COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

stroke

You still have not proved god exists.

Saying that god exists is no proof that god exists.

Laiti kama Mungu angekuwa anatoa hukumu kama binadamu, basi dunia nzima tusingekuwepo, tunamkashfu na kumkana ila bado anaendelea kukupa pumzi, bado anaendelea kukulinda na ajali, au unadhani hiyo pumzi yako anakupa baba au mama yako? Tusipende kumkufuru Mungu kiasi hiki
 
Last edited by a moderator:
Ninachooamini ni kwamba miongoni mwa alama za uwepo wa mungu ni akili, sasa nikiono watu hapo juu mkichallengiana inamaanisha akili, tayari one of the signs..

Pia wanadamu tumepewa ukomo wa uelewa, so hakunaga kujua yoote. There is not but one God!

Allah..

Utaki kakojoe ulale..

Ahahahah nimependa comment yako, wenzetu wanapewa pumzi na uhai na baba zao matajiri, sie maskini wacha tumtegemee Mungu mtetezi wetu, Mungu asiye na upendeleo, Mungu wa wote
 
Laiti kama Mungu angekuwa anatoa hukumu kama binadamu, basi dunia nzima tusingekuwepo, tunamkashfu na kumkana ila bado anaendelea kukupa pumzi, bado anaendelea kukulinda na ajali, au unadhani hiyo pumzi yako anakupa baba au mama yako? Tusipende kumkufuru Mungu kiasi hiki

Huoni kwamba hilo linaonesha mungu hayupo?

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote anaruhusu watu wasio na hatia wapatwe na mabaya kwa mafungu walati majambazi wanadunda tu?
 
Mungu yupi unayemuamini wewe? Mungu bahari au Mungu yupi?

Wapi nimesema namuamini mungu?

Unaanzaje kuniuliza mungu yupi namuamini wakati sijakwambia kwamba namuamini mungu yeyote?
 
Ninachooamini ni kwamba miongoni mwa alama za uwepo wa mungu ni akili, sasa nikiono watu hapo juu mkichallengiana inamaanisha akili, tayari one of the signs..

Pia wanadamu tumepewa ukomo wa uelewa, so hakunaga kujua yoote. There is not but one God!

Allah..

Utaki kakojoe ulale..

Umeanza kwa kuandika "ninachoamini", unaamini au unajua?

Unaelewa tofauti?

Kwa nini akili ni alama za kuwepo kwa mungu?

Unaelewa kwamba kuwepo kwa alama ya kitu si sawa na kuwepo kwa kitu? Kwamba alama ya kitu inaweza kuwepo bila ya kitu chenyewe kuwepo? Kwamba alama za vidole za mtu zinaweza kuonekana katika dirisha lililovunjwa katika wizi, na mtu huyo akawa kafikiriwa kuwa mwizi, kwa alama zote, lakini asiwe mwizi na mwizi akawa mtu tofauti? Au kusiwe na mwizi kabisa ila mwenye nyumba kichaa tu?

Kama wanadamu tumepewa ukomo wa kuelewa, utajuaje kwa uhakika kwamba mungu yupo?

Ukiwa na ukomo wa kufikiri, huwezi kusema kwa uhakika kwamba mungu yupo, kwa sababu una ukomo wa kufikiri.

Maneno yako yanajipinga yenyewe. Ni kama vile unasema umefungiwa katika chumba ambacho hakina mawasiliano yoyote na nje (una ukomo wa kufikiri) lakini unajua nje kuna mvua inanyesha (kuna mungu).

Kama umefungiwa katika chumba ambacho hakina mawasiliano na nje, utajuaje kwamba mvua inanyesha nje?
 
stroke

kwa upande wangu yoote hayo HAYAJATHIBITISHA WAZI UWEPO WA MUNGU labda kdg hilo la ajali kama wasimuliavyo iliwahi tokea ajali watu wote wakafa akapona mtoto mchanga akielewa mtoni (kama ni tukio la kweli)

Kwangu mm nathibitisha uwepo wake MUNGU kama ifuatavyo;

1. mara moja moja sana may be mara 1 au hata mara 2 kwa mwaka.. hutokea kulala na kuota tukio tofauti kabisa, na mara nyingi ya kushtua/ajabu na asb yake naweza kukumbuka kdg tu na kusahau tena,, sio muda murefu HUTOKEA TUKIO HUSIKA hapo sasa ntalikumbuka ndoto yote yaweza isiwe exactly 100% kufanana lakini by 90 % lazima...

