Synod
JF-Expert Member
- Oct 10, 2016
- 4,143
- 4,180
Ndo maana nikakuita maana walau una taaluma hiyo kama alivyo Annael, binafsi hapa nategemea ubishani wa hoja na sio ubishani wa kishabiki.Asante kwa kuniita huku lakini mada kama hizi itakua vigumu sana kuzijadili maana wachache watakua na uelewa wa nini kinajadiliwa, halafu pia kila mtu anachomekea na kujiita mtaalam. Hebu ona kama huyo Annael eti anaponda kisa website inatumia Wordpress.
Mwisho wa siku cha msingi huwa jinsi unavyotengeneza website yako na kuilinda, haijalishi hata kama umeitengeza from scratch au umetumia framework yoyote, na kingine hiyo Wordpress inatumiwa na mashirika ya kutajika kama vile BBC America, Microsoft news n.k. Haya ni mashirika ambayo huwa makini sana kwa kila aina ya teknolojia wanayotumia, hawana Uswahili mwingi na uzembe kwenye maamuzi.
40+ Most Notable Big Name Brands that are Using WordPress
Kuna hata serikali kama vile ya Uingereza wanaotumia Wordpress UK Government Website uses WordPress | Roger Steer
Halafu nikiamua kupoteza wangu niidadavue kitaalam hiyo mnayoisifia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais nitatiririka na mambo mengi tu.
Nimeangalia kwa haraka tu na kuona machache yanayohusiana na performance bado hata sijawaza kuangalia design, na security na mengine.
Haya tu baadhi ya performance issues
Images hazijawa scaled, unakuta zingine ni 2mb
Hawajatumia gzip compression, wamejaza file za scripts na CSS kiholela, na hawajafanya JavaScript parsing deferment
Watumie CSS sprites kufanya combination ya images
Kuna page zingine zina 404 http://ikulu.go.tz/files/gallery/videos/thumbs/IMG_8156.JPG
Wenye taaluma ndogo na haya mambo tutakuwa tunachokoza mada tu!