Siku zote Tope Fc ndio muanzilishi wa mambo ya ajabu ajabu hapa nchini, mfumo wa kutafuta ubingwa FIFA muazilishi ni Tope Fc na kwa taarifa fupi tu ni kwamba haujafanikiwa, mbwembwe za kusajili timu ya bilioni 1.3 muanzilishi ni huyu huyu ila mpaka leo unaelekea kufeli, mbwembwe za ujenzi wa uwanja wa Bunju na uwepo wa nyasi bandarini umeshafeli rasmi.
Kwani hamjui pia kuwa Tope Fc ndio muanzilishi wa kanuni ya mchezaji mwenye kadi za njano 3 kuchagua mechi? Au hamjui kuwa hawa ndio waanzilishi wa kufoji mikataba ya wachezaji wake hasa vijana wadogo?
Halafu huyu mdhamini mpya mmesahau kuwa alikuwepo Malikia wa Nyuki aliyeaminika angemfunika Bakhresa na Manji ila sasa hivi yuko Oman kwa mumewe anapika? Hizi mbwembwe za hisa ni mbwembwe tu ila timu ni ile ile na watu wake ni wale wale Rage aliotuambia kuwa ni mbumbumbu.