2. waweza kufanya maamuzi yasio na logic kabisa,, hun sababu ya kufanya hicho kitu na tena hata ukiuuliza watu unaowaamni/wataalam kwa ushauri watakuzuia tu, LAKINI HURIDHIKI moyo wako unakutuma kufanya tu hata kama pana hasara ya wazi wazi....

mwisho unalifanya na baada ya muda tu unakutana na matokeo yaajabu NEEMA TUPU USIOWEZA SIMULIA ILIKUWAJE MWANZO HADI MWISHO na pia hakuna anaweza amini ni hatari wanaweza kukuita mchawi au hata mwizi vyovyote vile kwa imani zao lakini HAKIKA MUNGU NI WAAJABU.

3. Unaingia mkataba aidha wa kibiashara kwa tahadhali zote na ushauri wa watu kadhaa, na wa gharama kubwa, bahati mbaya baada siku chache tu unagundua kuwa utapata hasara kubwa sn mfano shs 20 mln (hili limetokea feb hii) Inakuumiza sana kupata hasara kwa kutoelewa ya kesho. kwa sisi tunaojali kauri hata kama hujamlipa huwezi KUMRUSHA NI ZURUMA,,

Linalo baki ni wewe kulia na mungu wako na maumivu usiku hulali, cha AJABU jamani MUNGU ni mwema yule yule anayekudai anghaili na kuvunja yeye mkataba akitegemea mashali zaidi kuliko yako uliokuwa unamlipa(wakati huo na yeye hana uhakika) Kwang mm nauona huo ni UWEPO WA MUNGU..

4. Mwisho ni watu wengi sana hupata ISHARA mbalimbali kuwajulisha matukio kama KILIO cha ndugu wa karibu kabla HAJAPATA TAARIFA RASMI, Au MAFANIKIO MAKUBWA lkn akipata ishara fulani tu haichukui muda yaweza chukua hata wiki hadi kupata taarifa rasmi ya tukio husika....

Unafahamu maana ya kuthibitisha? Unatumia neno hilo katika framework gani? Maana hayo yote uliyoelezea hayathibitishi kuwepo kwa mungu.

1. Unaweza kuwa na ugonjwa wa akili tu.

2. Random luck is not proof of exiatence of god.

3. This is sheer desperation rather than proof b of the existence of god.

4. How does that prove gid exists? How do you know that DNA can transmit certain signals that we do nit know about yet or some equally weird telepathy/ESP like that?
 
Last edited by a moderator:
Huoni kwamba hilo linaonesha mungu hayupo?

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wite na upendo wote anaruhusu watu wasio na hatia wapatwe na mabaya kwa mafungu walati majambazi wanadunda tu?

Tatizo lako unajadiri kitu ambacho hata haujui sifa zake.
 
Huoni kwamba hilo linaonesha mungu hayupo?

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wite na upendo wote anaruhusu watu wasio na hatia wapatwe na mabaya kwa mafungu walati majambazi wanadunda tu?

Mungu anaruhusu yote hayo ili tumjue yeye ni nani na ana uwezo.gani? , binadamu tunanuka dhambi, na ndio maana kila siku vifo vya ajabu vinatokea, magonjwa ya ajabu yanazuka kila siku, ila binadamu tumekuwa wagumu, kama tungeamua kumtegemea yeye na kumwabudu yeye sidhani kama haya yote yangetokea
 
Wapi nimesema namuamini mungu?

Unaanzaje kuniuliza mungu yupi namuamini wakati sijakwambia kwamba namuamini mungu yeyote?

