Clouds yatoa ufafanuzi malipo ya TSh milioni 629 yaliyotajwa na CAG

Meneja wa fedha wa kampuni ya Clouds Media Group, Issa Masoud amesema walitoa vielelezo vyote ikiwa ni pamoja na stakabadhi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia malipo ya Sh 629.7 milioni kwa ajili ya matangazo ya tamasha la urithi mwaka 2018.

Masoud ametoa ufafanuzi huo leo Alhamisi Aprili 8, 2021 katika kipindi cha Traffik Jamz kinachorushwa na redio Clouds saa chache baada ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kueleza kuwa Clouds ililipwa kiasi hicho cha fedha lakini hakukuwa na risiti zozote za kielektroniki zilizotolewa kuthibitisha malipo husika.

Katika ripoti hiyo ya CAG, imeeleza kuwa televisheni ya Clouds walilipwa Sh 629.7milioni na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Sh201.4 milioni kwa ajili ya kuonyesha matangazo ya tamasha hilo.

Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG, Charles Kichere amesema kodi ya zuio ya Sh31 milioni na Sh10 milioni kutoka Clouds na TBC hazikukatwa kutoka katika malipo hayo.

"Wizara haikutimiza wajibu wake katika kukata hiyo kodi ya zuio, vilevile sikupewa ushahidi ukionyesha kuwa manunuzi ya huduma za matangazo kutoka TBC na Clouds yalipatikana kwa ushindani ulio sawa.”

“Pia nilibaini Sh487 milioni zilipelekwa kwenye taasisi saba kwa ajili ya utekelezaji wa tamasha hata hivyo hakukuwa na nyaraka zilizowasilishwa kwa wakaguzi kuthibitisha matumizi hayo,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
Haya maelezo angempa CAG alipoonana nao...
 
Clouds acheni usanii mtajitetea TAKUKURU huko wakati Kigwangala atakapokuwa anahojiwa soon or later

Nitag siku Kigwa au taasisi yeyote ile ikihojiwa let alone kuwajibishwa.

Ripoti ya CAG ni useless haina impact yeyote ile, ni routine tu kila mwaka muda kama huu kuizungumzia na kuisahau after a month.
 
Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa??

*Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.
*
Muda utaongea .
Kweli kichwani umejaa
 
Hivi ni kwann sisi waizi wa kuku tunapigwa sana mvua mahakaman lakin Hawa wabadhilifu wa pesa nyingi za serekali huwa hawachukuliwi hatua yoyote? Yani inachukuliwa kama kashfa tu na mwisho wa siku wanaachwa wanaendelea kuwa wanasiasa au wanaachana na siasa na wanaendelea kula maisha kwa pesa za ufisadi, inawezekana uwizi kwa wanasiasa kuiba pesa nyingi unaruhuswa kisheria
 
Meneja wa fedha wa kampuni ya Clouds Media Group, Issa Masoud amesema walitoa vielelezo vyote ikiwa ni pamoja na stakabadhi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia malipo ya Sh 629.7 milioni kwa ajili ya matangazo ya tamasha la urithi mwaka 2018.

Masoud ametoa ufafanuzi huo leo Alhamisi Aprili 8, 2021 katika kipindi cha Traffik Jamz kinachorushwa na redio Clouds saa chache baada ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kueleza kuwa Clouds ililipwa kiasi hicho cha fedha lakini hakukuwa na risiti zozote za kielektroniki zilizotolewa kuthibitisha malipo husika.

Katika ripoti hiyo ya CAG, imeeleza kuwa televisheni ya Clouds walilipwa Sh 629.7milioni na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Sh201.4 milioni kwa ajili ya kuonyesha matangazo ya tamasha hilo.

Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG, Charles Kichere amesema kodi ya zuio ya Sh31 milioni na Sh10 milioni kutoka Clouds na TBC hazikukatwa kutoka katika malipo hayo.

"Wizara haikutimiza wajibu wake katika kukata hiyo kodi ya zuio, vilevile sikupewa ushahidi ukionyesha kuwa manunuzi ya huduma za matangazo kutoka TBC na Clouds yalipatikana kwa ushindani ulio sawa.”

“Pia nilibaini Sh487 milioni zilipelekwa kwenye taasisi saba kwa ajili ya utekelezaji wa tamasha hata hivyo hakukuwa na nyaraka zilizowasilishwa kwa wakaguzi kuthibitisha matumizi hayo,” amesema.

Chanzo: Mwananchi

Wasimsingizie Mtani wangu Late Ruge.
 
Amepewa lakini akapuuza
Mmehamia kwenye kusingizia sasa
 
Hivi ni kwann sisi waizi wa kuku tunapigwa sana mvua mahakaman lakin Hawa wabadhilifu wa pesa nyingi za serekali huwa hawachukuliwi hatua yoyote? Yani inachukuliwa kama kashfa tu na mwisho wa siku wanaachwa wanaendelea kuwa wanasiasa au wanaachana na siasa na wanaendelea kula maisha kwa pesa za ufisadi, inawezekana uwizi kwa wanasiasa kuiba pesa nyingi unaruhuswa kisheria
Mbowe alipokula michango ya wabunge mlimchukulia hatua gani?
 
Kuna shida hapa Wizara ilipewa taarifa juu ya utata wa malipo hayo na wakashindwa kujibu ndani ya muda. Sii busara Clouds TV and Radio kwenda kwenye vyombo vya habari na kujibu tuhuma hii kwani hazikuwalenga wao. Huu ni utovu wa nidhamu, CAG hajibiwi hivyo!
 
TRA fuatilia muamala huo hamkupata gawio lenu sasa lala mbele na Clouds TV wazitapike.
 
Kuna shida hapa Wizara ilipewa taarifa juu ya utata wa malipo hayo na wakashindwa kujibu ndani ya muda. Sii busara Clouds TV and Radio kwenda kwenye vyombo vya habari na kujibu tuhuma hii kwani hazikuwalenga wao. Huu ni utovu wa nidhamu, CAG hajibiwi hivyo!
Clouds hawapo tayari kuchafuliwa
 
Taasisi iliyotuhumiwa haiwezi kujisafisha, hapo wanatafuta pabliki simpathi tu......wasubilie mamlaka itakayokabidhiwa kufuatilia ndiyo italeta majibu.

Wenzao wasafi na tibisi wako kimya, wao wanajifanya kupiga kelele.......mara zote ukiona mtuhumiwa anapepesa pepesa ujue nikweli kaiba
 
Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa??

*Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.
*
Muda utaongea .
Usiwe mwakilishi wa umma, hayo ni maoni yako na sema atakutana na nguvu yako. Umma uutajao ni huo alio kuwa anawadhalilisha kwa kuwaita wanyonge, kisa amewafunga midomo? Hao alio wanyima uhuru wa kuchagua viongozi wawatakao?
 
Hivi CAG alikagua Clouds media? Kama sio wao hawatakiwi kujibu, hata utaratibu wa kujibu hawajui. Kama wana any evidence wapeleke kwa aliyekaguliwa apeleke kwa CAG mambo yaishe sio kupiga porojo za maneno tu.

Back
Top Bottom