Clouds media na utapeli wa mchongo wa clouds kupitia kipindi cha 360

Clouds media na utapeli wa mchongo wa clouds kupitia kipindi cha 360

Ukiwa mtafutaj jaribu hata kwenye upuuzi...kuna lakujifunza....
20211104_124257.jpg
20211104_124442.jpg
image_6e4a167d-1aef-42b7-8ce0-88af28790e1120211101_131434.jpg
 
Cha msingi serikali ichukue kodi kwa sababu ni bahati nasibu kama zingine!
 
Unajua maana ya utapeli..?

Hiyo ni bahati nasibu na watu wanacheza kwa ridhaa yao wenyewe..

Acha wivu negative
Sheria zetu za jamhuri ya muungano zinasema kuna utapeli wa kuaminiwa

Sasa huu mchongo ndio utapeli wenyewe wa kuaminiwa na Ni kosa kisheria kumlaghai mtu kwa kua tu hajui
 
Wacha waliwe pesa zao na wanyolewe hadi mavuzxx nchi imejaa mapopoma wengi sana wanaotaka mafanikio ya kirahisi rahisi.
Narudia wacha waliwe hata tigo zao ziliwe tu hakuna namna wala huruma kwa hao watu.
 
ukimmenyea karanga kipofu lazima upige MLUZI......wacha watu na fweza zao.....jipambanie.....
 
Lottery zipo hadi USA acha uzwazwa mkuu..

Hapo pia serikali inachukua kodi yao..

Utapeli ni kudanganywa..hapo hamna ulilodanganywa..unaambiwa unaweza kushinda..hujaambia ukicheza ni quarantee wewe kushinda hizo mamilioni.

Hata mitandao ya simu ina hizi bahati nasibu.
 
Pamoja na ukweli kwamba matangazo ndo moja ya vyanzo vya mapato kwa media hizi lakini kwa station hii ya Mawingu daah yamezid hadi unakosa ile radha ya kusikikiza redio na hili tangazo lao mchongo pesa kila baada ya dk 5 (makisio) tangazo linajirudia.
Ubunifu kwa redio hii kadri sikuu zinavyoenda unapungua plus watu weledi wenye taaluma na vipawa vya utangazaji wamepungua ...Anyways ngoja niache makasiriko nisikilize Mashujaa Fm Sisi pamoja na wewe
 
Huo sio utapeli, ila ni kamari(bahati nasibu) kuna kuliwa na kula.
Ndio maana dini nyingi zimekemea vikali

Mfano. Qur-an 5:90
Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.

na kwanini umuonee huruma aliyekubali kutoa kipato chake kwa tamaa yake ili akizalishe kwa haraka na akijua kwa imani ya dini yake hairuhusiwi...

Usimlaumu anaekula hizo pesa ila walaumiwe wote wanaoshiriki kamari hiyo na wanaoiwezesha kufanyika.

Kamari ni kamari tusipunguze ukali wa maneno eti ni bahati nasibu

#Vijana_tufanye_kazi
#Tule_vya_halali
 
Back
Top Bottom