Wana JF;
Napenda niwaambie kuwa kwa bahati nzuri au mbaya nimewahi kuwa karibu na Gadna na Kibonde. Naomba niwaeleze au niweke sawa mambo.
Kibonde ni mfuatiliaji mzuri wa mambo na ana upeo mzuri tu wa kutathmini mambo. Ana Secondary education lakini ninawahakikishia anawazidi hawa graduate wetu wengi wa siku hizi kwa exposure na uelewa.
Gadna sio mfuatiliaji wa mambo ila yupo exposed kwenye anga za life na starehe (muzic, cinema, sanaa kwa ujumla), hana hobby ya mambo ya kisiasa wala hayuko interested nazo, ni mfanyabiashara na mzuri kwa ubunifu.
Back to the topic, Radio kama ilivyo media yoyote, watangazaji wake wanawakilisha mawazo ya mmiliki, refer magazeti ya Mengi RA na hata Mbowe. Absalom Kibanda mlimuona nyinyi wenyewe humu.
Waandishi na watangazaji wengi bongo hawa exercise their right kwa sababu wamiliki wana ajenda zao binafsi. Mtawalaumu bure hawa jamaa kuhusu suala la CCM na serikali.
Clouds FM ni timu ya watafutaji na wasanii. Na ni watafutaji kweli kweli, lakini mnyonge mnyongeeni lakini Clouds wana entertain hasa kwa vijana. Utani na upuuzi kidogo ni moja ya entertainment yao, wanafanya maksudi kabisa sio kwamba hawana akili.
Anyway nitamtaarifu Kibonde aingie hapa ajibu baadhi ya hoja hata kama sio kwa jina lake halisi, Gadna sijui kama anajua hata JF ina exist.
FP