Club za mpira wa miguu duniani zinazoongozwa kwa mfumo wa hisa ni hizi

Club za mpira wa miguu duniani zinazoongozwa kwa mfumo wa hisa ni hizi

Yanga naona mnatoa mapovu, nyie mmeanza kutumia huo mfumo lini?? Kwa hiyo Madrid wakishinda sababu ni mfumo kama wenu na nyie mnajiona mmefanikiwa??
Simba Sc daima inaweka mifano ya kufuatwa hapa EA.
Tumeshawazoea ,endeleeni kujitekenya na kujichekesha baadae mtaanza kulialia kama kawaida yenu
 
Siku zote Tope Fc ndio muanzilishi wa mambo ya ajabu ajabu hapa nchini, mfumo wa kutafuta ubingwa FIFA muazilishi ni Tope Fc na kwa taarifa fupi tu ni kwamba haujafanikiwa, mbwembwe za kusajili timu ya bilioni 1.3 muanzilishi ni huyu huyu ila mpaka leo unaelekea kufeli, mbwembwe za ujenzi wa uwanja wa Bunju na uwepo wa nyasi bandarini umeshafeli rasmi.
Kwani hamjui pia kuwa Tope Fc ndio muanzilishi wa kanuni ya mchezaji mwenye kadi za njano 3 kuchagua mechi? Au hamjui kuwa hawa ndio waanzilishi wa kufoji mikataba ya wachezaji wake hasa vijana wadogo?
Halafu huyu mdhamini mpya mmesahau kuwa alikuwepo Malikia wa Nyuki aliyeaminika angemfunika Bakhresa na Manji ila sasa hivi yuko Oman kwa mumewe anapika? Hizi mbwembwe za hisa ni mbwembwe tu ila timu ni ile ile na watu wake ni wale wale Rage aliotuambia kuwa ni mbumbumbu.
 
Timu ambazo ni mabingwa wa kihistoria kwenye ligi zao unazijua...?Bibi Hindu Fc akili zenu kawashikia Manara [emoji23][emoji23]
 
Sio kweli Barcelona na majority ya timu za Spain zinaongozwa kwa mtindo wa wanachama. Wanachama ndio wenye sauti na ndio maana zina mafanikio makubwa kuliko hizo za hisa.
Hata timu za Germany ni hivyo hivyo tu including Bayern Munchen.
Ujerumani kuna sheria inaitwa 50+1 rule, ambapo asilimia 50 ya hisa inatakiwa kumilikiwa na wanachama wale ambao ni season ticket holder, hii ndio inafanya wanachama ama mashabiki kuwa na nguvu sana kwenye club za ujerumani tofauti na ligi zingine
 
1. SIMBA SC (Tanzania).
2. Arsenal FC (England)
3. Man Utd (England)
4. AC Milan (Italy)
5. Barcelona (Spain)
6. Bayern Munich (Germany)

Club zinazoendeshwa kwa mfumo wa wanachama ni;

1. Yanga SC(Dar Tz)
2. Kiluvya Utd (Pwani Tz)
3. Kauzu FC(Dar Tz)
4. Mlalakua (Dar Tz)
5. Mbao FC(Mwanza Tz)
6. Misosi FC(Dar Tz)
7. Majimaji FC(Songea Tz)
8. Coastal Union (Tanga Tz)
9. Lipuli FC (Iringa Tz)
Mmeanza Kuwanga
 
madrid na barcelona ni za wanachama na zikitaka mchezaji ni timu chache zinashindana nazo, timu za Ujerumani asilimia 51 lazima zimilikiwe na wanachama tatizo kwa timu zetu mpaka mtunza fedha unataka awe mwanachama badala ya kuajili watu wenye uweledi na taaluma zao
 
1. SIMBA SC (Tanzania).
2. Arsenal FC (England)
3. Man Utd (England)
4. AC Milan (Italy)
5. Barcelona (Spain)
6. Bayern Munich (Germany)

Club zinazoendeshwa kwa mfumo wa wanachama ni;

1. Yanga SC(Dar Tz)
2. Kiluvya Utd (Pwani Tz)
3. Kauzu FC(Dar Tz)
4. Mlalakua (Dar Tz)
5. Mbao FC(Mwanza Tz)
6. Misosi FC(Dar Tz)
7. Majimaji FC(Songea Tz)
8. Coastal Union (Tanga Tz)
9. Lipuli FC (Iringa Tz)


Umeanza kuangalia mpira lini kiongozi? Barcelona ina wanahisa Ila team ya members au wanachama.
 
Tatizo mbumbumbu Fc wanamategemeo makubwa sana ndani ya muda mfupi wamesahau kuwa sio pesa yote anayotoa Mo ndani ya mwaka mmoja.
Haiwezekani yote akafanya ndani ya mwaka mmoja lkn nashangaa wao wanawaza mwakani watakuwa na uwanja na kila kitu mpk kujifananisha na kina TP Mazembe nk!
 
Matopeni nayo imo au ndiyo kwanza inaingia with unexpected results?
Niambie Real Madrid ipo kwenye mfumo gani. Ndiyo Club iliyoshinda zaidi Champions League including back to back

Hawa Jamaa wa msimbazi huwa sijui wanatumiaga visigino kufikiri...😀😀
 
Yanga naona mnatoa mapovu, nyie mmeanza kutumia huo mfumo lini?? Kwa hiyo Madrid wakishinda sababu ni mfumo kama wenu na nyie mnajiona mmefanikiwa??
Simba Sc daima inaweka mifano ya kufuatwa hapa EA.

Yanga SC hakuitaji mfumo wa hisa kubeba NDOO 26 za ligi kuu bara!
 
Imeuzwa mpaka na wanachama wake

Mleta mada atambui kuwa hata yeye mwenyewe kama shabiki aamekwisha nunuliwa kwa zile hisa za Bil 20. Jamaa kainunua klabu na mashabiki wake wote!

Angetaka Klabu pekee nadhani angebaki Singida UTD.
 
1. SIMBA SC (Tanzania).
2. Arsenal FC (England)
3. Man Utd (England)
4. AC Milan (Italy)
5. Barcelona (Spain)
6. Bayern Munich (Germany)

Club zinazoendeshwa kwa mfumo wa wanachama ni;

1. Yanga SC(Dar Tz)
2. Kiluvya Utd (Pwani Tz)
3. Kauzu FC(Dar Tz)
4. Mlalakua (Dar Tz)
5. Mbao FC(Mwanza Tz)
6. Misosi FC(Dar Tz)
7. Majimaji FC(Songea Tz)
8. Coastal Union (Tanga Tz)
9. Lipuli FC (Iringa Tz)
Huu ndio ugomvi wa ngumi kabisaaa[emoji2]
 
Simba SC (Tanzania) thaman yake ni 39 bilion?. Kwa sasa imeuzwa kwa MO labda itaendelea na zaidi kama atawaondoa wafuatao;

1. Hans pope
2. Haji Manara
3. Kaburu

La sivyo watamtafunia hizo 20 bilion na barua za fifa zisizo na majibu
 
Naipenda simba lakin hapo mleta mada umetupiga fix kidogo. Mapenzi yakizidi sana ni maradhi kaka.
 
Back
Top Bottom