Clouds Media ombeni msamaha watanzania kwa kudanganya zoezi la uokoaji kariakoo limesimama

Maswala kama haya hayataki utani wazee, hata siasa hazihusiki - ni kosa baya media kubwa hivi kutoa taarifa kama hii alafu watu wapo ndani na wanapitia mtandaoni japo kwa shida
 
Wakuu, naombeni video za polisi wakifanya uokoaji 🙏 nna kazi nazo
 
Nawakumbusha tu aliekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera kipindi Precision air inadondoka ndo huyo huyo ambae sasa hivi ni RC wa Dar maana Kagera aliwatoa hofu wananchi kwamba Wana mawasiliano na ndani ya ndege, hivyo hata huku atatoa takwimu za mchongo
 
Maswala kama haya hayataki utani wazee, hata siasa hazihusiki - ni kosa baya media kubwa hivi kutoa taarifa kama hii alafu watu wapo ndani na wanapitia mtandaoni japo kwa shida
Serikali inaweza sema kazi ya uokoaji inaendelea ila ukiwepo eneo la tukio huoni kinachoendelea
 
Wizara ya habari ichukue hatua stahiki kwa vyombo hivi vinavyopenda kuripoti taharuki badala ya tukio
Ila sometime credibility ya baadhi ya vyombo vya habari Tanzania inatia mashaka Sana

Hasa hivi vijiredio vyenye vijana wengi wanataka habari itakayowapa engagement na sio news

Aise Kuna tatizo
 
Wanaofanya uokoaji ni wananchi au mamlaka za serikali maana vyanzo vingi vinaonyesha zoezi kimesitishwa hivyo tueleze wanaookoa ni wadau au vikosi vya uokoaji maana kama wadau pekee maana yake vikosi vimesitisha zoezi
 
Watu wanaendelea kuokolewa muda huu navyopost hapa..nyie endeleeeni kufanya siasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…