Kwanza unabidi ujue idadi ya timu zinazohitajika.
Ukishajua hilo utaona hoja yako ya kusema kigezo cha kucheza hayo mashindano ni kuchukua ubingwa ni hoja ya kijinga.
Kwasababu kwanza unapaswa uelewe kuwa wakati timu zingine zinatafuta nafasi ya kupita, tayari kuna timu zilishakuwa qualified hazihitaji kufanya jitihada zozote ili zifuzu.
Sasa unaposema kigezo ni mpaka timu ichukue ubingwa, umefikiria hatma itakuwaje ikiwa moja ya hizi timu zilizo qualify zikachukua ubingwa??
Yani Wydad au Al Ahly akichukua ubingwa ina maana watakuwa peke yao kwasababu wengine kushiriki ni mpaka wangechukua ubingwa??
Jibu rahisi ni kuwa iwapo itatokea Wydad na Al Ahly hawajachukua ubingwa basi hiyo nafasi ya mtu kupita kwa kigezo cha ubingwa ndio itakuwa applied.
Vinginevyo maana yake ni point ndio zitazoamua kwenye hizo nafasi mbili zilizobaki na ndio hapo mantiki ya kuletwa orodha ya timu 12 zenye wingi wa point inapojidhihirisha