Mtu yeyote kutumika katika promo si lazima apate malipo na kwa mantiki hiyo si lazima ategemee malipo.
Ndiyo maana nimekuwa nikihoji kama kuna watu humu waliousikia upande wa Coca-Cola ukisema nini kuhusu suala zima.
Ndiyo maana nimeuliza humu kama kuna ambaye anayajua makubaliano au maafikiano ambayo pande zote mbili ziliyafikia, hakuna aliyejitokeza na kusema anajua zaidi ya Le Mutuz ambaye alikuwa mmoja wa waliopewa hayo makopo.
Na alichokisema Le Mutuz humu kinakinzana na kinachosemwa na wengi. Yeye (Le Mutuz) kasema waliohusika na kuchagua majina ya watu kuwekwa kwenye hayo makopo ni kampuni ya ICL na si Coca-Cola wenyewe.
Na kaongeza kuwa hao ICL waliwasiliana na hao watu na wakawaeleza kinachoendelea. Waliokubali walipewa hizo 'zawadi' zao na waliokataa hawakupata kitu hivyo na picha hawakupigwa.
Binafsi nahitaji taarifa zaidi ili niweze kuhitimisha kama kweli kuna unyonywaji au la.
Lakini vilevile nashangaa kuona baadhi ya hao waitwao wasanii, watu ambao mtu ungedhani wana tajiriba ya kutosha na mambo ya mikataba na makubaliano, badala ya kwenda sehemu husika kudai haki yao, wanakimbilia kwenda kwenye mitandao ya kijamii na kulialia.