Simba ndio wa kwanza kumtaka Conte na mshenga alikuwa kipa wao Camara. Camara alifanya kazi yake ya ushenga vizuri sana na kila kitu kila poa. Kiufupi Simba walikuwa na nafasi kubwa ya kumpata lakini kilichowakwamisha ni mfumo wao wa kizamani wa usajili ambao unapitia mlolongo mrefu na mbaya zaidi ni maelewano hafifu kwa hivi sasa kati Mwekezaji na mwenyekiti wa wananchama. Shida ilikuja pale kwenye malipo hapo ndio Hersi alipita katikati ya Mangungu na MO kilichofuata huko Simba kila mtu kavurugwa mpaka wengine wanasema eti Kagoma ni mzuri kuliko Conte na wengine wamechanganyikiwa labisa wanatafuta assist na magoli aliyofunga Conte wanajisaulisha kuwa huyo jamaa ni kiungo mkabaji.