Coastal Union 0-2 Yanga | Ligi Kuu Bara | Sheikh Amri Abeid

Coastal Union 0-2 Yanga | Ligi Kuu Bara | Sheikh Amri Abeid

Bangala kachezewa Rafu mbaya sana

Mtenje Albano alistahili Red card kapewa ya njano pamoja na Yanick Bangala

Dk ya 11


Coastal 0 Yanga 1
Yannick kayataka mwenyewe kwenda kutafuta Kadi iliyomsaidia refa kubalance Kadi. Vinginevyo Kadi nyekundu ilikuwa inamhusu Mtenje.
 
Ni weekend tena. NBC Premier League inaendelea ambapo Wagosi wa Kaya, Coastal Union watashuka dimbani kuwaalika Mabingwa watetezi wa taji, Yanga katika dimba la Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika dimba hilo mwezi wa saba mwaka huu katika mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation ambapo Yanga walibuka na ushindi.

Je leo Juma Mgunda ( Guardiola Mnene) ataweza kuwadhibiti tena Yanga? Tukutane hapa saa 10:00 jioni.

Utabiri wangu: 1-1

=======

00' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo, Coastal union VS Yanga

01' Aziz Ki anaachia mkwaju wa kwanzo uliolenga goli, mlinda mlango Mahmud anasimama imara. Coastal union 0-0 Yanga

04' ⚽ Benard Morisson anaandika bao la kwanza kuitanguliza Yanga, akiunganisha pasi maridadi kutoka kwa Jesus Moloko. Coastal Union 0-1 Yanga

07' Yanga wanapata nafasi nyingine lakini Moloko anapaisha juuuuuuu. Mpira uliingizwa kwenye box na Benard Morisson.

10' Yannick Bangala yuko chini baada ya kusiginwa na Juma, nahodha wa Coastal Union. Bangala anamsukuma Juma.

11' 🟡Wote wawili wanapewa kadi ya njano

14' Coastal wanaachia mkwaju wa kwanza uliolenga goli kwa shuti la mkwaju wa adhabu ndogo kutoka kwa Betran, Mshery anakamata mpira barabara.
Leo kichaa Morisson kaona mwezi
 
Back
Top Bottom