EMT unapaswa kutambua kwamba kuna wasanii kwa hiyari yao wenyewe walikubali kwenda kwenye hiyo hafla na kupiga mapicha baada ya kupigiwa simu kuwa eti kuna "zawadi" zao wanataka kupewa na Coke, hawa hawajalalamika zaidi ya kutoa shukrani kedekede kama le mutuz
Sawa
Lakini pia wapo wasanii waliogoma kwenda baada ya kupigaiwa simu na kuambiwa eti kuna zawadi zao za mabango ya makopo ya coke YENYE MAJINA YAO na wanatakiwa waende kwenye hafla ya kukabidhiwa then wapige mapicha na kutupia istagram zao na social media za coke. Hawa ndio wanaolalamika
Tuambie ni wasanii wapi hao walipigiwa simu wakagoma kwenda?
Pili kama waligoma kwenda na Coca Cola wakaamua tuu kutumia majina yao bila ridhaa yao which is the proper avenue to air their complains?
Kwa nini wasiwasiliane na hiyo kampuni na kulalamika?
Kama kampuni haiwasikilizi au haitaki kuwalipa kwa kutumia majina yao bila ridhaa yako basi waende kwenye vyombo vya sheria kudai haki yao.
Wao si wanaona wana kesi? Waende mahakamani.
Tunarudi pale pale celebrity ni watu wenye ushawishi mkubwa popote duniani na hawa ndio hutumiwa na makampuni duniani kote kufanya matangazo. Ronaldo analipwa mamilioni ya usd just kwakuvaa viatu vya nike na anapewa viatu hivyo bure..... Why?
Kama maselebu wa Bongo wanaona wanaliwa wachukue hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Coca Cola.
Waache kulalama. Wafanye kama alivyofanya Rihanna.
Msanii unapaswa kujitambua kwamba wewe ni brandy inayotakiwa kutemgeneza pesa kwa namna mbalimbali
Msanii yeyote anapaswa kutambua kuwaita wasanii wakubwa sehemu moja kwenye tukio la kuwapatia kitu chochote chenye nembo ya biashara na kuwataka waweke kwenye social media zao ni kutangaza biashara husika...... Sielewi mnashindwa kuelewa nini haswa katika hili
Sasa kama wanajijua ni "brandy" kama unavyodai wewe si waende kwenye vyombo vya sheria wakadai haki zao kwa "brandy" zao kutumika bila ridhaa yao? Tatizo nini? Kutafuta sympathy mitandaoni hakutawasaidia.
Sharecoke haijaanza tz pekee ipo inazunguka duniani na kila nchi wahusika wanapewa namna ya kuangalia jinsi watakavyofanya kupata hayo majina. Hivi kweli USA unampigia tu simu Lily wyne au 50cent au Maywhether eti njoo lmg grand tumetengeneza bango la kopo la coke lenye jina lako tuje tukukabidhi tupate na picha na utupie kwenye social media zako...... Kweli inawezekana? Bila makubaliano yoyote kabla unabandika tu 50cent?
Sasa mjinga nani hapo kama siyo wasanii wa kibongo?
Narudia tena Wolper hakukuta kopo limeandikwa wolper ndio akalalamika maana anajua wolper wapo wengi tu, Coke wenyewe ndio wamempigia simu na kumwambia njoo kwenye hafla tukukabithi bango la kopo la coke lenye jina lako
Umejuaje? Kwa kuamini tuu alichokiandika? Do you have any inside information of what exactly happened, au umedakia aliyosema tuu?
Kwa msanii anayejutambua kwake yeye hii ni biashara sababu jina lake na yeye ni brand ya biashara....period
Kwanini hawakumfuata mwajuma wa mbagala wakauze naye sura mlimani city na mapich ya insta?
Labda wasanii ya bongo hawajitambui. Wangekuwa wanajitambua wasingeishia kulalama mitandaoni bali kuchukua hatua stahiki kudai haki zao.
Why wasanii wakubwa ndio wauze sura kwenye hiyo hafla ya kukabidhiwa? Unahitaji kujua kwa undani maana ya marketing kulijua hili
Sihitaji kujua marketing bse it is relevant here. Issue kubwa hapa ni contratual na IP rights ambazo ni za kisheria. Kwamba Coca Cola wametumia majina yao bila ridhaa yao. In any contract, there must be a consent given by both parties. Sasa kama hawa meselebu wanadai, hawaku-consent majina yao kutumia, then they can sue the company for damages.
