COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu


Mungu alipokuwa anaumba ulimqengu alikuwa na uwezo wa kufanya kusiwe na matetemeko ya ardhi yatakayoua watoto wasio na hatia au hajuwa na uwezo huo?

Mtoto kumuuliza baba kwa nini kamzaa wa kiyme so sawa na maswali yangu kuhusu mungu wenu.

Baba hana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Mungu wenu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Baba anaweza kujibu kwamba yeye alikuwa hana uwezo wa kuchagua mtoto azaliwe wa jinsia gani.

Mungu nikimuuliza kwa nini kaumba ulimwengu wenye matetemeko ya ardhi yanayoua watoto wasio na hatia atajibu vipi?

Atajibu hakuwa na uwezo wa kuchagua kuumba ulimwengu ambao hauna matetemeko ya ardhi yanayoua mpaka watoto wasio na hatia?
 
Hayo mnayoyaeleza yote anayajua maana naye alikuwa hukohuko,labda muanzie kumuuliza ni kipi nilichomtoa huko na kuamua kuwa alipo sasa.

Mungu wenu hana logical consistency.

Hapa tunaambiwa ni mungu wa mapenzi makuu na mwenye haki yote.

Kule tunaambiwa kaumba ulimwengu wenye matetemeko ya ardhi yanayoua mpaka watoto wasio na hatia.

Kama angekuwa mwanadamu angepelekwa The Hague ajibu mashtaka ya mass murder.

Kaumba ulimwengu wenye kuweza kuwepo na mabaya licha ya juwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya.

Lakini hilo halitawezekana


Kwa sababu hayupo, ni hadithi tu.

Zilizotungwa na watu waliokosa elimu ya logic ya kutosha.

Ndiyo maana mungu wenu ukimpa motihani ya logical consistency anashindwa vibaya sana.
 

Mungu, kwa kiwa ana uwezo wote, anatakiwa kutoshindwa kifanya yote yawe mema kwa wote.

Kwa nini hakufanya hivyo?
 

Mimi na wewe bado tunajadili maana ya kujipinga.

Ila kama wewe kweli ni mtu uliyehuru na unachokiamini basi waeleze ni kipi kilichokufanya uache dini yako na kuwa Atheist. Maana hoja unazozitoa humu ni hoja maarufu za kupingia mungu ila si hoja zenye kuweza kumfanya mtu aache dini na kuwa Atheist.
Kwahiyo kama unajiona upo huru unaweza ukatueleza ila kama haupo huru basi.
 

Dini yangu? Dini yangu kwa maana gani? Niliwahi kuanzisha dini dunia hii?

Hujajibu ni vipi mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani?
 
Mungu, kwa kiwa ana uwezo wote, anatakiwa kutoshindwa kifanya yote yawe mema kwa wote.

Kwa nini hakufanya hivyo?

Endapo kila jambo lingekua jema...je ungetambua umuhimu wa jambo hilo?...je endapo watu wangekua hawaumwi (au kufa),ungetambua umuhimu wa maisha?.ungetambua uumbaji wa mungu? Ungetambua na kushangazwa na namna mwili wako unavyofanya kazi?...bila matetemeko,ungeona wapi milima mizuri?,ungeona wapi mabonde?
Em fikiria kama KILA KITU kingekua chema,dunia ingekuaje..nisingetaka kuishi humo!
 

Jifanye kama hauelewi ila unanielewa vizuri. Najua hauna uhuru huo ndiyo huwezi kufanya hivyo.

Hilo kwako si swali kama usemavyo(ndiyo maana huwezi kukubali jibu la aina yeyote) bali ni hoja yenu ya kupinga mungu mliyoikariri na mnaiheshimu. Ndiyo maana miaka yote et hakuna aliyeweza kujibu hilo swali. Sasa mie kwa kulijua hilo sirudi tena huko.

Wewe tuendelee tu tulipoishia kuhusu kujipinga.
 



Anasema Mungu ni hadithi, haya anayosema yeye ni matukio mapya? Hizi pia si hadithi? Kila mtu kaamia kuamini yake. Maswali anayouliza ndio aina ya maswali yameanza kuulizwa kitambo sana.

