Usher-smith MD
JF-Expert Member
- Jul 7, 2015
- 9,558
- 12,335
Hakuna ubishi kwamba Davido, msanii kutoka Nigeria, anayewika na kufanya vizuri pengine kuliko msanii yeyote kwa sasa (kizazi kipya) nchini humo na Afrika kwa ujumla, ndiye msanii aliyemrahishia msanii namba moja wa Tanzania, Diamond Platinumz kulipata 'TOBO' la kimataifa kwenye kazi hizi za muziki wanazofanya..
Huo ni utangulizi, siandiki makala...
Lengo la kuuleta huu uzi hapa, ni kujaribu kubashiri kitakachotokea endapo atafanikiwa 'kwa mara ya pili' kumtafutia TOBO mwanamuziki mwingine kiwango wa BongoFleva, Ally Kiba na kuweza kufahamika Nigeria na duniani kama ilivyokuwa kwa Chibu.
Bado Sijaeleweka?
Kwa ufupi ni hivi, Collabo kati ya Davido na Ally Kiba imeshaanza kunukia kama alivyothibitisha mwenyewe Davido kwenye interview aliyofanya na mshikaji wetu wa nguvu MillardAyo.
Story nzima juu ya hili imo kwenye hii video fupi...
Hisani ya Video: MillardAyo
Davido ndio daraja la wabongo
Last edited by a moderator: