Coca Cola Company wamewezaje kuendesha biashara duniani kote bila kumiliki kiwanda wala magari ya kusambaza soda zao tofauti na Pepsi?

Coca Cola Company wamewezaje kuendesha biashara duniani kote bila kumiliki kiwanda wala magari ya kusambaza soda zao tofauti na Pepsi?

Safi sana
Kwa sasa Coca Cola wanauza soda zaidi ya bilioni 2 kwa siku

Mwaka wa kwanza Coca Cola ilipoingia sokoni waliuza chupa 25 tu mwaka mzima

Changamoto zimewakomaza mpaka kufikia hapo walipo

Hii inatukumbusha Never give up every challenge is a gift without challenge we wouldn't grow
 
Kwa Maelezo zaidi ya kinacho fanyika tafta hii movie
Screenshot_20231227-101250_TikTok.jpg
 
Sasa Mnaonaje wachumi Tusiwekeze kwenye STARLINK kwa Mfumo huu wa Francise?
Kabla ya kuondoka alie kuwa waziri wa habari Nape alisema Starlink haijaingia Tanzanis kwa sababu ya kutokukamilisha vigezo vya usajili

Ila kwa kenya una register kwenye kampuni y starlink unapewa device uwe distributor kama wakala wa decoder wanavyofanya kazi
 
Huu mfumo unauonaje?
Mwanzo kipindi unaingia mapokeo yalikua makubwa kwa vile price ya vifurushi ilikua cheap ukilinganisha na internet service provider wengine

Competition ikawa kubwa baina ya starlink na safaricom ( router) . Hali iliofanya wateja kuihama safrcom. Ndipo safaricom ikaingia ubia na starlink sahvi ndo distributor wakubwa wa hizo device kupitia mawakala wao
 
If you can't beat them
Join them
 
Nafikiri wengi wetu mmewahi kusikia na hata kutembelea viwanda vya kutengeneza soda za Coca Cola kama kile cha Coca Cola Kwanza pale Mikocheni, DSM, Bonite Bottlers pale Shiri Matunda, Moshi, Kilimanjaro na Nyanza Bottling Co, Ltd Mwanza.

Basi ujue Coca Cola company ambayo makao makuu yake yako Downtown Atlanta, GA, Marekani sio wamiliki wa viwanda hivyo. Wamiliki wa viwanda hivyo ni wadau ambao wamelipia leseni kwa Coca Cola Company kutengeneza na kusambaza soda za Coca Cola.

Coca Cola Company huwaita Bottling Partners. Wapo zaidi ya 200 duniani na wanamiliki viwanda zaidi ya 950 duniani kote.

Coca Cola Company wanafanyaje nao biashara? U.S Coca Cola HQ wao huwapa kwanza leseni ya trade mark kutumia nembo (brand) ya Coca Cola halafu Coca Cola Co, wanawauzia tu
  • Concetrates​
  • Beverage bases​
  • Syrups​

Kwa hiyo jukumu la
  • Kutengeneza
  • Packaging
  • Kutangaza
  • Kusambaza kwa wateja zaidi ya bilion 2 kwa siku duniani kote
Linabaki kwa Bottling Partners hapa tunazungumzia akina Coca Cola kwanza, Bonite Bottlers na wengine duniani. Kwa hiyo Coca Cola Company hawamiliki, hawa-manage wala ku-control bottling companies.

Hayo ni mambo ambayo Coca Cola Company iliyo na makao makuu Marekani hayawaumizi kichwa na wamesave billions of money.

Ni mchezo rahisi sana ambao hata bilionea Warren Buffet ambaye pia ni mwanahisa kwenye kampuni hiyo aliwahi kumwambia Bill Gates
:​

"Even a ham sandwich could run Coca-Cola"
Warren Buffet

Jinsi Coca Cola wanapiga pesa kwa kuuza syrup kwa bottling partners hii inaitwa The Syrup Secret:
Concentrate cost: $2.50
-Water & packaging (bottler pays) = Final product: $10+

Coca-Cola margin: 80%+
Bottler margin: 15%

FUN FACT: Coca-Cola sells 2.1 billion drinks every day.

Yet they:
Don't make the drinks
Don't own the factories
Don't handle distribution
Don't even bottle them

Present in 200+ countries
$46B annual revenue
Still worth >$280B.

Wakati makampuni mengi makubwa duniani yakitumia mabilioni ya pesa ili kuwafikia wateja wao worldwide, upande wa Coca Cola wamedominate global distribution without owning anything. They own the 'brand name' and the 'syrup secret'
Mbona hili ni jambo la kawaida sana kweye ulimwengu wa biashara. Bila kuwasahau akina Pepsi na KFC
 
Mwanzo kipindi unaingia mapokeo yalikua makubwa kwa vile price ya vifurushi ilikua cheap ukilinganisha na internet service provider wengine

Competition ikawa kubwa baina ya starlink na safaricom ( router) . Hali iliofanya wateja kuihama safrcom. Ndipo safaricom ikaingia ubia na starlink sahvi ndo distributor wakubwa wa hizo device kupitia mawakala wao
so wameshindwa kupambana nae wameungana nae!
 
Hiyo ndio power of branding

Uber ni kampuni kubwa ya Tax duniani ila haimiliki Taxi vehicle hata moja

Hata kampuni kubwa za consultancy kama PWC huwa zinauza majina tu kwa watu.

Hata kina Nike huwa wanauza brand tu. Wao wenyewe hawatengenezi raba hata moja
 
Big businesses karibu zote zinatumia hiyo system (franchise), na they are in control 99%, wanakuazima tuu kutumia brand name na standards zote, production, advertisement, distribution etc utafanya unachoambiwa na mpaka mkopo wa kujenga kiwanda watakupa, na wana uwezo kuchukua license yao anytime ukivuruga, uzuri wanakupa monopoly na power kwa sababu ya brand
 
Back
Top Bottom