Ila usela mav ni tabu sana, raia tulijipinda
kumpigia kura akaondoka na tuzo 5 fadhila
alizokuja kutulipa mashabiki ni kupuliza mibangi
hadharani, 20% please just go to hell, bahati haiji
mara2. Nakumbuka miezi michache baada ya
kutwaa tuzo 5 wasanii walikuja Mbeya kwenye
fiesta akiwepo na 20%. Kwavile wasanii walikuwa
wengi na mda ulikuwa umeenda B12 alikuwa
anawacontrol wasanii wasiimbe zaidi ya nyimbo
3, but alipoingia 20% akawa anataka kuimba
nyimbo zake zote sijui maana alikuwa anaimba
nyingine ambazo hata hatuzijui, B12 akamstua
'time' amalizie awape nafasi wasanii wengine cha
ajabu jamaa akazira akaweka mic chini akasepa
bila hata kuaga mashabiki. Yaani mashabiki
tukabaki tunashangaa tu alichokifanya jamaa.
Kuanzia sikuile sitaki hata kumsikia