Clouds Media ni media ya kinafiki sana

Clouds Media ni media ya kinafiki sana

PA ya Kiba imelipiwa ndo maana unaona inatangazwa vya kutosha. Tuzo za Mond zinabaki kuwa kama sehemu ya habari ya chombo husika kwani ni habari za burudani kama habari zinginezo. Ndio maana zinakua na muda mchache. Zipo Band nyingi mfano wa Malaika Band au FM Academia kila wiki zinafanya ziara na kufanya show mbalimbali kwenye makumbi bshaka mnasikiaga zikitangazwa pale studio, ukilipia laki 300000 show yako wanaitengenezea tangazo na kuipromote.

Tour ya Kiba kalipa hela nyingi kidogo ndio maana imepewa nafasi kubwa inatangazwa karibia kila kipindi. Hii hata Weusi washaifanya Mwishoni wa mwaka jana hadi wakambeba dj zero na b12 Kwenye ziara yao na wasanii wengineo kibao tu wanafanya(ga). Mbona hujagi kutoa mapovu? Ni kama tangazo la kibiashara la Tigo na makampuni mengine makubwa. Mbona hujiulizi kuanzia Power Breakfast, leo tena, xxl,jahazi na amplifaya unakuta kampuni moja inapatikana karibia vipindi vyote vya siku? Ina maana wadhamini wengine walalamike kwa upendeleo? Hahahahahaha...ujinga mzigo. Kadri unavyomwaga hela ndivyo unapewa airtime ya kufamtu.

Au mlidhani hii kanuni ina aply kwa makampuni tu na sio wasanii? Au mnadhani wasanii hawafanyi biashara ya kazi zao?
Kuna muda wa kutangaza kazi za wasanii kama sehemu ya vipindi lakini vilevile kuna muda special unalipia unapewa promo kulingana na bei yako.

Habari za Diamond wanatangaza kama media nyingine zinavyomtangaza. Mbona hujiulizi huko kulikoni? Ndio maana hata Diamond mwenyewe hawezi kuja kulalamikia huu upuuzi wako. Mambo mengine wanayajua watu wa industry husika ndio maana hayawapi shida.

Msiwe mnakurupuka kutoa lawama kama hamjui mambo yanavyoenda. Uliza upewe ufafanuzi, usipolidhika ndo utoe lawama zako.

Akimaliza hyo tour tunataka mahesabu TRA wachukue kodi yao
 
Habari wanabodi.. Leo nimeona niandike hili.

Nieleweke kabisa mimi sina timu yeyote hapa.. Hivi majuzi tulishuhudia clouds Media kujitangaza kuwa bila wao diamond asingefika pale na wanajivunia kwa hilo.. Baada ya muda akarud Ali Kiba na jinsi walivyompromote kupitia vituo vyake vya redio na televisheni tunaona ni wazi kabisa wana lengo la kuendeleza na kichochea bifu baina ya Ali kiba na Diamond.. Hayo yote yakapita ila hili la juzi limezidi, promo aliyopata na anayopata mpaka sasa Ali Kiba kupitia tour yake ya #ChekechaCHEKETOUR ni kuegemea upande mmoja kwa kumpa promo kupitia matangazo na hata post mitandaoni.. Imefika mahali wamempa hadi mtangazaji wao Mussa Hussein (mwanadaresalam) kuzunguka nae kwenye hiyo tour... Ukiangalia jana Diamond alikuwa na performance kubwa kwenye tuzo kubwa kimataifa nchini Nigeria lakini hakupata support yeyote kutoka kwenye hii Media.. Ndio maana nasema ni wanafiki kwa kuwa lengo lao sio kuongeza ushindani bali ni kukuza bifu...

muda hui maro kaingia nao ule chekechacheketua kiba kalipa hela kubwa bana
 
muda hui maro kaingia nao ule chekechacheketua kiba kalipa hela kubwa bana

Sikatai kama kalipa ni haki yake.. Nachokataa hapa ni kuzidisha hadi kwenye mitandao yao ya kijamii.. Na pia upendeleo wao upo juu wanapozungumzia kuhusu alikiba wanatumia promo na nguvu kubwa kuliko huyo hasimu wake Diamond
 
Clouds ni vibaka fm. Huo mziki wa Domoimondi ni mkusanyo wa kelele tu na hata huyo Kiba ni kawaida tu. Mziki wa prodyusa kuunga unga studio na mistari mutate aaarkhhhh chefua roho
 
Good... Unafahamu ya kwenye Industry.. Lakini una uhakika Ali Kiba kalipa hiyo pesa unayodai? Wakati anatoa wimbo wa Mwana pia alilipa promo? Siku ya show ya Fiesta kwa hy Alikiba ndo alilipa sio wao kumlipa? Ni kweli kabisa unachosema lakini tofautisha pesa wanayotoa wadhamini wa vipindi au segment kwenye kipindi na wasanii kupata promo.. Huu ni ukweli usiopingika kwamba Clouds wanakamata fursa, wakiona hela watapiga tu hela.. Ukitaka umaarufu usiokuwa na tija wanyenyekee.. Kwa promo anayopata Ali Kiba ni zaidi hata ya hayo makampuni maana katawala hadi mitandao ya kijamii... Videos na picha za show kila time... Sikatai kutoa support kwa wasanii hasa wanaofanya vizuri ila wao wanatumia chance ya bifu lao wao kuwa upande wa Ali Kiba..