Hakuna kipya.
 
Kwa nini nikuthibitishie?

Nataka nipate njia ya kukuthibitishia uwepo wa Mungu.
Na ndio maana nimekuomba unithibitishie hivyo ambavyo tunavyo kilasiku.
ukishathibitisha vitu hivyo vidogo huenda na mimi nikapata njia ya kukuthibitishia unavyotaka.
Ukishindwa ndio turudi kulekule kwamba kushindwa kuthibitisha kwa matakwa ya Kiranga haina maana kwamba Mungu hayupo.
 
Last edited by a moderator:

Kwa nini unafikiri mimi naamini katika kuwapo kwa hivyo vitu kama majini mpala nikuthibitishie kwamba vipo?

Ili niweze kuwa na mzigo wa kukuthibitishia kwamba jini lipo inabidi niamini kwanza kwamba jini lipo.

Umejuaje kwamba mimi naamini jini lipo?

Au una assume tu kwamba kwa kiwa kijijini kwenu kila mtu anaamini majini yapo, basi na Kiranga naye atakuwa anaamini hivyo?

Udakuzi unautafsirije wewe?
 
Last edited by a moderator:

Hahaha,huyo jamaa anataka useme unaamini majini yapo haha,hivi majini ni manini kwani haha
 

Baada ya kukamilisha uumbaji wake Mungu alimpa mwanadam Akili ili aweze kuchagua namna gani ataishi bila kumtenda Bwana makosa,ndo mana hata ukiangalia chanzo cha Mungu kuruhusu mabaya juu yetu ilikua ni mwanadam kumuasi yeye yaani kutotii maagizo aliopewa na Mungu!!
 

Well said
 
Wewe hicho ndiyo unachokiweza,ndiyo maana nilishangaa ulipoanzisha mada kule.

Wewe ninmgeni sana katika mijadala hii ndio maana hata maswali unayouliza yameulizwa sana humu mwaka 2013 na ndo mana Kiranga anakupa majibu papo kwa papo maana anajua kabisa nini utauliza baadae.

..Karibu katika ulimwengu huru kijana..
 
Last edited by a moderator:

Kwa nini mwanadamu asitii maagizo ya mungu?,kwani mungu hakujua kabla kwamba mwanadamu hatatii maagizo yake?.mbona unajichanganya mara unasema baada ya mungu kukamilisha uumbaji ndio akampa mwanadamu akili sasa uumbaji wa binadamu ulikamilika vipi bila kuwa na akili?
 

Akili niliozungumzia hapo ni upeo wa kupambanua mambo,Mungu alimruhusu mwanadam kuchagua lipi afanye na lipi aache, Mungu si dikteta. Alikua na uwezo wa kuamua hivyo uonavyo wewe lakin yeye ni mwenye busara na hekima na upeo kuzidi vyote ndo maana aliacha mwanadam afanye uchaguzi wake katika kumtii muumba wake
 
Wewe hicho ndiyo unachokiweza,ndiyo maana nilishangaa ulipoanzisha mada kule.


Ameanzisha mada ambayo ilikuwa ya kishabiki mada yenyewe ilikuwa haijionyeshi kwamba ilikuwa inataka nini.
 


Jinni umekwepa
unaniuliza tafsiri ya udakuzi.usinitoe kwenye hoja Nimekwambia tangia mwanzo unithibitishie UDAKUZI WA MMAREKANI KWENYE SIMU YA A.MARKEL.

Lakini tafsiri ya neno udakuzi limetokana na neno daka.

Tafsiri ya udakuzi inaweza ikawa pana laki kwa kifupi ni kunasa mawasiliano au kuvunja code au password na kuchokua inbox data kwa njia ya kimtandao.
 
Wewe ninmgeni sana katika mijadala hii ndio maana hata maswali unayouliza yameulizwa sana humu mwaka 2013 na ndo mana Kiranga anakupa majibu papo kwa papo maana anajua kabisa nini utauliza baadae.

..Karibu katika ulimwengu huru kijana..

Hebu toa mfano wa swali moja tu ambalo liliulizwa toka 2013.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…