Umeshawahi kujiuliza kwa nini watu wanakufa kila siku tena vifo vya ajabu ila wewe bado uko hai? Kuna watu wapo mahospitalini wanaugua hawajiwezi, je unadhani wewe ni msafi au mtakatifu kuliko wao? Mungu anataka ujifunze kitu kupitia hayo yote yanayotokea duniani ili baadae usije kumlaumu kuwa Mungu ana upendeleo wakati alikupa nafasi ya kumuabudu ukaufanya moyo wako mgumu, lazima tujifunze kumuamini Mungu
 
Mungu anaruhusu yote hayo ili tumjue yeye ni nani na ana uwezo.gani? , binadamu tunanuka dhambi, na ndio maana kila siku vifo vya ajabu vinatokea, magonjwa ya ajabu yanazuka kila siku, ila binadamu tumekuwa wagumu, kama tungeamua kumtegemea yeye na kumwabudu yeye sidhani kama haya yote yangetokea

Haya majibu rahisi sana kwa maswali magumu!.Tetemeko la ardhi,volcano naTsunami vinahusiana nini na maovu ya mwanadamu?.Kumjua mungu maana yake nini?,Alishindwa nini kutufanya tumjue automatically?.Ikiwa aliweza kutupa uwezo wa kuvuta hewa automatic alishindwa nini kuzifanya minds zetu zimjue automatically?,kwa nini nimsome mungu darasani?kuna haja gani ya kumjifunza juu ya muumba wangu?.

Huu ni udhaifu mkubwa wa huyo mungu(kama yupo) .Mungu anayepata hasira,mungu anayepata huzuni,mungu anayepata jazba?,huyo ni mungu ?,

God is man made!,HAKUNA MUNGU ....... Changanuka kijana ...karibu katika Ulimwengu huru....
 
Pengine unaona Mungu hayupo kwa kuwa labda unaishi maisha mazuri, unafanya unachokitaka ,unajiona wewe una mamlaka kuliko kitu chochote apa duniani, mimi nilikuwa mkaidi kuliko wewe, nilimpinga Mungu kuliko wewe, ila wakati wako ukifika utalia na kusaga meno, muache shetani afanye kazi yake ili baadae Mungu ajidhihirishe kuwa yupo
 
Kila mtu amepangiwa siku yake ya kufa na ndio maana tunaambiwa tumrudie Mungu ili zamu yetu ikifika basi nafsi zetu zikapumzike mahali pema peponi, ndio maana huyu Mungu ninayemwamini anatusihi tuache kutenda dhambi na tumrudie yeye,ila sisi tunampinga na ndio maana tunakufa vifo vibaya na vingine vya aibu, tumemsahau Mungu na kumtukuza shetani
 
Mungu anaruhusu yote hayo ili tumjue yeye ni nani na ana uwezo.gani? , binadamu tunanuka dhambi, na ndio maana kila siku vifo vya ajabu vinatokea, magonjwa ya ajabu yanazuka kila siku, ila binadamu tumekuwa wagumu, kama tungeamua kumtegemea yeye na kumwabudu yeye sidhani kama haya yote yangetokea

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aruhusu mabaya yote hayo ili tu tumjue yeye ni nani na ana uwezo gani?

Kama yeye ana uwezo wote, kwa nini ni muhimu sana sisi watu tumjue na kutambua uwezo huo? Tusipoutambua unapungua?

Huyu mungu wenye uwezo wote mnavyosema karuhusu mabaya ili tu tumtambue mbona mnamfanya mungu narcissistic mwenye inferiority complex, a curious combination, especially for an omnipotent and omniscient godhead.

Hata kama kwa sababu fulani tusiyoifahamu ni muhimu tumjue yeye ni nani na ana uwezo gani:

Ameshindwa kufanya namna nyingine yoyote ambayo haihusishi viumbe wake aliowaumba bila kuombwa wala mkataba kupata tabu na mateso mengi katika maisha yao?

Unaposema binadamutunanuka dhambi hujajibu swali langu la msingi, huzungumzii mzizi wa swali langu, unaongelea binadamu na dhambi, vitu ambavyo vyote vimekuja baada ya mungu na kwa ruhusa ya mungu.

Ksa nini mungu alipoumba ulimwengu, ambapo tunaambiwa akikuwa na uwezo wa kuumba uimwengu wowote, hakuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani kufanyika? Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekaniki?
 
