Alure
JF-Expert Member
- Dec 27, 2014
- 1,100
- 1,054
PA ya Kiba imelipiwa ndo maana unaona inatangazwa vya kutosha. Tuzo za Mond zinabaki kuwa kama sehemu ya habari ya chombo husika kwani ni habari za burudani kama habari zinginezo. Ndio maana zinakua na muda mchache. Zipo Band nyingi mfano wa Malaika Band au FM Academia kila wiki zinafanya ziara na kufanya show mbalimbali kwenye makumbi bshaka mnasikiaga zikitangazwa pale studio, ukilipia laki 300000 show yako wanaitengenezea tangazo na kuipromote.
Tour ya Kiba kalipa hela nyingi kidogo ndio maana imepewa nafasi kubwa inatangazwa karibia kila kipindi. Hii hata Weusi washaifanya Mwishoni wa mwaka jana hadi wakambeba dj zero na b12 Kwenye ziara yao na wasanii wengineo kibao tu wanafanya(ga). Mbona hujagi kutoa mapovu? Ni kama tangazo la kibiashara la Tigo na makampuni mengine makubwa. Mbona hujiulizi kuanzia Power Breakfast, leo tena, xxl,jahazi na amplifaya unakuta kampuni moja inapatikana karibia vipindi vyote vya siku? Ina maana wadhamini wengine walalamike kwa upendeleo? Hahahahahaha...ujinga mzigo. Kadri unavyomwaga hela ndivyo unapewa airtime ya kufamtu.
Au mlidhani hii kanuni ina aply kwa makampuni tu na sio wasanii? Au mnadhani wasanii hawafanyi biashara ya kazi zao?
Kuna muda wa kutangaza kazi za wasanii kama sehemu ya vipindi lakini vilevile kuna muda special unalipia unapewa promo kulingana na bei yako.
Habari za Diamond wanatangaza kama media nyingine zinavyomtangaza. Mbona hujiulizi huko kulikoni? Ndio maana hata Diamond mwenyewe hawezi kuja kulalamikia huu upuuzi wako. Mambo mengine wanayajua watu wa industry husika ndio maana hayawapi shida.
Msiwe mnakurupuka kutoa lawama kama hamjui mambo yanavyoenda. Uliza upewe ufafanuzi, usipolidhika ndo utoe lawama zako.
Akimaliza hyo tour tunataka mahesabu TRA wachukue kodi yao