Cocacola kubandika majina ya watu bila ruhusa/malipo, Jacline Wolper aomba wanasheria kuingilia kati

HarakatiNews

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Posts
218
Reaction score
187


Kampeni mpya ya Vinywaji Baridi ya Coca cola Kutumia Majina ya watu maarufu na Mastaa wa filamu Nchini na Kuipa jina la #shareacokeTz imeanza kulalamikiwa baada ya mmoja wa wigizaji Maarufu hapa Nchini Tanzania JACKLINE WOLPER ambaye jina lake limewekwa katika makopo hayo kudai ni utapeli kwani hakujulishwa na hakulipwa lolote.

Hapa chini ni Andishi lake katika mtandao;

"habari Followers pamoja na wa Tanzania wote ambao naamini huwa mnaingia katika page yangu ya insta. Nimepokea zawadi hii ya coca cola kwa siku 6 , Na sio kwamba sikutaka kupiga picha kama wenzangu au ku post kama wenzangu , nilikuwa natafakari Kweli Kampuni kubwa ya Kitaifa Na Kimataifa inaweza kutumia gharama kubwa kuandika majina Yetu bila kuchukuwa hata nafasi na heshima kubwa tuliyonayo kutushirikisha tu katika makubaliano ya kuandika majina Yetu Katika Makopo Yao.

Maana Naamini maFan's wa woolper wangeweza kushare na coca cola kutokana Jina Langu kuwa label katika makopo yao. Sasa Naamini tuna wanaharakati, wabunge, wanaSheria pamoja na serikali ambao huwa wanafwatilia wale wauza CD wa kariakoo basi Naomba Juhudi hizi mzihamishie huku katika kampuni hii kubwa ya Kimataifa coca cola ili kutetea haki za Wasanii na sio kudhalilishwa kwa kiasi hiki jamani. sijui kama wasanii wenzangu walilipwa siwezi kuwasemea lakini haya ni mawazo yangu binafsi. #shareaCokeTz"

CHANZO: Harakati news
 
1) Hilo jina la Wolper ni jina lake kweli?

2) Kama ni jina lake, nchi nzima hakuna mwingine mwenye hilo jina?

3) Ni kweli kabisa kuwa Coca-Cola iliandika tu hayo majina bila hata kuwasiliana na hao wasanii?

4) Coca-Cola wameshatoa le tamkoz lolote kuhusiana na hilo suala?
 
Hii ni kwa tz tu maana yalianza mabango ya biashara bila malipo na kwa kutokujuwa au ulimbukeni watu wakaona sawa tu kuwekewa bango la TIGO au Airtel kwenye biashara zao huku wenzao wakijitangaza na kupata mabilioni ya pesa, na sasa watu wanafurahia na coca wanapiga bao.
 
Juha huyu anafikiria kwa kutumia tumbo
 

Hii issue ya kulalamikia majina ya kwenye makopo ya Coca bila kuchukua hatua zozote za kisheria naona ndo kuzidi kuipa promo ya bure, nadhani ndio sababu hadi leo hii hawajatoa tamko lolote ili waendelee kupata free promo.
 
wolper bana... Njaa kali.. Sasa simple kweshen ana hati miliki ya hilo jina???? From there ndo unaweza ku'claim... Ingekuwa picha sawa.. Ila jina.. No way.. Sio registered brand.. Hakuna mwana wa sheria atakayeshulika na upuuzi huo.. Ndo maana kila siku mnashauriwa fanya jina lako kuwa brand na lisajili.. Kama unaoona wolper wapo wengi we ongeza tu iwe woolper kuleta utofauti then sajili... Mbweha wewe!!!!
 
Juha huyu anafikiria kwa kutumia tumbo

Kweli kabisa....na huyo mwanasheria wake atakuwa kihiyo/ kishoka kwani hilo jina lake ameliwekea kinga kisheria kuwa halitakiwi kutumika mahala pengine popote isipokuwa mpaka atapojisikia yeye huyo "mvujo" ? aache ubwege asidhani coca -cola wameanza kufanya biashara jana au juzi , hiyo kitu ya majina hata china na ulaya huko inatumika na wala hakuna longo longo.
 
Ye alilinunua wapi mpuuzi tu huyu au wazazi wake ndo walilitoa mbinguni.. mpuuzi kabisa kwa hiyo mi naitwa kevin nikikuta jina nikawashtaki bonite???? Jinga sana hili ..kuna vibinti vimetoka sitimbi vimekkuja mjini kwao vilikuwa vinaitwa raheli vimefika vimegundua kwa kizungu ni rechel navyo vitaenda kushtaki sasa ehh?? Pumbav kabisa na mi lips yake utadhani yule nanii wa gombe (makalio )...
 
Hii issue ya kulalamikia majina ya kwenye makopo ya Coca bila kuchukua hatua zozote za kisheria naona ndo kuzidi kuipa promo ya bure, nadhani ndio sababu hadi leo hii hawajatoa tamko lolote ili waendelee kupata free promo.

Kuna uzi mmoja nimewauliza sana watu kwa nini hawaendi mahakamani kama kweli kuna exploitation imetokea?

Hawana majibu!

Wamebaki kulialia kwenye twitter na instagram.
 
Judith sio brand name ila lady jay dee na brand



Hilo wolper sio brand name kwani kuna wolper kibao hapa duniani.
 
We unaona ni sawa kutumia majina yao kuuza soda bila chochote? sasa fikiria nani juha zaidi?

Yeye alilitoa wapi??? Hawa ndo nawafananisha na jirani yangu mmoja nilitaka kuvuta umeme kutoka kwenye nguzo akanambia nimlipe nusu ya bei nikataka kumpa robo tatu akakataa tanesko walivyokuja wakamwambia na yeye amlipe yule alipochukulia ndo akaingia upepo mwisho nikala umeme billa kumpa mia....
 
Kama ni jina lake halali, ana pointi endapo hawakulipwa au kuridhia majina yao kutumika.
Mi ningewachuna balaa.
 
Mange Kimambi
January 16, 2015 at 5:46 am
Reply
Koku I know for a fact hawajalipwa coz Nimeongea na mmoja wao hapo (staki mtaja asije ambiwa snitchi,lol) nikamuuliza umepewa mshiko wa maana for that coke thing akasema hapana walinipigia tu wakasema wanazawadi yangu tukapanga time ya kuonana ndo wakaniletea basi ,nikaaliwa na kwenye function yao ya mlimani city. Nikamuuliza whaaaaaat? waliwaambiwa ni zawadi huku wanawapiga picha mnavyokabidhiwa na wanazirusha kwenye insta page yao ya coke africa. Hiyo ni zawadi au promo? Na wakaambiwa kabiwa wazirushe instagram hizo picha na waweke hash tag #shareacoke nilichoka kabisa….
Kwanza mie ningepigiwa tu simu na kampuni kama coca cola ningeanza kuota mahela, kabla hata sijambiwa naitiwa nini ningeanza kuitumia pesa ambayo hata sijapewa hahahahahah….
 

Mkuu wangu , kweli huyu dada anahitaki ufafanuzi wa kisheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…