Hafla ya makabidhiano ya eneo hilo ilifanyika katika ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, ambapo Mkurugenzi Mkongwa alikabidhi rasmi eneo hilo kwa kampuni ya Coca-Cola Kwanza kwa ajili ya kuanza ujenzi wa soko maalum litakalowahudumia wanawake wajasiriamali wa Mama Lishe wa eneo hilo.
Mradi huu ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kuimarisha wanawake wajasiriamali na kuchangia maendeleo ya kijamii katika Manispaa ya Morogoro.
Katika hafla hiyo, pia walihudhuria maafisa waandamizi kutoka Manispaa ya Morogoro pamoja na wawakilishi wa Coca-Cola Kwanza.