Nafikiri hata hujanielewa. Ukitoa wimbo mpya unapewa PA ya bure kwani ni sehemu ya vipindi kutambulisha kazi za wasanii. Hata huyo Diamond huwa anapewa PA ya kutosha kila atoapo ngoma. Show za Fiesta alipewa PA 2. Kwanza alikua katoa wimbo mpya wa Mwana, pili Leaders ilikua ni jukumu la kila msanii kuja na mbwembwe zake wala haikua kazi ya clouds ndio maana baadhi ya wasanii walikuja na mikwara mbuzi,wengine wakaja kama wafalme, wengine kama wanajeshi na wengine wakatambulishwa na watangazaji wa vituo vingine vya radio.

Hii ni Tour nakuhakikishia na nina uhakika na ninachokisema kuwa kailipia hela nyingi ndio maana inatangazwa sana. We unafikiri kampuni gani itaingia mfukoni kumsafirisha mfanyakazi wake akahudhulie show ya msanii bila kampuni kupata chochote? Yaan wao waingie hasara kwa sababu zipi?

Weusi mwishoni mwa mwaka jana nao wamepiga Tour yao mpaka wakawa wanawatumia B12 na Dj zero mbona hamjaja kulalama?

Tatizo mashabiki mmetanguliza hisia kila sehemu linapokuja suala la clouds na wasanii ni kwasababu mlikalilishwa na baadhi ya watu toka kitambo. Hata pasipo na tatizo mnapatengenezea mawazo mgando kuhalalisha makosa. Pole sana.
 
Clouds ni vibaka fm. Huo mziki wa Domoimondi ni mkusanyo wa kelele tu na hata huyo Kiba ni kawaida tu. Mziki wa prodyusa kuunga unga studio na mistari mutate aaarkhhhh chefua roho

Chizifresh jingine hili hapa, hata halieleweki.
 
Mh! Watanzania wengi ni wabinafsi na ndo maana taifa let halifanikiwi kuwa na watu mbali mbali wenye vipaji Kwasababu mnataka mtu mmoja tu ndo aiwakilishe nchi milele na akitokea mwingine atakae onyesha nia kwamba anaweza basi huyo ni HATER. Mafanikio hawawezi kuletwa na mtu mmoja ni vema tukawasaport wote bila kujali nani kafika wapi na kwanini. Diamond keshatoka kimataifa basi aungane na wenzake ili watanzania wazidikuwa wengi kwenye mziki wa kimataifa badala ya kuweka umimi mbele, wafanyakazi hii kwa faida ya taifa.
 
Mi naona clouds inafanya kazi kwakuwa haipromoti msanii mmoja forever na hii ndo inavyotakiwa kila mtu apewe nafac ajaribu kwa uwezo wake. Tujifunze hata kwa wanaigeria c msanii mmoja anayejulikana kimataifa Ila wanasuport wote wenye kuonyesha nia na uwezo
 
Mleta mada ndio tukushangae,siku zote hizo leo ndio unagundua Clouds ni wanafiki
 
Mi naona clouds inafanya kazi nzuri kwakuwa haipromoti msanii mmoja forever na hii ndo inavyotakiwa kila mtu apewe nafac ajaribu kwa uwezo wake. Tujifunze hata kwa wanaigeria c msanii mmoja anayejulikana kimataifa Ila wanasuport wote wenye kuonyesha nia na uwezo
 
Jf kunawatu cjui wanafrika gani....tambua clouds ni media ya kibiashara hivyo kuangalia upepo ambao utakuw na soko ni jambo lakawaida....kama unatak anzisheni vituo vya habar vinavyomilikiw kwa pamoja ili kuleta usawa unaotaka...pia hatakam wanachochea bifu ilimradi inawalipa wataendelea kufanya hivyo cz ndo jinsi ya kupata kula....so funguk kifikra mwanzishaj mada sio kupiga kelele ilihali wenzak wanatengenez pesa both alikiba diamond na clouds media
 
Mleta mada una kichwa cha kuku 100%
Clouds media ni kampuni na matangazo ni sehemu ya kujiingizia kipato chao
Je unajua kua kiba kalipia yale matangazo au unaropoka tu ?
 
Clouds wanataka msanii wanayempangia nini cha kumlipa ila sio msanii wa kuwapangia nini wamlipe. Wanataka msanii anayewasujudia ili waweze kumyonya vinzuri kwenye malipo. Ukiangalia ishu ya Alikiba, anapigiwa promo sana kwa sababu wao Clouds wanajua kupitia tour zake watatengeneza pesa, ila Alikiba watamlipa kiduchu. Wanafanya hivyo kwa sababu wanajua kwa sasa Alikiba anahangaika kurudi kwenye chati kama ilivyokuwa zamani hivyo chochote watakachompangia kumlipa atakubali tu.

