Clouds Fm wamshukia Mnyika, wampuuza kwa kuchanganya mambo

Clouds Fm wamshukia Mnyika, wampuuza kwa kuchanganya mambo

Wakati mwingine tuwe serious, hivi kweli waweza kusikiliza habari kutoka kwa "WAFUGWAJI" hawa (KI-BONDE & GARDENER) ukaamini?....they are not source of credible information, wanachojua ni kufugwa.

Sometimes ukisikiliza kipindi cha Jahazi jioni huwezi kuamini kama hiyo radio mawingu kama ina wasimamizi wa vipindi, ni utumbo mtupu wanaongea...wakurupukaji, wasio na hoja, wanaoleta ubinafsi kwenye chombo cha habari, wenye dharau, wanaotukana hovyo redioni, wafitini,,,,huenda ikiwa ni wachawi pia.

Hoja ya Mnyika iko sawa, tatizo ni Certificate zao hawawezi ku-connect hoja....nime-attach hiyo report ya UN, tatizo je wataweza japo hata kuisoma kama sio kuielewa?kwani imeandikwa kiingereza

hahahaah kwani wana vyeti wale...? yani wale ni ma-em-siii wengine walikua wauza maduka yani ni vijana wa mtaani ambao shule imewapitia kando. sometimes wanasifia bangi kwenye radio...imagine that...

sikilizeni hata XXL hamna kitu, kama mnabisha watuwekee cv zao humu..they got nothing i wonder why people are wasting time to discuss this dirty stuff!
 
MZee Mwanakijiji alisema haya hawa wanaosema ni wanahabari waje huku JF wasome ripotyi hizi.. Mnyika ameogeza tu
 
Hata kama watangazaji wao wanaelim ndogo, one crdit lazima tuwape ni kwamba, WAPO DOMINANT KATIKA REDIO STATION ZA TZ.

Pili wanahaki ya kutoa maoni kama JF members wengine walivyomkosoa mnyika, so me hapa sioni big deal lolote.

Kama maneno haya ni ya kweli basi kikwete ni zawadi yetu watanzania kwa M.Mungu.hakuna anayelazimishwa kuwasha radio na kuchagua clouds,kwani kila familia/mtu anamiliki radio,ni mali yake,ana matakwa ya kuweka station anayotaka.

sasa kama watanzania wengi wameamua kuichagua clouds wakati hawalazimishwi,sioni kwa nini watashindwa kumchagua kikwete kwani atawalazimisha(kupitia mtandao na fedha chafu wakati wa uchaguzi ect) kufanya hivyo.

kwa wanaokerwa na clouds FM ni vema wakatafuta Station nyingine,hii itawafanya wadhamini wawakimbie na u-DOMINANT WAO UTAKWISHA.
 
Wadau JF

Mimi nina mawazo tata katika hili. Kwanza kabla ya kuchangia naomba niweke wazi kuwa currently sipo Bongo, ila ni mfatiliaji mzuri sana wa matukio yanayotokea ndani ya Bongo lakini kwa bahati mbaya source ya habari hiyo sijaipata ili niweze kuconfirm lakini kwa jinsi habari ilivyo inaonekana inanifanya niwe na side mbili; moja ni kweli Mnyika alisema hayo na kama kweli, basi ni kweli hao ''wauza sura'' walikuwa sahihi lakini walichokosea tu ni kuacha kuisoma habari hiyo kwa kigezo kuwa imechanganywa kwani watu walihitaji kusikia imechanganywa vipi? Pili ni kuwa pengine si kweli kuwa alitamka hayo (Na naomaba niweke wazi pia namkubali sana kijana) hivyo either gazeti au Radio Clouds wanatakiwa kumuomba radhi. Lakini pia wadau katika haya masuala ya siasa tusiwe na perception moja kuhusu mtu we have to think before we argue kwani perception inaweza kukupelekea katika maamuzi hasi. Ni mawazo tu!

Nawasilisha
 
Yani nakereka kila nikiingia humu naikuta hii mada ya hawa wajinga wawili inaendelea, hivi hamjui tunavozidi kuwajadili ndio wanapata kichwa hawa coz i'm sure kwamba either watakua wanaingia humu JF au watakua wanapata habari kwamba Great thinkers wanaendelea kuwajadili...pliz lets close the topic..
 
Yani nakereka kila nikiingia humu naikuta hii mada ya hawa wajinga wawili inaendelea, hivi hamjui tunavozidi kuwajadili ndio wanapata kichwa hawa coz i'm sure kwamba either watakua wanaingia humu JF au watakua wanapata habari kwamba Great thinkers wanaendelea kuwajadili...pliz lets close the topic..

Bollo,

Part ya kuwa great thinkers ni kuruhusu mjadala as long as hauna matusi yaso staha.

Kwa hiyo watu wanawajadili tu, kila mtu ana maoni tofauti.Kulazimisha kufunga mjadala bila sababu ya msingi ni kinda totalitarianism ambayo ni the opposite of anything to do with Great thinkers.

Hapa ni kama Kariakoo, Picadilly Circus na Times Square combined . Ukijaribu kuchunga paka kama ng'ombe utakufa kwa ugonjwa wa moyo.
 
Hili ni tatizo la waandishi na watangazaji wetu wengi kwa ujumla. Wengi ni vibaraka wa watu na mifumo ya wizi uliopo.
Uchambuzi wa maana haupewi kipaumbele kabisa. Vyombo vya habari kazi yao ni kuhamasisha vijana kujiunga na Bongo fleva na kuhudhuria matamasha tu. Matokeo yake vijana wote wanaamua kuwa waimbaji wa Bongo fleva.
Kusimama kwenye radio inayosikika na watu wengi kupinga kitu ambacho huna uelewa nacho ni uendawazimu.
 
Mimi bwana hata Clouds wenyewe sijui wanapatikana katika station gani . Yaani Radio hizi ni wajinga sana ukitaka kuona ni wapuuzi na si wajuzi wa mambo ngojea ikiwa inakaribia Feb 14 utawasikia wanavyo wadanganya watu kuwa ni siku ya wapendanao Duniani na hawajui hata historia basi wao makelele tuuuuuuuuuu
 
Back
Top Bottom