KERO Coaster zinazotoa huduma Masasi - Tunduru zimekuwa kero kwa kusimama kila Kituo kama daladala

KERO Coaster zinazotoa huduma Masasi - Tunduru zimekuwa kero kwa kusimama kila Kituo kama daladala

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Tupelo_lei

New Member
Joined
Jul 12, 2026
Posts
1
Reaction score
0
Nimekuwa nikikumbana na changamoto kubwa katika usafiri wa Costa (mini bus) kati ya Masasi na Tunduru, umbali wa takribani kilomita 195.

Badala ya kutoa huduma ya safari ya masafa marefu, Costa nyingi husimama karibu kila eneo kama daladala, hali inayofanya safari inayopaswa kuchukua muda mfupi kuchukua zaidi ya saa sita. Hii husababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na kuongeza muda wa safari bila sababu za msingi.

Tunaomba Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) iingilie kati na kupitia utaratibu wa utoaji wa leseni kwa Costa zinazofanya safari za masafa marefu. Kwa safari za kuanzia kilomita 100 na kuendelea, tunashauri zipewe masharti yanayofanana na mabasi ya masafa marefu badala ya kufanya kazi kama daladala.

Hatua hiyo itasaidia kuboresha huduma, kupunguza muda wa safari na kuwaondolea abiria usumbufu wanaoupata mara kwa mara.
 
Uko sahihi mkuu, U
Huo umbali wa Masasi - Tunduru Hauna tofauti kubwa na Mtwara - Masasi (KM 201) ila hizi Costa Huwa zinasimama Kila Kijiji au kituo. Kama ni Abiria mwenye harakati zako za haraka Go and Return inakuwa ni Shida kubwa kuwa nje ya muda
 
Back
Top Bottom