Cocochanel interview prep!

Cocochanel interview prep!

Habarini wana jamvi
Kutokana Na ushauri Wa wadau ambao kwa kiasi kikubwa unajenga,
Tumeona ni vema tukawa Na utaratibu mzuri Wa uendeshaji Wa interview (mkabala) hapa jf.

Hii kwa kiasi Fulani itapunguza uholela Na malalamiko yasiyo ya lazima.

Tungependa kila mmoja wetu ajisikie inclusive ktk mikabala yetu
Na awe Na haki Na kushiriki bila bhugha!

Sasa Basi utaratibu ni huu,
Tutakuwa tunawajulisha nani yupo katika interview siku husika masaa matano kabla,ambayo tutatumia kukusanya maswali Na kuyachambua Na kumtumia interviewed maswali kumi ya msingi ambayo atayaandalia majibu mujarabu.

Kisha nusu saa kabla ya muda rasmi tutabandika Uzi Wa interview, ili kutoa taarifa Na watu kupata nafasi nzuri ya ushiriki.

Mgeni ataulizwa Na host maswali kumi au host atavyoona inafaa kisha
Atairuhusu hadhira (audience) kuuliza maswali ya randomly!

Kwa leo tunataraji cocochanel kuwa
Nasi jioni aghalabu kuanzia saa kumi Na nusu jioni.

Kwa hiyo tunakaribisha maswali ya maana ambayo unadhani linafaa kuwa swali la msingi Na kunufaisha
Wengi.

Asanteni.
Regards,
DJ sepetu.
Tumeshakuchoka na wewe

[emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57]


[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Me naomba unisaidie kumuuliza maswali haya 3.
1-Amewahi kuugua ugonjwa wowote wa akili ktk maisha yake!?.

2-Jinsi yake hasa ni ipi! Ni KE au ME!??

3-Je! Ktk maisha yake amewahi kufanya jambo gani la kutumia akili nyingi liwe la kijamii au kifamilia na likafanikiwa(ataje jambo hilo) na km halikufanikiwa kwa nini!??

Ni hayo tu ntarudi kwa maswali ya nyongeza..!!
 
Nakumbuka huyu bwana mdogo alivyoanzishaga Interviews zake wabongo mlikuwa mnamponda sana kama anatafuta kiki.
Lakini leo ubunifu wake ndiyo unafanya ChitChat iwe moto moto mnataka kujimilikisha kipindi chake: Haiwezekani.

Hahahahaha
 
PENDEKEZO; UKISHAMUULIZA HAYO MASWALI KUMI YANATOSHA...baada ya hapo wewe utakuwa unarekebisha hili na lile mfano swali la marudio unamwambia limeshajibiwa na liko kwenye post namba fulani

Tuachie sisi wengine tuendelee, vile vile Mwambie Cocochanel awe anajibu maswali papo kwa papo ndio itafaa zaidi kuliko tuweke maswali yetu hapo yaje kujibiwa baaadae sana kitu ambacho kinakatisha tamaa ambapo muda mwingine unakuta halijajibiwa
Pamoja mkuu point sana umeronga
 
Huyu dem hafai interview uuuuwwiii uuuuwwiii uuuuwwiii Uuuuuuuwwiiii hafai hafai hafai namjua vzr
 
Back
Top Bottom