Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Swali uliloulizwa hujalijibu, ulilolijibu hujaulizwa.
Choice inekuja baada ya mungu kuanua kuumba ulimwengu huu, na choice itakuwapo, na choice hiyo itakuwa na mipaka gani, hivyo ndivyo maandiko yanavyosema.
Kwamba ulimwengu na misingi yake vimeumbwa na mungu.
Swali langu halihusiani na kutaka kujua kwa nini kuna manaya katika ulimwengu huu, lingekuwa swali ni hilo, ungeweza kunijibu kwamba, kuna mabaya kwa sababu watu wamepewa uwezo wa kuchagua mema na mabaya nao wanachagua mabaya.
Swali langu ni tofauti, na hujalijibu.
Swali langu ni, mungu huyu mnayemsema ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, ukiwamo uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kabisaaa, kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani?
Ni kweli alikuwa ana uwezo wa kuuumba ukimwengu huo lakini hakutaka tu?
Kama ni hivyo hana upendo qote basi, maana mqwnye upendo hawezi kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
Au, alitaka sana kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, lakini akashindwa tu?
Kama ni hivyo basi hawezi yote, maana alitaka kuumba ulimwengu usiowezekabika kuwa na mabaya lakini akashindwa.
Ni hivi, wewe utanirudisha kuleee, nilikosema unauliza swali ambalo kuna namna tayar unataka ujibiwe, ikienda tafauti unajenga hoja hapo ukitumia neno "Kwanini"....
Nikueleze vile mimi naelewa. Mambo mengi mabaya chimbuko lake ni Uasi wa MalaikA huko Mbinguni, ambapo kati ya walioasi ni Pamoja Na Shetan ambae ndie Chimbuko la Uovi, nae alikuja kwa Maswali ya Mitego kama yako, nia ikiwa ni kudhoofisha Imani ili shetani atawale Maisha ya Mwanadamu.
Ukijiuliza hili linawezekana vipi, ndio Huo Upendo ambao Mwenyezi Mungu anao juu yetu, shetan anautumia kwa Faida yake... Hapa namaanisha hivi,
Tumepewa Uhuru wa kuchagua namna tunavyotaka tuishi, tuamini n.k.... Katika hayo ya kuchagua ndio yapo mawili ambayo yote yamehainishwa Mwisho wake kwa Kila Mwenye imani nalo.
Hii nafasi ya kuchagua, ndio katikati yake yupo shetani, na hii unaweza hoji kwann Mwenyezi mungu asimuue tuu shetani mara moja....
Jibu ni rahisi, kwanza Mwenyezi mungu hafanyi kwa matakwa yako na Pili, Uwepo wa shetani ni ktk Maisha ya mwanadamu ndio mtihani mwanadamu anatakiwa kuushinda, Ili approve kuwa ametambua Mamlaka aliopewa ni makuu kuliko shetani, all you ni to do I LEARN AND UNDERSTAND THE WORD OF GOD. And Live what you Preach.
Hilo ndio jibu Langu.
Nimekuuliza kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao ubaya unawezekana, kwa maana nyingine kwa nininhakuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani.
Wewe unanijibu chimbukonla ubaya ni uasi.
Hata swali hujalielewa.
Mwenyezi Mungu kaumba Ulimwengu ambao Maasi yanawezekana kama ambavyo mema yanawezekana ili kila mmoja atambue uwezo alionao juu ya mambo hayo mawili kisha kwa Maamuzi yake achague kuishi kati ya hayo Mawili. Uwepo wa Maasi au mabaya ni kipimo, kuyashinda ama kushindwa ni matokeo yanayotokana na kiasi ama kiwango cha elimu ulichonacho juu ya mambo hayo mawili, na maamuzi utakayochukua kulingana na Elimu uliyopata.
Niulize swali Lingine tafadhali.
<..Mungu Yupo Full STOP..>
****** :canada: :canada: ​******
Siyo rahisi hivyo.
Tatizo lako lipo kwenye mind setting yako....! kama umeamua kuamini ivyo mi siwezi kukubadilisha cha kufanya nakuombea sala fupi Mwenyezi Mungu akujalie Upate Ufahamu wa kumtambua, kutambua uwepo wake na uwepo wa kazi zake. Amin
Tatizo lako unarahisisha mambo mpaka unakosa maana.
