Clouds Fm wamshukia Mnyika, wampuuza kwa kuchanganya mambo


Inasikitisha kwa sababu, Clouds imetokea kupendwa sana na watu wa rika zote.Tukubali kuwa wako innovative japo wanahitaji miongozo namna ya kufanya kazi zao ili kuhakikisha wanazingatia maadili hasa wakati wa kutangaza vipindi vyenye kusikilizwa na watu makini.Tatizo linakuja - nani wa kuwaongoza? Ni Joseph Kusaga au ni Ruge Mutahaba?Wanahitaji consultants wawasaidie katika mengi.Wenyewe wanaona Fiesta ndio kitu cha maana sana walichofanikiwa nacho.

Ukija kwenye hawa watangazaji wawili - Kibonde nilikuwa namheshimu sana hadi majuzi nilipomsikia akizungumzia ngono waziwazi kwenye kipindi cha Jahazi ndio nikamdharau moja kwa moja..Gardner naye hana indipendent mind na ndio maana kila mara anatafuta validation ya thinking yake kwa Kibonde.

Tukija kwenye Power Breakfast - Kipindi ni kizuri ila waache utoto maana hapo siyo mahali pake, wawaachie akina Dina Marios na Gea Habib kwenye Leo Tena wajishaueshaue.Nilishangaa kwenye PB akina Gerald wameanza kuchombezea habari kama akina Gea wafanyavyo kwenye Leo tena wakati nyimbo za taarabu zikiwarusha watu roho!

In short CLOUDS INASHUKA THAMANI WASIPOANGALIA WATASHUKA HADI WAFIKIE LEVEL YA MAGAZETI YA UDAKU YA AKINA SHIGONGO!

I hope Joseph Kusaga atapitia JF aone kukoselewa huku ili wajirekebishe.
1ST THING JOSEPH - GET SOME CONSULTANTS TO HELP YOU COZ U R GROWING FAST..SASA MNA TV....usipoangalia utaporomoka kama a pack of cards!
 
tambua wao wamelenga kundi lipi ili ujumbe wao ufike. By the way kwanini usome kila jambo lililoandikwa magazetini hata kama dhahiri shahiri halina tija kwa jamii bali kundi fulani la jamii lenye makusudio potofu. 100% clouds fm kwa hilo ingawaje kama ni siasa basi nao wana upande wanaoufagilia kama ipp wafanyavyo.

All in all ndio the hottest radio station in dar
 

Safi

mama yangu nakuunga mkono kwa maelezo uliyo yatoa hapo juu.

 
Wana JF;

Anyway nitamtaarifu Kibonde aingie hapa ajibu baadhi ya hoja hata kama sio kwa jina lake halisi, Gadna sijui kama anajua hata JF ina exist.
hahahaaaaa, jamaa anapelekwa kama bendera ifanyavyo mbele ya upepo!.
upeo mdogo sana wa kufikiri.
 
Siwezi kukaa na kusikiliza kwa makini kinachotoka kwa watangazaji hao. Kuna watu wananunulika kirahisi sana na kutumia na baadaye kutupwa. Hata uksikia wanachotangaza unaona ni much better usikilize kile kipindi cha zamani sana cha RT kilichokuwa kinaitwa mazungumzo baada ya habari.
 
FairPlayer bado sijakuelewa hapa hebu mwite mwenyewe Kibonde na gadner wake wasome kwanza hii mada ndo wakarushe hivyo vipindi vyao na wawe wanafikiri kwanza
 
HAYO NI MAONI yako, unawezaje kuitenganisha MEREMETA na DEAL la SIlaha??????????


Mkuu kandambili;

Jibu ni kuwa UNAWEZA KUITENGANISHA na vilevile UNAWEZA USIWEZE KUTENGANISHA.

Remember no research no right to speak. Ukiangalia kwa hali halisi, hisia itamtuma kila mmoja wetu kuwa Meremeta inahusika, hii hisia inakuja kutokana na dhana ya UFISADI na uendeshaji wa Meremeta na USIRI mkubwa uliopo humo ambao hata Waziri mkuu hataki kuugusia.

