Hautakiwi kukata tamaa. Hizo scholarships ni very competitive zote. Ideally, mara nyingi zaidi unavyozidi ku apply, unaongeza chances zako za kufanikiwa. Ni wachache sana wanazipata on the first attempt. Mimi nilipata hiyo ya Commonwealth, ila nilipata on my third attempt, na my breakthrough ilikua kumpa a previous year winner a review my essays, alinisaidia sana.
Fanya yafuatayo:
1.Ingia Youtube, search 'how to write competitive cheveneng scholarship essays" utapata channels na videos kibao ambazo zimeongelea kinaga ubaga namna ya kufanya essays zako kuwa competitive. Do the same for Commomwealth as well.
2.Hakikisha essays zako zinakua reviewed na mtu ambae aliwahi kushinda mojawapo ya hizo scholarship, hii ni muhimu sana sana, I cant emphasize this enough!! Aliewahi shinda anakua na uzoefu na anajua what it takes to write a winning essay. Unaweza ukawa unasubmit essays kila siku kumbe ziko chini ya kiwango. Ukishaandika essays zako, tafuta mtu aliewahi shinda mtumie azicheki atakusaidia kukwambia wapi pa ku improve. I can assist you with this one free of charge if you wish, as nimewahi pata Commonwealth scholarship.
3. Referees' recommendation letters-Hizi scholarships zote wanahitaji recommendation letters from referees, na zinapokua strong zinakuongezea chances za kushinda pia. So, kusaidia saa zingine huwa inashauriwa wewe kuandika the recommendation letter, ikiwa ume link kwa ustadi na ulichoandika kwenye essays zako, kisha unamtumia referree, yeye anaisoma na kuongezea vichache kama ana cha kuongezea, then anaisaini, sometimes kinachoangusha ni kwamba unakuta recommendation letter toka kwa referrees wako haziko strong kihivyo au hazina link yoyote na ulichoandika kwenye essays zako.
4. Soma kitabu hiki hapa (See attachment) kimeeelezea vizuri SANA namna ya kuandika competitive essays za Cheveneng kwa essay moja moja, nini cha kuweka, how to write it with specific examples. Very useful.
You can PM me kama utakua na maswali zaidi au kuhitaji usaidizi zaidi.Asante.
MoroGent