Coca Cola Company wamewezaje kuendesha biashara duniani kote bila kumiliki kiwanda wala magari ya kusambaza soda zao tofauti na Pepsi?

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
Nafikiri wengi wetu mmewahi kusikia na hata kutembelea viwanda vya kutengeneza soda za Coca Cola kama kile cha Coca Cola Kwanza pale Mikocheni, DSM, Bonite Bottlers pale Shiri Matunda, Moshi, Kilimanjaro na Nyanza Bottling Co, Ltd Mwanza.

Basi ujue Coca Cola company ambayo makao makuu yake yako Downtown Atlanta, GA, Marekani sio wamiliki wa viwanda hivyo. Wamiliki wa viwanda hivyo ni wadau ambao wamelipia leseni kwa Coca Cola Company kutengeneza na kusambaza soda za Coca Cola.

Coca Cola Company huwaita Bottling Partners. Wapo zaidi ya 200 duniani na wanamiliki viwanda zaidi ya 950 duniani kote.

Coca Cola Company wanafanyaje nao biashara? U.S Coca Cola HQ wao huwapa kwanza leseni ya trade mark kutumia nembo (brand) ya Coca Cola halafu Coca Cola Co, wanawauzia tu
  • Concetrates​
  • Beverage bases​
  • Syrups​

Kwa hiyo jukumu la
  • Kutengeneza
  • Packaging
  • Kutangaza
  • Kusambaza kwa wateja zaidi ya bilion 2 kwa siku duniani kote
Linabaki kwa Bottling Partners hapa tunazungumzia akina Coca Cola kwanza, Bonite Bottlers na wengine duniani. Kwa hiyo Coca Cola Company hawamiliki, hawa-manage wala ku-control bottling companies.

Hayo ni mambo ambayo Coca Cola Company iliyo na makao makuu Marekani hayawaumizi kichwa na wamesave billions of money.


Ni mchezo rahisi sana ambao hata bilionea Warren Buffet ambaye pia ni mwanahisa kwenye kampuni hiyo aliwahi kumwambia Bill Gates
:​

"Even a ham sandwich could run Coca-Cola"
Warren Buffet


Jinsi Coca Cola wanapiga pesa kwa kuuza syrup kwa bottling partners hii inaitwa The Syrup Secret:
Concentrate cost: $2.50
-Water & packaging (bottler pays) = Final product: $10+

Coca-Cola margin: 80%+
Bottler margin: 15%


FUN FACT: Coca-Cola sells 2.1 billion drinks every day.

Yet they:
Don't make the drinks
Don't own the factories
Don't handle distribution
Don't even bottle them

Present in 200+ countries
$46B annual revenue
Still worth >$280B.

Wakati makampuni mengi makubwa duniani yakitumia mabilioni ya pesa ili kuwafikia wateja wao worldwide, upande wa Coca Cola wamedominate global distribution without owning anything. They own the 'brand name' and the 'syrup secret'
 
Bilionea Warren Buffet na kampuni yake ya Berkishire Hathaway atabaki kuwa miongoni mwa wanahisa bora zaidi kutokea duniani anajua wapi pa kuwekeza ambako hakuna risk.​

"Nobody buys a farm based on whether they think it's going to rain next year. They buy it because they think it's a good investment over 10 or 20 years."
—Warren Buffet​
 
Umesahau Nyanza Botling ya Mwanza
 
Soma kuhusu "Franchise".
 
Inaitwa Franchise business
Franchise business kwangu naona ni nzuri kuliko company owned business. Kwanza kufungua branches kwa company owned business ni gharama kubwa sana. Wakati yule wa franchise anachohitaji ni kuwauzia tu wengine leseni

Faida nyngine unayemuuzia leseni (franchee) atapambana ili awin market pale alipo ila upande wa pili ni sawa na kusema anakupambania wewe

Unakuwa kama middleman tu hutasikia suala la kufirisika
 
Sasa Mnaonaje wachumi Tusiwekeze kwenye STARLINK kwa Mfumo huu wa Francise?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…