Clouds Media ni ya kutambulishia audio wakati EATV ni kwa ajili ya kutambulisha video

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Aman iwe nanyi wapendwa
Soma kichwa cha habar hapo juu
Hivi huu utaratibu aliouweka ni nani?

Clouds media imekuwa kimbilio la wasanii kwenda kutambulisha audio zao, msanii akitoa audio huwa ana anzia mawingu kwanza ndo sehemu zingine zinafata

Lakin msanii huyo ambaye katambulishia audio yake mawingu hawez kabisa kuitambulisha video yake mawingu hata kama ni kama ni dawa

msanii akitoa video cha kwanza ni EATV, sijawahi kuona msanii katoa video halafu akaipeleka clouds video lazima ataanzia EATV then huko kunafuata

Sasa bas naomba kujua huu utaratibu nan aliuweka au ni wasanii tu wenyewe wameamua kufanya hivyo

Au Clouds ina wasikiliziji lakin haina watazamaji?
Au EATV ina watazamaji wengi sana na haina wasikilizaji?
Kwenu wadau

LONDON BABY
 
Kwanini wasipeleke Le Mutuz TV, tv bab kubwa tv ya kisasa!!!!!😀
 
IPO wazi EATV wapo very professional, kwenye TV za burudani hakuna anayewakaribi. Ila kwa redio Clouds wako poa sana. Hivyo basi kwa TV EATV the best Clouds tv haoni ndani. Na kwa redio Clouds wako the best kuliko EA radio. Ingawa EA radio walikuwa bora sana, sahizi na wao wameingiza uswahili, ingawa kipindi cha jioni cha Drive mi ni msikilizaji wao namba moja. Nakipenda sana
 
Ni kweli kabisa sijui ni kwanini labda Ruge alishawaambia wao ndio lazima wabikiri nyimbo zote mpya
 
True kabisa..Ea radio walikuwa vizuri sana,wakaanza mambo ya ajabu ajabu ya kuondoka watangazaji wao makini refer George bantu,Mamybaby,Kenedytheremedy na Dj sinyorita..kumwondoa Anna peter,Sam Missago kwenye redio na kuwepo kwenye tv tu..sijui hawalipi au tatizo liko wapi?
 
Hlo halina ubish ndo hvo
Audio wakianzia eatv inabuma
Video wakianzia mawingu
lazma itabuma sasa

Sasa ilikuokoa hilo lazma
Utaratibu ufwatwe
 
Kweli.... clouds TV haona swagger zozote..... pia haifiki nchi nyingi zaid
 
Ni rahisi sana.
CLOUDS ni radio ya burudani yenye wasikilizaji wengi kuliko washindani wake
EATV ni TV ya burudani yenye watazamaji wengi kuliko washindani wake
Kila msanii anataka kujitangaza sehemu atakayosikilizwa au kutazamwa na watu wengi zaidi
 
Ni rahisi sana.
CLOUDS ni radio ya burudani yenye wasikilizaji wengi kuliko washindani wake
EATV ni TV ya burudani yenye watazamaji wengi kuliko washindani wake
Kila msanii anataka kujitangaza sehemu atakayosikilizwa au kutazamwa na watu wengi zaidi


Nakubaliana na wewe.


Vipi kati ya Clouds tv na TVE ipi inawatazamaji wengi ? Mimi baa zote mtaani hadi club tv zao huwa nakuta wameweka TVE , labda am wrong
 
Nakubaliana na wewe.


Vipi kati ya Clouds tv na TVE ipi inawatazamaji wengi ? Mimi baa zote mtaani hadi club tv zao huwa nakuta wameweka TVE , labda am wrong
Rahisi sana Chief.. Wengi huweka tv e kwa sababu ya vipindi vya muziki mfululizo.. Na /tv e wameamua kuwekeza huko..na maeneo ulotaja muziki "non stop" ndo mahali pake sahihi.

Clouds tv ni wakongwe zaidi ya tv e. Hilo ni faida kwao

Style ya kurusha matangazo yao ni ya kibunifu inayofanya wasipoteze watazamaji wao

Pia clouds tv inabebwa sana na brand ya clouds fm.. Automatically wafuatiliaji wa clouds fm wanajikuta wanafuatilia clouds tv

Asilimia kubwa ya wasikilizaji wa efm ni wanaofuatilia vipindi vya michezo. Wakati tv e ni wafuatiliaji wa muziki.

Clouds tv ina watazamaji wengi zaidi kwa sasa kwa sababu ya coverage kubwa. Imefika maeneo mengi zaidi kuliko tv e..

Angalia idadi ya wadhamini kwenye vipindi vya clouds na tv e. Utagundua clouds tv ina wadhamin wengi.Siku zote Wadhamini wanaweka mpunga wa ktosha kwenye vipindi vyenye watazamaji wengi

Kiujumla angalia idadi ya vipindi vinavyofuatiliwa na watu wengi kwa kila tv, ukubwa wa eneo ambalo tv zote mbili zimekwishafika na style ipi ya urushaji wa matangazo inawavutia watu wengi zaidi kwa tv zote mbili Utagundua ipi ina watazamaji wengi zaidi

Hata hivyo tv e bado inakuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…