Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Baada ya kukamilisha uumbaji wake Mungu alimpa mwanadam Akili ili aweze kuchagua namna gani ataishi bila kumtenda Bwana makosa,ndo mana hata ukiangalia chanzo cha Mungu kuruhusu mabaya juu yetu ilikua ni mwanadam kumuasi yeye yaani kutotii maagizo aliopewa na Mungu!!
Swami language halihusu baadaya kumaliza uumbaji.
Linahusu wakati mungu anaanza kuuumba ulimwengu.
Na kama mungu ndiye aliyempa mtu akili, na akili hiyo ikawa haitoshi kushinda vishawishi kiasi cha kumfanya mtu kumuasi mungu, mungu muweza yote hastahii lawama kwa kumoa mwanadamu akili ambayo imeshindwa na vishawishi?
Halafu mtoto mchanga anayekufa kwenye tetemeko la ardhi, moja ya mabaya ninayoyazungumziau , amefanya maasi gani?