Vita ya kiuchumi na China Marekani haijashindwa popote. Taja kampuni ya China iliyowekewa vikwazo na ikaendelea kuteka soko duniani. ZTE iko wapi hadi leo watu hawaijui, Huawei iko wapi hadi tenda za 5G karibia zote Ulaya imepoteza na kwenye global shipment ya simu haipo hata top 7 hata kwao China haipo top 3 wakati ilikuwa ya kwanza. Kwani Marekani kashindwa nini kwenye trade war. Hali mbaya ya US kiuchumi unaipimaje.
Marekani haipo katika vita ya Ukraine. Haipo kabisa, kutoa vidola bilioni moja moja na units kadhaa za silaha usidhani vinaathiri chochote kwenye uchumi wake. Narudia kuwasisitiza ni mwaka 2020 hapo ambapo Chairman wa Federal Reserve aliidhinisha kutoa dola trilioni 2 kama stimulus ya uchumi kutokana na COVID-19. Marekani inatoa kama dola bilioni 5 kila mwaka kwa Israel miaka nenda rudi, inatoa bilioni kadhaa kwa Egypt kila mwaka, inatoa billions kwa nchi tofauti tofauti. Hiyo 2035 ni mapema sana kusema Marekani itafeli, bado ipo sana