Maelezo ya kawaida ni hivi. Fedha ina sifa kuu ya kuwa ngumu kupatikana (scarcity), ukichapisha noti nyingi zinazagaa mtaani mwisho wa siku mwenye elfu kumi kumi 100 tiyari anajiona ana milioni moja hivyo hata asipofanya kazi anaweza kula mwezi mzima. Hapo hapo wauzaji wanaona hela zipo wanapandisha bei wakijua watauza, huyo mwenye milioni aliyopata kirahisi ananunua ovyo kwa kuwa anayo hela.
Mwishowe uzalishaji unapungua na bei zinapanda (inflation). Gharama za maisha zinapanda na thamani ya fedha inashuka badala utumie 2,000 kununua mkate unatumia zaidi.
Maelezo mengine. Kila nchi inatengeneza hela itumie ndani, sio nje. Ukitoa hela zako zikatumike nje unakuwa na options mbili. Ya kwanza uchapishe hela nyingi zaidi kufidia zilizopo nje ya nchi, ya pili uchukue hizo hela zilizo nje urudishe ndani.
Option ya kwanza ni sawa na ya juu ya kufyatua makaratasi mengi, ni ujinga.
Option ya pili ndicho Marekani ufanya, uchukua hela zake zilizo nje na kuzirudisha. Kuchukua hizo hela hawawaambii tuleteeni hela zetu bali wanalazimika kuzalisha wauze nje ili mnunue kwa hela zao. Hili nchi ifanye hivi ni LAZIMA iwe na uzalishaji mkubwa, uchumi mkubwa, teknolojia na vitu vingi. China na Japan huwa zinafanya devaluation ya hela zao kukwepa kulazimika kuzirudisha zikitoka kwenye mzunguko ndani ya nchi. Ndio maana Japan ile Yen yao inalingana thamani na shilingi ya Kenya, sio kwamba hawawezi kuzidi ila ikijaribu kukua Benki Kuu yao inafanya strategies inarudi kwenye level fulani. Wakifanya hivyo wanaondoa utegemezi wa watu nje ya nchi ndio pale tunalazimika kutumia sanasana USD, Euro au Pound.
Marekani inalazimika kuwa na jeshi kubwa na ulinzi imara, kufuata sheria na kuwa na mambo yaliyonyooka ili nchi ziiamini na kutunza fedha kwa USD kama reserve. Faida yake ni kwamba Marekani inaweza kukopa muda wowote ule kwa haraka na gharama nafuu kwa kuwa karibia nchi zote duniani zimetunza hela yao ya akiba kwa dola za Kimarekani. Na mifumo ya fedha wao ndio hasa wanalinda na kusimamia kwa gharama kubwa.
Anayesema wanafyatua tu hela naye afyatue aone. Kwamba nchi zote duniani ni wapumbavu kuwa na foreign reserve kwenye USD, yani hawaamini usalama wao wenyewe kuliko wanavyoamini usalama wa Marekani. Alafu mtu anakuja anasema eti itakuwa third world country