Coastal Union yatoa tamko kuwa haina mkataba na Kocha Mgunda

Coastal Union yatoa tamko kuwa haina mkataba na Kocha Mgunda

Aibu kubwa mno. Kocha wa timu inayoshiriki ligi kuu, kuazimwa kwwnda kuwa kocha wa timu nyingine inayocheza Ligi kuu. Acha kuhamisha magoli, kasome taarifa ya CEO, amewashukuru viongozi wa Coastal kwa kukubali kuwaazima
Unashindwaje kusoma barua ya coast union , unanilazimisha nikasome barua ya CEO wa Simba ,mgunda alikuwa coast au Simba?Tumia akili vizuri huyo CEO wa Simba anaijua coast kuliko viongozi wa coast wanaosema mgunda alimaliza mkataba na walikuwa kwenye mazungumzo?Narudia Tumia akili.
 
Mikataba ya wachezaji na Makocha yote Ipo pale Tff, sasa coast na Simba kutofautiana kwenye maelezo ndio izo chupri za Tff.Tff ukweli wote wanaujua ila shida inakuja Mwenyekiti wa Coast ni Simba, Karia, Simba.Kidau Simba Sasa watafanyaje.
 
Imewakataa vipi?
IMG-20220908-WA0002.jpg
 
Wamewakata? Hali zao zikoje? Vipi damu imevuja sana au?
 
Kwa hiyo kelele zote za jangwani and their allies zilikuwa za kujifurahisha tu Simba haina kosa lolote Mgunda hakuwa na mkataba
 
Hii ni janja janga baada ya YANGA kuingilia kati. Coastal Union na Simba ni Club pendwa za Rais msomalia, W. Karia. Anajua kabisa, hizo club 2 zote zina stahili adhabu kali. Hivyo hii barua ya Coastal kukanusha kuwa hawana mkataba na Mgunda ni janja janja na uhuni kutaka kukwepeshwa rungu na Karia.
Kawaida makocha wote hutuma CV zao mapema kabla ya msimu kuanza. Je hadi ligi kuanza Coastal Union walituma CV ya kocha yupi ili hali huyu Mgunda ndie alikaa kwenye mechi zote za Yanga msimu huu??

Ingekuwa kwa Yanga!! Kocha huyo angefungiwa mwaka 1.
 
Hivi mechi ijayo ya Simba vs Coastal Union Mgunda atasimama kama Coach wa Coastal Union? Possibly yes; ni kweli pengine hakuna sheria wala kanuni iliyo kiukwa lakini katika utamaduni wa mpira ni sahihi? Naamini Mgunda ameenda Simba kwa nia njema kabisa kuwasaidia lakini inaleta ukakasi ukizingatia kwa sasa tuna vimigogoro vingi. Kwa maslahi ya muda mrefu ya hivi vilabu viwili itakuwa vema Mgunda abaki Simba walau mpaka msimu huu uishe vinginevyo itabidi itumike nguvu nyingi sana kuwaaminisha watu kuwa hakuna upangaji wa matokeo.
 
Back
Top Bottom