Ni hisia tu, ukweli haujajulikana

Hayo ndio maoni yangu.
 

To be honesty sio tu kuwa mie ni msikilizaji wao mzuri ila nilijaribu kufuatilia nami kujua kama hawa jamaaa wanegemea upande wa mtu na nkagundua sivyo


All in all ndio the hottest radio station in dar

Sio tu in Dar bali mikoa yote Radio Clouds inaporusha matangazo yake


FDR ukiona mtu anamsakama sana mtu humu ndani basi kwa namna nyingine yeye ni mlengwa husika au yukaribu na iyo issue inamgusa kwa namna fulani au!

Na nimegundua humu ndani ya JF ikirushwa Thraed ya Siasa utaona wanchagia mada ile mbaya yani watu wanapenda siasa humu ndani ya JF.

Mfano mzuri Hospital ya mwnanyamara ina scandal chungumzima wakina mama wajawazito wanakumbwa na matatizo hakua mwana JF hata mmoja esp wanoishi huko Dar kutupa the real picture hakuna zero, non. ikitokea siasa utawaona hapa point wanazo shusha teh teh
 
Kuna tetesi kuwa mmoja wao hao ni Mu-Anglikana Anglikana?

Kite;

Kama nilivyosema awali, hawa jamaa ni watu ambao nina socialize nao na nawafahamu kiasi cha kutosha. Nakuhakikishia kuwa ni wanaume rijali na hawatumii mashoga kama una maana hiyo.

Na hata uwezo wa kufikiri wanao mkubwa tu, labda ume miss point niliyoelezea mwanzoni. Tanzania media zote zinaripoti kutokana na bosi anataka au ana malengo gani, hii haiwafanyi wafanyakazi wa hizo media kutokuwa na akili.
 
in red siyo malumbano.malumbano ni kwamba wanapinga kuoanisha meremeta na uuzaji wa silaha. wanasema hakuna mausiano.Repoti ya UN imeweka wazi uusiano uliopo. ndo myika akanukuu.Wao wangethibitisha kwamba hakuna uhusiano siyo kukejeli tu.Kamahawana uelewa soma jinsi ilivyo au ruka basi.
 

Asante mkuu kama ni kweli uliyosema, naomba pia kuelimishwa Clouds ni mali ya nani hasahasa anayeimiliki?
 


Tatizo ni kutoa service bila bravery.

Ni kweli wengi wanafanya hivyo lakini ni hatari kwa akili ya binadamu kufanya mambo bila dhamila yako eti tu kwa sababu unalipwa. Baada ya muda mrefu ukiwa hivyo, hutaweza tena kufikiria unavyotaka mana hutakuwa na sehemu ulikowahi ku-test thinking yako.

Ndo yanayowapata Changu doa. Bora pesa.

Hawa akina Kibonde kama kweli ni kutimiza mahitaji ya mwajili wao bila wao kuyakubali, basi watahitaji rehabilitation centre pale watakapoamua kuwa independent.

Watajiita wasanii, right! lakini usanii siyo stupidity ya kujifanya matusi ni lugha ya kawaida kwako.
 
Joseph Kusaga and family asilimia 80 na Ruge Mutahaba 20

Sina uhakika na percentages lakini inakaribia humo humo
 
I find the two announcers with very simple minds. Their ability to analyze issues is sub zero. They don't deserve a space in our jf.
 

Kwanza nakupongeza kwa kukubali kuwa ni radio inayopendwa na watu.

....Tatizo linakuja - nani wa kuwaongoza? Ni Joseph Kusaga au ni Ruge Mutahaba?Wanahitaji consultants wawasaidie katika mengi.Wenyewe wanaona Fiesta ndio kitu cha maana sana walichofanikiwa nacho.