Umeshawahi kujiuliza kwa nini watu wanakufa kila siku tena vifo vya ajabu ila wewe bado uko hai? Kuna watu wapo mahospitalini wanaugua hawajiwezi, je unadhani wewe ni msafi au mtakatifu kuliko wao? Mungu anataka ujifunze kitu kupitia hayo yote yanayotokea duniani ili baadae usije kumlaumu kuwa Mungu ana upendeleo wakati alikupa nafasi ya kumuabudu ukaufanya moyo wako mgumu, lazima tujifunze kumuamini Mungu

Na mimi siku moja nitakufa That is the deeper implication of second law of thermodynamics at work.

What is your point? I only see ureasoed fear of the unkown.

Watu kufa ndiyo proof kwamba mungu yupo?

If aything, watu kufa kunaoesha mungu mwenye uwezo wote na upedo wote hayupo. Otherwise kwa nini kaumba uiwengu wenye vifo vinavyoteganisha wapendanao kwa msiba sana?

What is your point, if you have any?
 
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu unaoruhusu ajali kutokea na viumbe wake kuumia vikali na hata kufa?

Wakati alikuwa na uwezo wote wa kuumba ulimwengu ambao ajali haiwezekani.
 
Ndg yangu kiranga kwa kila jambo hapa duniani na hata Mbinguni KUNA KANUNI ZAKE,usipozijua huwezi kuwa katika nafasi ya kuelezea Chochote hata kama hapa nchini Au duniani tunao uhuru wa kuongea
 
Pengine unaona Mungu hayupo kwa kuwa labda unaishi maisha mazuri, unafanya unachokitaka ,unajiona wewe una mamlaka kuliko kitu chochote apa duniani, mimi nilikuwa mkaidi kuliko wewe, nilimpinga Mungu kuliko wewe, ila wakati wako ukifika utalia na kusaga meno, muache shetani afanye kazi yake ili baadae Mungu ajidhihirishe kuwa yupo

Ni vizuri kwamba umeanza na "pengine", maana hujui hilo kwa uhakika, ni speculation.

Lakini tukitaka kuongea mambo ya uhakika, from the perspective of what our existence could have been had it been created by an omnipotent, omniscient and omni benevolent godhead, hakuna mtu anayeishi maisha mazuri.

1. Kila mtu atakufa. Hata ukiwa na maisha mazuri vioi, ni ya muda mfupi tu ukilinganisha na milele.
2. Kila mtu anapata mambo asiyotaka kupata. Magonjwa, matatizo, kutofanikiwa etc.
3. Kila mtu kuna vitu anavyotaka ambavyo hapati. Unaweza kusa bikionea kama Ted Turner lakini katika maisha huna familia nzuri.
4. Kila mtu anaishi bila ya uhakia wa kitakachokuja mbele.

Sasa kama maisha mazuri yoyote atakayokuwa nayo mtu bado yatakuwa chini ya hayo hapo juu, basi maisha hayo hayajawa mazuri vya kutosha.

Pia, unakosea ukihusisha kuhoji kuwepo kwa mungu na tu kujiona ana mamlaka kuliko chochote hapa duniani.

Kwa kweli, it is quite the opposite. Wanaoamini kuwepo kwa mungu wanasema wana mamlaka kuliko chochote hapa duniani, na mamlaka hayo wamepewa na mungu. Kama umesoma bibkia utakuwa unafahamu mstari unaosema kwamba mungu kawaambia watu zaeni mkaijaze na kuitawala dunia. Atheists hatuna mandate kama hiyo, sasa utasemaje wasioamini mungu ndio wanaojiona wana mamlaka kuliko chochote duniani unapata wapi rationale ya kusema hilo?

Unaposema "nilimpinga mungu kuliko wewe" unawezaje kuwa na uhakika wa hilo? Unajua ukomo wa kumpinga mungu wa huyo unayejadiliana naye? Unajua kazi zake zote katika kumpinga mungu? Au una assume tu kama unavyo assume kwamba mungu yupo?

Umemtaja shetani. Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao shetani anawezekana kuwepo wakati alikuwa na uwezo wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao shetani hawezekani kuwepo?
 
Back
Top Bottom