Au kama wanadhani kuwa majina yao yanalindwa na intellectual property law, basi wakaishtaki hiyo kampuni for infringing their IP rights kama alivyofanya Rihanna. If Coca Cola has infringed their IP rights, mahakama itaamua kuwa hao maselbu walipwe fidia.
Mwisho si sahihi kusema eti wanalialia kwenye social media badala ya kwenda mahkmani, si kilakitu unakwenda mahakamani jamani, hata akina Dr slaa wanadaigi kutoshiwa maisha lakini hawaendi mahakamani
Maisha ya sasa kwa wasanii social media inabeba sehemu kubwa sana na ndio hutolea madukuduku yao tofauti na zamani hadi uitishe media conference
Kwa hiyo huku mitandaoni ndiko haki zinapatikana? Mie nilidhani wako serious kumbe walikuwa wanaonyesha madukuduku yao tuu? Shame on them.
Topshop walipotumia image ya Rihanna bila ridhaa yake hakukimbilia fasta kwenye social media kutoa madukuduku yake kwa followers wake.
Bali alimtafuta mwanasheria akampa ushauri wa kisheria na mwisho kuishtaki Topshop na kushinda kesi na kufidiwa kama dola milioni 5 za kimarekani hivi. That's what I call being clever in using the law to protect your rights na siyo kuishia kutoa dukuduku kwenye mitandao ili kupata sympathy kwa watu ambao hata hawajui what exactly happened.
Kwenye suala kama hili hakuna cha kwenda kwenye social media au kuitisha media conference. That is a waste of time and money.
Ni ufinyu wa kudadafua mambo kunakopelekea watu kuaminishwa eti coke "wanawaenzi" wasanii kwa kuwapatia hayo mabango ya makopo yenye majina yao wakati kumbe wenzao wanafanya marketing kubwa sana
Mjinga ndiye aliwaye.
Binafsi naweza kusema huu ni mwanzo mzuri wa wasanii kuanza kujitambua kwamba wao kama wao na majina yao ni brand
Mwanzo mzuri? Subiri Octoba watakavyoanza kutumiwa na wanasiasa kama kondomu kwenye kampeni za uchaguzi.
Kuwatumia wasanii kama hivyo sio vibaya isipokuwa kuwepo na makubaliano kabla hata kama itakuwa ni bila malipo na si kukurupuka na kupigiwa tu simu eti njoo mlimani city kunaHafla ya kukabidhiwa kopo lako LENYE JINA LAKO
Waliovyoambiwa waende nao wakakurukupa na kwenda bila hata kuhoji. Baada ya kulishwa huko wanakuja kulalama mitandaoni. Waende zao huko.
Tambua coke wakindika juma basi juma neture hawezi kulalamika wala
Sioni la maana ambalo unawashauri hao masebu. If you really like them, if you really want their interests to be protected wasaidie angalao kwa kuwapa ushauri wa maana.
Kuwaambia eti ni sawa kuelekeza madukuduku yao kwenye mitando huwasaidii chochote. Wakishatoa madukuduku yao so what?
Kama kweli wanadhani wana kesi, basi waichukulie hiyo kampuni hatua stahiki. Waiandikie kampuni kutaka ufafanuzi juu ya kutumia majina yao bila ridhaa yao na kuwa wanastahili kulipwa or their IP rights have been infringed.
Kama hawaridhishwi na majibu yao au kama kampuni inagoma kuwalipa, wawape notice ya kulipa, vingenevyo watawapeleka kwenye vyombo vya sheria. Kama kampuni bado ikigoma, waende mahakamani wakadai haki zao huko.
Ila la muhimu ni kupata ushauri wa kisheria kama kweli wana kesi. Maana waki-rely kwenye hizi sympathy zenu na kwenda kudai kichwa kichwa the so called haki zao, watakuja kujuta kwa sababu sheria haina sympathy na hutakuwa mahakamani kuwatetea kwa kuandika kama ulivyoandika.