CNN: 73% ya Wamarekani wanataka Biden asigombee 2024, hawaelewi nchi inakoelekea chini ya Biden

Nawewe print uone utafika wapi, kwanini Russia au China wasiprint wakaizidi Marekani au hawataki. Kumbe nabishana mtu asiyejua hata basics za uchumi.
Germany ilivyoprint hela zake au Zimbabwe ilivyoprint sana noti zake walifikia wapi?
Tupe Somo boss!
 
Wakati wa Bush US ilitumia dollar Trillion 8 kwa vita vya Afghanistan na Iraq, dollar million 300 kila.siku huko Afghanistan kwa miaka 20. Hizo dollar bilioni 40 za Biden anazozitoa kidogo kidogo ni tone tu katika bahari ukilinganisha na Bush. Bush pia ndiye aliyeondoka akiacha mgogoro mkubwa wa uchumi wa 2008 ambao ulikuja kutatuliwa na Obama.
 
Hakuna rais goigoi katika historia ya Marekani kama huyu Biden, eti wakati Putin anataka kuivamia kijeshi Ukraine akawaondoa wale wanajeshi 2,000 wa Marekani waliokuwa nchini Ukraine. Bure kabisa.

Putin hupenda kufanya upumbavu wake chama cha Democratic kikiwa madarakani lakini hawezi kuthubutu wakiwemo Republicans.

Miezi kadhaa nyuma nilisikia mbunge moja wa Russia akidai kwamba ni wakati sasa kwa Russia kudai Marekani iwarejeshee Alaska hata ikibidi kwa nguvu.

Huyu Biden sio mtu serious hata akiongea anaonekana kuongea kimzaha mzaha tu hafai kabisa kuwa rais wa nchi ya Marekani hata yule makamu wake anamzidi. Bure kabisa.
 
Jamaa hajui Bush aliharibu uchumi. Katika ratings za marais wa Marekani huyo Bush Jr na baba yake wote wako mbali mwishoni uko. Kuanzia miaka ya 1970s mwishoni mpaka sasa ukiuliza Wamarekani marais wao wanaowakubali ni kina Ronald Reagan, Bill Clinton, Obama. Hata Trump anakubalika kuliko Bush
 
Tupe Somo boss!
Maelezo ya kawaida ni hivi. Fedha ina sifa kuu ya kuwa ngumu kupatikana (scarcity), ukichapisha noti nyingi zinazagaa mtaani mwisho wa siku mwenye elfu kumi kumi 100 tiyari anajiona ana milioni moja hivyo hata asipofanya kazi anaweza kula mwezi mzima. Hapo hapo wauzaji wanaona hela zipo wanapandisha bei wakijua watauza, huyo mwenye milioni aliyopata kirahisi ananunua ovyo kwa kuwa anayo hela.
Mwishowe uzalishaji unapungua na bei zinapanda (inflation). Gharama za maisha zinapanda na thamani ya fedha inashuka badala utumie 2,000 kununua mkate unatumia zaidi.

Maelezo mengine. Kila nchi inatengeneza hela itumie ndani, sio nje. Ukitoa hela zako zikatumike nje unakuwa na options mbili. Ya kwanza uchapishe hela nyingi zaidi kufidia zilizopo nje ya nchi, ya pili uchukue hizo hela zilizo nje urudishe ndani.
Option ya kwanza ni sawa na ya juu ya kufyatua makaratasi mengi, ni ujinga.

Option ya pili ndicho Marekani ufanya, uchukua hela zake zilizo nje na kuzirudisha. Kuchukua hizo hela hawawaambii tuleteeni hela zetu bali wanalazimika kuzalisha wauze nje ili mnunue kwa hela zao. Hili nchi ifanye hivi ni LAZIMA iwe na uzalishaji mkubwa, uchumi mkubwa, teknolojia na vitu vingi. China na Japan huwa zinafanya devaluation ya hela zao kukwepa kulazimika kuzirudisha zikitoka kwenye mzunguko ndani ya nchi. Ndio maana Japan ile Yen yao inalingana thamani na shilingi ya Kenya, sio kwamba hawawezi kuzidi ila ikijaribu kukua Benki Kuu yao inafanya strategies inarudi kwenye level fulani. Wakifanya hivyo wanaondoa utegemezi wa watu nje ya nchi ndio pale tunalazimika kutumia sanasana USD, Euro au Pound.

Marekani inalazimika kuwa na jeshi kubwa na ulinzi imara, kufuata sheria na kuwa na mambo yaliyonyooka ili nchi ziiamini na kutunza fedha kwa USD kama reserve. Faida yake ni kwamba Marekani inaweza kukopa muda wowote ule kwa haraka na gharama nafuu kwa kuwa karibia nchi zote duniani zimetunza hela yao ya akiba kwa dola za Kimarekani. Na mifumo ya fedha wao ndio hasa wanalinda na kusimamia kwa gharama kubwa.

Anayesema wanafyatua tu hela naye afyatue aone. Kwamba nchi zote duniani ni wapumbavu kuwa na foreign reserve kwenye USD, yani hawaamini usalama wao wenyewe kuliko wanavyoamini usalama wa Marekani. Alafu mtu anakuja anasema eti itakuwa third world country
 
Uko Manungu ila unahoji rais wa US alivyopatikana! Waafrika ingekuwa tunahoji vile mambo yetu yanavyoendelea ungekuwa tuko mbali zaidi. US ni kama alishamalizana na mambo yote ya msingi kwenye dunia hii, sasa wanawekeza kwenye sayari nyingine.
Sisi tuna miaka around 50 ya uhuru tunakimbizana na matundu ya vyoo na tohara za watu wazima.
 
Tuliwaambia Biden hakushinda uchaguzi amesaidiwa kupita na morons and stooges wa Shetani a.k.a NWO na hivyo Trump kaporwa ushindi,hawakutuelewa.Ngoja wapate joto ya jiwe na bado.

Tusubiri Marekani in the coming 4 weeks Diesel fuel iishe,mmm,Marekani itakuwa hell on Earth.Wakati huo pia hapatakuwa na chakuka,watu watakuwa wanakufa,inflation itakuwa at all time high ,gas prices nazo at all time high,pesa haitakuwepo kwa hiyo Wamarekani hawataweza kulipa utility bills na pango!!!!!Aisee,Marekani
itakuwa kilio na kusaga meno.Yetu macho.Yajayo Marekani yanatisha,yes,all because of the stupidity of Americans,but most importantly,kwa kuwa wamempa Mungu kidogo na kumkumbatia Shetani.Ndio,Shetani hana cha bure.
 
Shukrani!!!
 
Heheeee
Na ipo siku watairejesha tuu hata kwanguvu yaani nisuala la muda tu
Kiufupi linapokuja suala la RUSSIA hao NATO wanakua wapole
Sio REP wala DEMO
Mkae kwakutulia vijana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwanini US vitu bei juu nauliza tu nasehem nyengine huko kwenye EURO POUND nk vitu bei ghali sanaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…