Kumwonoza nani na kwanini? Tatizo la Kusaga na Ruge ni lipi? wana hitaji Consultants ipi just be specific and give us precisely details ya ki consultant!
Mpwa una taaabu kweli kweli Fiesta we ndio imekukela sana? hujui kuwa ni part ya starehe? ivi umejiuliza kama kweli wewe ni msikilizaji mzuri wa Clouds FM - kipindi cha PowerBreak Fast mtangazaji mmoja alienda wapi na amerudi na kipi kipya cha kuiambia jamii??


Inamaana kwamba kibonde unamdharau sasa au ndio tuseme? tatizo la kutamka matukio ya ngono hadharani linakupashida gani mpwa? unawatoto?je swala la elimu ya ukimwi unaielimisha vipi kwa jamii inayo kuzunguka? isije wewe matendo yako yakawa ndio machafu zaidi ni kipi hakijulikani siku izi au kuwepo kwa vyombo vya habari vingi na watukujua mambo hukupenda?

Independent mind ipi iyo? ivi somo la elimu kwa jamii linakuingia akilini mwako vyema? ulitaka Gardner from no where aanze ku crush points za Kibonde? ivi nkuulize mpwa from ur heart kilichoongelewa siku hiyo hakipo kweli huko mitaani kwetu tunapo ishi au wewe waishi anga nyingine? be honesty kwa ilo!


Waache utoto upi? we ni mpenzi wa hiki kipindi au? wasema hata bonge anapo report tokea huko barabarani nae huleta utoto?
Kwa hio akina Dina Marios na Gea Habib kwenye Leo Tena ndio wao hupenda mambo ya kitoto?Kwahiyo ifikapo heka heka wewe unaziam radio husikii matukio ya watoto kuchomwa vidole mot na mama zao kunyanyaswa kwa wanawake we hii yote kwako ni utoto? kwahiyo hii ndio independent mind yako?imekutuma ivyo? watangazaji wa PB wakichombeza chombeza mambo ya kian Gea we ina huuuu?hii Radio wewe ulitaka iwe kama Radio Tanzazia (RTD) enzi izo mama na mwana, iwe kama kipindi cha mikingamo? ivi hii radio wewe hupenda kipindi gani XXL,Bambataaa?au Chombeza time cha Usiku, Habari za Michezo?


In short CLOUDS INASHUKA THAMANI WASIPOANGALIA WATASHUKA HADI WAFIKIE LEVEL YA MAGAZETI YA UDAKU YA AKINA SHIGONGO!

Kivipi inashuka thamani mkuu?
Kwani magazeti ya udaku yana shida gani mkuuu? wataka kuniambia yote yaandikwayo ni uongo au?hayo matukio yanatokea hayatokei?

I hope Joseph Kusaga atapitia JF aone kukoselewa huku ili wajirekebishe.
1ST THING JOSEPH - GET SOME CONSULTANTS TO HELP YOU COZ U R GROWING FAST..SASA MNA TV....usipoangalia utaporomoka kama a pack of cards!


Mpaka hapo alipofikia ana consultant wake na mwanasheria wake mkuu hafanyi vitu kubahatisha tuu. Mie sijaona mapungufu uliyo yafafanua hapo bari ni kutopenda vipindi furani tu kwa roho yako


 
Pole uliyetuma hii post, ulitakiwa ujiolize kati ya hawa watangazaji na mnyika nani anayeelewa anachokifanya? ulitakiwa pia ujiulize kama ulikuwa wakati wa kusoma magazeti au kupiga polojo? Ukifanya hayo utapata picha.

Pole mafisadi wamekupa kazi ngumu kweli kuwasafisha. Hatudanganyiki!!!!!!!!!!
 


Ndugu yangu, inatakiwa uwe na uwezo wa kujiajiri ndo ufikie maamuzi hayo. Wewe unajua wazi kuwa Tanzania hakuna FAIR Ground kwenye competition. Hasa ukujiajiri.

Mie siwezi kuwalaumu ingawa pia sijasema kuwa Clouds ndo inawaagiza waseme hayo, nimezungumzia media industry kwa ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…