Kwa upande wa Diamond wameshaona hawamuwezi, hawana tena uwezo wa kumpekesha kama ilivyokuwa zamani. Leo hii Diamond focus yake ni kimataifa ambako haitaji msaada wa Clouds kuweza kufika huko. Ni bahati mbaya kwamba Clouds wana tabia ya chuki za kijinga ambazo si nzuri katika ukuaji wa sanaa ya muziki hapa bongo. Kwa level aliyopo Diamond sasa hivi ilipaswa ingekuwa changamoto kwao Clouds kuweza kuwapa moyo wasanii ambao bado hawajajulikana kimataifa ili waweze kufikia level hizo.

Clouds Media wana mambo ya Kitoto sana.
 
Habari wanabodi.. Leo nimeona niandike hili.

Nieleweke kabisa mimi sina timu yeyote hapa.. Hivi majuzi tulishuhudia clouds Media kujitangaza kuwa bila wao diamond asingefika pale na wanajivunia kwa hilo.. Baada ya muda akarud Ali Kiba na jinsi walivyompromote kupitia vituo vyake vya redio na televisheni tunaona ni wazi kabisa wana lengo la kuendeleza na kichochea bifu baina ya Ali kiba na Diamond.. Hayo yote yakapita ila hili la juzi limezidi, promo aliyopata na anayopata mpaka sasa Ali Kiba kupitia tour yake ya #ChekechaCHEKETOUR ni kuegemea upande mmoja kwa kumpa promo kupitia matangazo na hata post mitandaoni..

Imefika mahali wamempa hadi mtangazaji wao Mussa Hussein (mwanadaresalam) kuzunguka nae kwenye hiyo tour... Ukiangalia jana Diamond alikuwa na performance kubwa kwenye tuzo kubwa kimataifa nchini Nigeria lakini hakupata support yeyote kutoka kwenye hii Media.. Ndio maana nasema ni wanafiki kwa kuwa lengo lao sio kuongeza ushindani bali ni kukuza bifu...

Naomba ueleze kosa lililofanywa na Clouds maana nimesoma silioni kabisa!
 
Clouds wanafanya biashara kwahiyo hakuna suala la kumpa promo Ali Kiba hapo! Ulitaka waitangaze show ya Diamond Nigeria kwa faida ya nani au ili kiwe nini? Ili waongeze mauzo ya ma-dish ya DStV, au? Anyway, hata kama isingekuwa na faida kwa yeyote, endapo Diamond, management yake au DSTv or anyone else wangelipia matangazo, Clouds wangetangaza tu coz' wao biashara yao kubwa ni matangazo!

Kwa show ya Ali Kiba kwa sasa itakuwa ni ama management ya Kiba imelipia publicity hapo Clouds au Clouds wana mkono wao kwenye show husika kwa kuwa, hiyo ni moja ya shughuli wanazofanya... yote kwa yote, hakuna dhambi! Huwezi kusema Clouds wasipokee matangazo kuhusu Kiba kwa kuwa Kiba ana bifu na Mond au huwezi kusema Clouds wasiwe sponsor wa show za Kiba kwa kuwa Kiba ana bifu na Monds coz' ile radio ni ya kibiashara, na mwenye kisu kirefu ndie hula nyama! Aidha, wakifanya kama unavyotaka mleta mada, basi hiyo itakuwa ndo ku-promote bifu... kwanini wasihusike na show za Kiba?

Andaa show ya Diamond kisha kalipie publicity pale Clouds ukiona wamekataa, ndipo rudi hapa na habari sawa na hiyo uliyokuja nayo otherwise, tuache utoto!
 
Sikatai kama kalipa ni haki yake.. Nachokataa hapa ni kuzidisha hadi kwenye mitandao yao ya kijamii.. Na pia upendeleo wao upo juu wanapozungumzia kuhusu alikiba wanatumia promo na nguvu kubwa kuliko huyo hasimu wake Diamond
Ndugu yangu, mie ni mmoja wa mashabiki wa Diamond ambae wala sijifichi humu jamvini! Hebu nielimishe... hao Clouds kwa sasa ulitaka wafanye promo ipi kwa Diamond? Umegusia show ya Nigeria... uifanyie promo ile show ili iweje na kwa faida ya nani? By the way, ile show ya Nigeria ni ya Multichoice na washirika wake... na ni show ya kibiashara! Sasa ulitaka show ya kibiashara ya kampuni nyingine itangazwe na Clouds bure kivipi? Unadhani hao Clouds wangefanya hivyo wangekuwa wanamtangaza Diamond au wangekuwa wanaitangaza Multichoice na washirika wake?
 
Back
Top Bottom