Collaboration bora zaidi za Bongo Fleva

Collaboration bora zaidi za Bongo Fleva

Mr 2 na mike t wameimba utanipenda? Sio yule mganda ndio kaimba na mike?
Utanipenda ni wimbo wa Mike Tee na Mganda Mad Ice, ila remix yake ndio Sugu akashirikishwa/akaongezwa.
 
Naupenda huu wimbo, enjoy mistari toka kwa Dallarz na Banana

Mtaani kwetu mwanangu kuna mambo mengi,
mtaani kwetu vituko vingi, mtaani kwetu mwanagu wambea wengi.
Mtaani kwetu wachawi wengi.

mtaani kwetu ee bwana wee utakonda, unakula nyama wengine wanakula ng'onda,
Mtaani kwetu hakuna anayekupenda,
Unahaimia leo kesho unakwenda,
Unapigwa chale usiku unaliwa denda.

mtaani kwetu tunapaweza wenyewe,
Akiibiwa mtu wenyewe kwa wenyewe tunaimbizana Hadi kesi zinakwisha.

mtaani kwetu kunanifurahisha,
Mtoto mdogo anakutingisha,
Kashika bisibisi huku anakutisha,
Ukiwa muoga utasema leo nimekwisha,
Mtaani kwetu hatupendi shule,
Ukitagaza ndoa demu unapewa bure,
Mtaani kwetu usifungue duka,
Wataliwangia hadi liwe linanuka,

Mtaani kwetu hata vyumba havipo,
Tarehe 28 ujiandae na malipo,
Ukipitisha siku vitu vyako havipo,
Kachukua nani baba mwenye nyumba
Mtaani kwetu misikule inalishwa pumba,

Mtaani kwetu kwani mbali,
Si unasikia ngoma watu wanamlema mwali,
Mtaani kwetu chakula chetu ugali.

Mtaani kwetu kweli kiboko,
mpaka sikukuu ndio tunafanya mitoko,
Likinyesha mvuatope la ugoko

Mtaani kwetu usiwe mroho wa nyama,
Mjanja mzima wamenilisha panya,
Mtaani kwetu pananichanganya,
Mtu anapengo utazani mwanya,

Mtaani kwetu mimi sina la kufanya,
Nikiimba mziki eti bishoo,
Nifanye kazi gani? Mzibua vyoo
Mtaani kwetu jamani mnanizingua,
Maendeleo sina mnataka kuniua

Mtaani kwetu kondom ya nini,
Karibia wote tunaumwa Ukimw,
Mtaani kwetu heshima hakuna,
Mtoto mdogo anatukana wakubwa,
Na mzazi anamwabia mwanae mbwa,
Kama yeye mbwa na wewe mbwa,
Jibu kamili wote mijibwa[emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kipindi hicho muziki muziki kweli, watu hawaangalii NANI kaimba wanaangalia NINI kimeimbwa. Tofauti na leo wasanii wanatoa nyimbo za hovyo ila majina yanawabeba
"Nakuhitaji" kipindi unatoka huu wimbo ulikua na mingap miaka??
 
CHRISTIAN BELLA Ft OMMY DIMPOZ- MAMA (hii[emoji91])

F.a FT G-NAKO- Mfalme

WEUSI - GERE

izi. Ni za kizazi kipya...za kizazi cha kale ZOOOOOTE Kali walitisha sana Malegend kweli zakale ni dhahabu

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Hi 👋
Ningependa kushea orodha yangu ya nyimbo bora walizoshirikishana wasanii wa bongo ambazo hazichuji hata ikipigwa leo hii lazima uipende. Naruhusu kurekebishwa penye makosa, lakini pia nipende kuwapa pongezi kubwa Producers Miika Mwamba, PFunk na Master J kwa kazi nzuri waliyofanya maana nyimbo nyingi hapa zitakua zimetengenezwa na wao.

PS: Sijapanga kwa mtirirko rasmi, so hakuna wakwanza wala wa mwisho.

  • Prof Jay ft Ferooz _ Nikusaidieje
  • Caz T ft Wagosi wa kaya _ Tuvumiliane
  • Afande Sele ft Jay Mo &Prof J _ Mtazamo
  • GK ft AY & FA _ Leo
  • Ngwea ft Jay Mo _ Kimya Kimya
  • Ngwea ft Chege _ Kiumeni
  • Afande Sele ft Ditto _ Darubini
  • Prof J ft Diamond _ Kipi sijasikia
  • Berry Black ft Alikiba _ Niko radhi kujitoa roho
  • Keisha ft Squeezer _ Uvumilivu
  • Spack ft Chid Benz _ Laiti Ungejua
  • Tundaman ft Chid Benz _Neila
  • Ferooz ft Prof J _ Starehe
  • K Sal ft Ferooz _ mkiwa
  • Alikiba ft Bery black _ Nakshi Nakshi
  • Abby Skilz ft Mr Blue _ Mimi nawewe
  • Ally Com ft Mishi _ Selina
  • At ft Stara Thomas _ Nipigie
  • Prof J ft Lady Jaydee _ Niamini
  • Abby Skillz ft Bob Junior _ Mpaka milele
  • Jebby ft Afande Sele _ Swaiba
  • Berry Black ft Sumalee _ Nataka unisamehe
  • Juma nature ft Chameleon _ Mikiko mikiki
  • Christian Bella ft Ommy Dimpoz _ Mama
  • Darassa ft Lameck Ditto _ Weka ngoma
  • Young Killer ft Stamina & Quick Rocker _ Jana na leo
  • Gerry wa Rhymes ft Mwasiti _ I love you
  • GK ft TID _ Tunakukumbuka (Tid aliua sana hapa daah)
  • Bushoke ft Juliana _ Usiende mbali
  • K Lyn ft Bushoke _ Nalia kwa Furaha
  • Prof Jay Ft Juma Nature _ Zari la Mentali
  • Kigwema ft Marlaw _ Sitomsahau
  • Marlow ft Chid Benz _ Bado umenuna
  • Matonya Ft Lady Jaydee_ Anitha
  • Mb Dog ft Madee _ Latifa
  • Mez B Ft RayC & Noorah _ Kaa vipi
  • Mr II ft Mike T _ Je utanipenda
  • Mwana FA ft GNako _ Mfalme
  • Ngwea ft Mchizi Mox & Ferooz _ Mikasi

List itakua updated nikikumbuka nyimbo zingine. Je unaipa marks ngapi list yangu

Kama unataka wimbo unaweza kuomba, ninazo kaa 8000 song za zamani
Nazipataje mkuu
 
Mangwair ft Mchizi Mox demu wangu
Nipe ripoti spark ft tunda
Madee &Zillah hili game


Hizi ngoma nasikilizaga tangu zamani sijuagi nani kamfunika mwenzake.
 
Ay ft Lady jaydee-Imani imetoweka,,,nyimbo bora kabisa kutoka kwa Ay,flow kali sana na biti tamu kutoka kwa Pfunk majani[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Afande sele ft Prof jay, solo thang - Mtazamo
Prof jay ft Juma nature - zali la mentali
 
Mbna nyimbo zote za wahenga , au nyie ni wahenga , anyway Recently
1. Kwangwaru - Harmonize ft Diamond
2.Mziki - Darasa ft Ben Pol
3.My number one - Rayvanny ft Zuchu
4.Ni wewe - Killy ft Harmonize
5.
Mtaongezea
Kwangwaru my favorite song
 
Back
Top Bottom