/wanaharakati kutengeza ripoti hawa vipbonde watakuja na kuanza upuuzi wa kukanusha
 
Hawa vibonde wa Clouds wanapenda vijana wenye akili za fiesta fiesta, hawasomi kuongeza uelewa zaidi ya kusoma habari za ligi ya England
 

Ni ukweli ukisikiliza Clouds hasa Kibonde na Garder analysis yao ni very shallow sana. Hawasomi kwa undani mambo na comments zao mara nyingi ni misdirected. Nadhani hata kwa vile wanapendwa sana na vijana, kupendwa kwao kumewafanya kiasi kuwa na ka-arrogance fulani kama walivyo Ze Commedy. Anyway kwa vile mie sio kijana tena kipindi chao nawaachia vijana.
 
Wana JF;

Napenda niwaambie kuwa kwa bahati nzuri au mbaya nimewahi kuwa karibu na Gadna na Kibonde. Naomba niwaeleze au niweke sawa mambo.

Kibonde ni mfuatiliaji mzuri wa mambo na ana upeo mzuri tu wa kutathmini mambo. Ana Secondary education lakini ninawahakikishia anawazidi hawa graduate wetu wengi wa siku hizi kwa exposure na uelewa.

Gadna sio mfuatiliaji wa mambo ila yupo exposed kwenye anga za life na starehe (muzic, cinema, sanaa kwa ujumla), hana hobby ya mambo ya kisiasa wala hayuko interested nazo, ni mfanyabiashara na mzuri kwa ubunifu.

Back to the topic, Radio kama ilivyo media yoyote, watangazaji wake wanawakilisha mawazo ya mmiliki, refer magazeti ya Mengi RA na hata Mbowe. Absalom Kibanda mlimuona nyinyi wenyewe humu.

Waandishi na watangazaji wengi bongo hawa exercise their right kwa sababu wamiliki wana ajenda zao binafsi. Mtawalaumu bure hawa jamaa kuhusu suala la CCM na serikali.

Clouds FM ni timu ya watafutaji na wasanii. Na ni watafutaji kweli kweli, lakini mnyonge mnyongeeni lakini Clouds wana entertain hasa kwa vijana. Utani na upuuzi kidogo ni moja ya entertainment yao, wanafanya maksudi kabisa sio kwamba hawana akili.

Anyway nitamtaarifu Kibonde aingie hapa ajibu baadhi ya hoja hata kama sio kwa jina lake halisi, Gadna sijui kama anajua hata JF ina exist.

FP
 
Tatizo la hawa watangazaji wa Clouds FM wanaupeo chini ya kiwango cha kati (below average) kwahiyo haya mambo ya uchambuzi wa kisiasa wangeyaacha tu! wajikite kwenye burudani zaidi..!
 
Nadhani radio zipo nyingi kama yalivyo magazeti. Unajuwa inategemea mtu unapenda kusikiliza habari za namna gani. Kama redio au gazeti linataja mambo siyoyapenda.. kwa nini usiipotezeee tuuuu. Uzuri ni kuwa redio zetu zinaweza kushika stesheni moja at a time,.. we badili frequency tu badala ya kubaki kulalamika.
 
FP,
Nayakubali sana maelezo yako. Angalia redio hii inakowapeleka vijana wetu ambao wengi wao hawana elimu na uelewa wa kutosha. Tamasha la juzi pale viwanja vya posta lilikuwa ni maangamizi kwa vijana wetu. Walilewa, wakafanya upuuzi mwingi tu.
Kukusanya pesa kwa njia hii kuna laana yake.
 


HAYO NI MAONI yako, unawezaje kuitenganisha MEREMETA na DEAL la SIlaha??????????
 

Tatizo lako ulitaka wakusomee magazeti yote mwanzo wa habari hadi mwisho na ndio maana siku hizi wamegoma soma magazeti ya wanasiasa na siasa zao kwani imekuwa ni kama kutwanga maji kwa kinu, Magazeti kwanza nayo yanatupotezea muda wetu hayana habari za maendeleo kila kukicha ni wanasiasa tuuuu. Hakuna siku yametuambia barabara ya kutoka iringa kupitia Dodoma mpaka Arusha imefikia wapi? Babati Singida nayo je??Umeme je Huko Ukerewe ni uko pale nansio tuuu na haufiki kule kazilankanda au bugorola je wakara wataupata huoumeme leo??

Sasa siwaelewi na hao wahariri wenu mtazamo wao uko wapi kimaslahii zaidi ya kisiasa ili wauze magazeti ambayo wewe unayoyalilia ati watangazaji wa asubuhi(Power Brakfast) wakusomeee kama wako darasani.

Mie naunga mkono hoja kwa Clouds FM(Power BreakFast, Jaahazi) kwa wanachokifanya wanelimisha Jamii wanatupa habari nyingi sana na wanakosowa vyema tuuu, tatizo sie wabongo hatupendi kuambiwa ukweli siku zote twapenda mambo ya kupindisha pindisha

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…