Club ya Real Madrid imetangaza rasmi kumsajili Kylian Mbappe kwa mkataba wa miaka mitano

Najaribu kuwaza itajuwaje.. Mbappe na vini wanakuwa bora zaidi wakitokea upande wa kushoto, aidha LF ama LS, huku kwingine watacheza tu ila ubora ni wakitokea kushoto. Binafsi yangu nikiambiwa nianze na yupi mitaanza na mbappe hilo halina ubishi ila vini nae si mchezaji wa kuanzia benchi.
 
Kaka Kwani kuna ubaya gani kusifia Madrid ilivyo Hii leo!!?

Hao uliowataja walikua wanashindana na kina Nani?

Kipindi hicho Seria A timu zipo Moto, EPL ndio usiseme, Ufaransa walikuepo Lyon Watu wa maana kabisa, Germany vile vile, sasa utalinganisha na kizazi hiki?

Saivi Timu nyingi zipo Hoi Mwenye afadhari ni city, kwahyo tusiisifie na kuitabilia makubwa Madrid Hii et kisa kina flani walishindwa???

Hata Perez angekua na mawazo Kama hayo basi asingekua anasajili majina makubwa kisa kina De Lima walifeli.
 
Epl haikuwa ya moto kivile, Italy palikuwa pamoto sana chini ya utawala wa Ac Millan ya Maldin, Sedoff, Dida, pipo inzagh, shevchenko, kaka, rui Costa 😁,, lakin cha ajabu walipotea Kwa Liverpool final ya miujiza 😁
 
Mbappe na Vini mi naanza na Vini kushoto. Mbappe akae kati. Bado nina mashaka na uwezo wa Mbappe nje ya klabu inayoabudiwa na wengine wote huku yeye akiabudiwa na timu nzima.

Kiukweli angekuja EPL ndiyo ningezidi kutamani kumuangalia atafanya nini huku kwenye malow block ya kila aina
 
 
Ngoja tuone nani atakiwasha zaidi kati yake na vini jr maana kijana wa kibrazil kishaanza kuweka utawala,ninachokiona ni hawa vijana wawili kuleta umimi ndani ya klabu....kila mmoja akitaka ufalme isitoshe mbappe alikuwa kishaaminishwa ni bora zaidi duniani.
 
Epl haikuwa ya moto kivile, Italy palikuwa pamoto sana chini ya utawala wa Ac Millan ya Maldin, Sedoff, Dida, pipo inzagh, shevchenko, kaka, rui Costa 😁,, lakin cha ajabu walipotea Kwa Liverpool final ya miujiza 😁
Hata EPL Kaka kulikua Moto Tazama 2005 kachukua Liverpool,
2006 Arsenal kafika final, 2007 LiIverpool final,
2008 Chelsea Vs Manchester United final, 2009 Manchester final.
Cheki mambo hayo.
 
Nilitaka kuandika ichi ulicho andika mkuu umeniwahi
 
Kwa sasa mkuu wasipochukua ni uzembe sababu kwa sehemu kubwa sana ulaya vipaji vya mpira vimeshuka. Zamani ukiiona Madrid ya moto, basi Barcelona, Man U, Liverpool, AC Milan n.k unawakuta wa moto pia sio kama sasa hivi timu za moto zinajulikana kirahisi sana, ukimtoa Madrid mwamba mwingine ni Man City.
 
Hata EPL Kaka kulikua Moto Tazama 2005 kachukua Liverpool,
2006 Arsenal kafika final, 2007 LiIverpool final,
2008 Chelsea Vs Manchester United final, 2009 Manchester final.
Cheki mambo hayo.
mie ni shabik mkubwa wa man UTD, lakin tulimtoa Barcelona Kwa mbinde sana, goal la scholes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…