Kati yangu mimi ninayeuliza maswali na kujadili kwa kina na wewe unauelazimisha tu kirahisi kwamba mungu yupo bila kutaka mjadala (Mungu yupo. Full Stop.) nani ana tatizo la kuwa na mindset ambayo haitaki kubadilika?
Siyawezi mabishano na samahani kama nitakuwa nimekukwaza. . . .
Tangu bandiko la kwanza ushaonesha huwezi majibizano kwa kuandika "Mungu yupo. Full Stop".
Kama vile wewe ndiye hakimu wa suala hili.
Hukuwa hata na haja ya kurudia kuandika kwamba huwezi majadiliano.
Kwa nini unafikiri kila ninapoongelea mabaya naongelea maasi na habari ya uwezo wa binadamu kuchagua mema na mabaya?
Leo tumesikia habari limepiga tetemeko la ardhi huko Papua New Guinea, 7.7 on the Richter scale.
Tetemeko kama hili litaua mpaka vichanga ambavyo havijui chema ni kipi na kibaya ni kipi.
Huyo mungu wako aloshindwa kuumba ukimwengu ambao hauna kitu kama hiki?
Au ulimwengu ambao likija tetemeko liue mijambazi tu ambayo haijafanya mema na kuacha vitoto vichanga ambavyo havina hatia?
Si mnasema ni mungu wa haki?
Sasa haki iko wapi hapo?
Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao matetemeko kama haya yanaweza kutokea na kuathiri viumbe wake wasio na hatia wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya haya, na hata yakiwemo, kwa nini yawapate wasio na hatia?
Kama kweli kuna mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote, upendo wote na haki yote.
http://www.cnn.com/2015/03/29/asia/papua-new-guinea-earthquake/
Kila kilicho complex kinahitaji muumbaji?
Mwenyezi Mungu kaumba Ulimwengu ambao Maasi yanawezekana kama ambavyo mema yanawezekana ili kila mmoja atambue uwezo alionao juu ya mambo hayo mawili kisha kwa Maamuzi yake achague kuishi kati ya hayo Mawili. Uwepo wa Maasi au mabaya ni kipimo, kuyashinda ama kushindwa ni matokeo yanayotokana na kiasi ama kiwango cha elimu ulichonacho juu ya mambo hayo mawili, na maamuzi utakayochukua kulingana na Elimu uliyopata.
Niulize swali Lingine tafadhali.
Tusameane mkuu then naomba kama yaishe vileee....., au unaonaje??
Siyo kila kilichocomplex tu...kwa ujumla wake hakuna kitu kilichojizukiaga tu, lazima kina mwanzo wake na mwanzo wa ulimwengu na kila kilicho ujaza katika ajabu zake ni Mungu, ambaye Wewe pasco katika kufikir kwako kwenye ukomo unam ignore kwamba hayuko, complexity na imposibilities...vyote hiv vinajaribu tu kumwelezea Mungu ni wa Namna gani.
Aisee hii ni hatar kama jibu lako ndiyo hili!.Hivi ulishawahi kuchukua muda kufikiria juu ya tofauti yetu wanadam na wanyama?,okay najua utanijibu kirahisi kwamba sisi tuna utashi,sasa je tukimchukua mtoto mdogo aliyezaliwa jana tukamtenga na wanadamu na kumwela sehem flani safe porini kisha tukamuhudumia kila kitu lakini tusiwe close nae kisha akafikia umri umri fulani kama miaka 5 huku akiwa hajawahi kumwona mwanadamu kabisa zaidi ya kuona wanyama wa mwitu.Hapo tukamwacha bila kumuhudumia chakula.Je unadhani nini kitatokea?,
Okay kwa taarifa yako baada ya muda atakuwa hana tofauti na mnyama wa mwitu kimatendo na hataweza kudevelop lugha zaidi ya kukop zile za wanyama.
Haya sema sasa hapo mtoto huyo atamjuaje mungu wako?,nani atakaye mwelewesha maswala ya uumbaji(kama mnavyoamini?).Binadam wanapata ustaarabu pale tu wanapokuwa katika integration ya wao kwa wao na hapo ndipo wazo la kutafuta asili yake linapoanza kisha tunapata mema na mabaya kisha tunapata idea mbali mbali kama vile uwepo wa mungu,shetani na kadhalika.
Kijana karibu katika ulimwengu huru...