Hivi kwanini kwa tanzania ukisema coding au programming mtu anawaza IT tu?
Kuna tatizo moja naliona kwa tanzania, ni kuhusu embedded system programming.
Unaweza kukuta mtu ni programmer kabisa ila hawezi kuandika program akaweka kwenye microprocessor ifanye kazi fulani,hii naiona ni tatizo kubwa.
Programmers wengi ni IT tu,nje ya hapo hajui chochote.
Nadhani tupanue ulingo zaidi,ni ajabu kukuta programmer haijui hata arduino ambayo ni basic kabisa.
Nimewahi kuonana na mtu mmoja anacheza na kuandika program za arduino balaa,anasema amejifundisha mwenyewe,jamaa anawazidi mbali sana hata waalimu wa programming huko vyuoni.