Ni vizuri kwamba umeanza na "pengine", maana hujui hilo kwa uhakika, ni speculation.
Lakini tukitaka kuongea mambo ya uhakika, from the perspective of what our existence could have been had it been created by an omnipotent, omniscient and omni benevolent godhead, hakuna mtu anayeishi maisha mazuri.
1. Kila mtu atakufa. Hata ukiwa na maisha mazuri vioi, ni ya muda mfupi tu ukilinganisha na milele.
2. Kila mtu anapata mambo asiyotaka kupata. Magonjwa, matatizo, kutofanikiwa etc.
3. Kila mtu kuna vitu anavyotaka ambavyo hapati. Unaweza kusa bikionea kama Ted Turner lakini katika maisha huna familia nzuri.
4. Kila mtu anaishi bila ya uhakia wa kitakachokuja mbele.
Sasa kama maisha mazuri yoyote atakayokuwa nayo mtu bado yatakuwa chini ya hayo hapo juu, basi maisha hayo hayajawa mazuri vya kutosha.
Pia, unakosea ukihusisha kuhoji kuwepo kwa mungu na tu kujiona ana mamlaka kuliko chochote hapa duniani.
Kwa kweli, it is quite the opposite. Wanaoamini kuwepo kwa mungu wanasema wana mamlaka kuliko chochote hapa duniani, na mamlaka hayo wamepewa na mungu. Kama umesoma bibkia utakuwa unafahamu mstari unaosema kwamba mungu kawaambia watu zaeni mkaijaze na kuitawala dunia. Atheists hatuna mandate kama hiyo, sasa utasemaje wasioamini mungu ndio wanaojiona wana mamlaka kuliko chochote duniani unapata wapi rationale ya kusema hilo?
Unaposema "nilimpinga mungu kuliko wewe" unawezaje kuwa na uhakika wa hilo? Unajua ukomo wa kumpinga mungu wa huyo unayejadiliana naye? Unajua kazi zake zote katika kumpinga mungu? Au una assume tu kama unavyo assume kwamba mungu yupo?
Umemtaja shetani. Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao shetani anawezekana kuwepo wakati alikuwa na uwezo wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao shetani hawezekani kuwepo?