WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
Ni ukweli ukisikiliza Clouds hasa Kibonde na Garder analysis yao ni very shallow sana. Hawasomi kwa undani mambo na comments zao mara nyingi ni misdirected. Nadhani hata kwa vile wanapendwa sana na vijana, kupendwa kwao kumewafanya kiasi kuwa na ka-arrogance fulani kama walivyo Ze Commedy. Anyway kwa vile mie sio kijana tena kipindi chao nawaachia vijana.
Inasikitisha kwa sababu, Clouds imetokea kupendwa sana na watu wa rika zote.Tukubali kuwa wako innovative japo wanahitaji miongozo namna ya kufanya kazi zao ili kuhakikisha wanazingatia maadili hasa wakati wa kutangaza vipindi vyenye kusikilizwa na watu makini.Tatizo linakuja - nani wa kuwaongoza? Ni Joseph Kusaga au ni Ruge Mutahaba?Wanahitaji consultants wawasaidie katika mengi.Wenyewe wanaona Fiesta ndio kitu cha maana sana walichofanikiwa nacho.
Ukija kwenye hawa watangazaji wawili - Kibonde nilikuwa namheshimu sana hadi majuzi nilipomsikia akizungumzia ngono waziwazi kwenye kipindi cha Jahazi ndio nikamdharau moja kwa moja..Gardner naye hana indipendent mind na ndio maana kila mara anatafuta validation ya thinking yake kwa Kibonde.
Tukija kwenye Power Breakfast - Kipindi ni kizuri ila waache utoto maana hapo siyo mahali pake, wawaachie akina Dina Marios na Gea Habib kwenye Leo Tena wajishaueshaue.Nilishangaa kwenye PB akina Gerald wameanza kuchombezea habari kama akina Gea wafanyavyo kwenye Leo tena wakati nyimbo za taarabu zikiwarusha watu roho!
In short CLOUDS INASHUKA THAMANI WASIPOANGALIA WATASHUKA HADI WAFIKIE LEVEL YA MAGAZETI YA UDAKU YA AKINA SHIGONGO!
I hope Joseph Kusaga atapitia JF aone kukoselewa huku ili wajirekebishe.
1ST THING JOSEPH - GET SOME CONSULTANTS TO HELP YOU COZ U R GROWING FAST..SASA MNA TV....usipoangalia utaporomoka kama a pack of cards!