Clouds yatoa ufafanuzi malipo ya TSh milioni 629 yaliyotajwa na CAG

Clouds yatoa ufafanuzi malipo ya TSh milioni 629 yaliyotajwa na CAG

Njia rahisi siyo kusema, ukaguzi wa kihasibu siyo kama kufanya shopping soko la Kingalu, wao Clouds wanazo copy za malipo na makubaliano na makato ya kodi e.t.c wapeleke nakala,
Siyo kuita waandishi wa habari na kujibu kwa maneno bila ushuhuda, waweke vielelezo vyao.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
CMG warudishe fedha ya watanzania zaidi ya milioni 600 ambayo hakuwa na risiti wala invoice. warudishe haraka hiyo hela vinginevyo wataabika zaidi ya hapo.
 
Clouds tena! Wazee wa fursa.
Ndio anajibu ripoti ya CAG au alikuwa anapiga stories news room, kumbe yuko live
 
Usiwe mwakilishi wa umma, hayo ni maoni yako na sema atakutana na nguvu yako. Umma uutajao ni huo alio kuwa anawadhalilisha kwa kuwaita wanyonge, kisa amewafunga midomo? Hao alio wanyima uhuru wa kuchagua viongozi wawatakao?
Hata mpinge vipi hamtakaa mzikwe kishujaa kama JPM
 
Hivi ni kwann sisi waizi wa kuku tunapigwa sana mvua mahakaman lakin Hawa wabadhilifu wa pesa nyingi za serekali huwa hawachukuliwi hatua yoyote? Yani inachukuliwa kama kashfa tu na mwisho wa siku wanaachwa wanaendelea kuwa wanasiasa au wanaachana na siasa na wanaendelea kula maisha kwa pesa za ufisadi, inawezekana uwizi kwa wanasiasa kuiba pesa nyingi unaruhuswa kisheria
Ndiyo maana China wanafanyaga yao.. hawanaga discussion na mwizi, mla rushwa na wengine wa kufafana na hao... ALIYEHUSIKA NA UWANJA WA KWA MKAPA, KESHATANGULIZWA MAANA HAUKUTAKIWA KUWA VILE ULIVYO, ULIKUWA DESIGNED UWE ZAIDI YA VILE... alioshirikiana nao huku kwetu wanapeta, ukute hata kaburi la mwenzao hawajui lilipo..!!
 
Na chadema nao wameiba huku
Ndo mnapochemkiaga... hamna hoja... YAANI HAPO UNATAMANI USEME CAG NI WA CHADEMA NA AMETUMWA NA MABEBERU... ila namna ya kuiweka ndo ngumu. haiwekeki...
 
Hivi CAG alikagua Clouds media? Kama sio wao hawatakiwi kujibu, hata utaratibu wa kujibu hawajui. Kama wana any evidence wapeleke kwa aliyekaguliwa apeleke kwa CAG mambo yaishe sio kupiga porojo za maneno tu.
USISHANGEATCRA WAKASEMA NAO... MAANA HAWAJABALANSI STORI... WANGEMUITA NAYE ASEME YAKE
 
Ndo mnapochemkiaga... hamna hoja... YAANI HAPO UNATAMANI USEME CAG NI WA CHADEMA NA AMETUMWA NA MABEBERU... ila namna ya kuiweka ndo ngumu. haiwekeki...
Chadema ni wezi
 
Ifahamike kuwa ripot ya CAG inakuwa ni uhalisia wa kila jambo. Wakaguzi hawaondoki sehemu pasipo kupata maridhiano ya pande zote mbili kukubali.

Mfano mimi nimenunua kitu cha laki 3 na sina risiti. Mkaguzi akija kuuliza risit ipo wapi, nikamwambia sina au nikatoa ambayo ni nje ya utaratibu. Basi mkaguzi yeye ataandika ule uhalisia.

Ndo maana huwezi ukakuta mabenki, taasisi, vyama n.k vinapinga uhalisia wa ripoti ya mkaguzi.

Ifamike pia, kabla CAG hajasoma hizo hesabu zake, mashirika kama ATCL, TPA wanajua kabisa ni madudu gani katika mashirika yatakwenda kuwekwa wazi. Wanajua kabisa kuanzia sehemu ya kwanza mpaka ya mwisho.

Ni aibu kubwa kwa taifa kumjibu CAG kienyeji enyeji tu.
Hili liko wazi kuwa mkaguliwa huwa na nafasi ya kufuta hoja za ukaguzi zinazojitokeza iwapo atatoa au kuwasilisha majibu sahihi ya hoja/queries zilizoibuliwa ikiwa ni pamoja na viambatanisho vinavyohitajika.

Sidhani kama CAG anaweza kuhitimisha hoja ambazo zina majibu sahihi kulingana na mahitaji ya kiukaguzi.
 
Katika ripoti hiyo ya CAG, imeeleza kuwa televisheni ya Clouds walilipwa Sh 629.7milioni na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Sh201.4 milioni kwa ajili ya kuonyesha matangazo ya tamasha hilo.

Sasa ndugu zangu, hivi hayo matamasha huwa yana effect kiasi cha kutumia fesha nyingi kiasi hiki?..

He hilo tamasha ni la uzalishaji au ni destructive?.

Je @Hkkigwangalla analiongeleaje hilo suala maana yeye alikuwa ni moja ya wahusika wa tamasha hili alikuwa Waziri Mwenye dhamana.
 
Clouds Media wakae kimya kabisa wasithubuti kujadili ripoti ya CAG. hawana uhalali wa kujadili kwa sababu wanaguswa na kashfa ya kukwapua milioni 600. hivyo ni wachafu.
 
Back
Top Bottom