Wrong, nguzo ya umeme haionekani yenyewe.
Wewe unaona photons zinazosafiri kutoka kwenye nguzo ya umeme na kufika kwenye macho yako. Unaiona nguzo ya umeme si kama ilivyo sasa, bali kama ilivyokuwa hapo photons zilipotoka.
Kama mtu anaweza kwenda kwa kasi sana, anaweza kwenda kwenye nguzo ya umeme akaiondoa kabla ya particles zinazokuonyesha nguzo ya umeme ilipo hazijakufikia machoni, nguzo ya umeme isiendelee kuwapo, lakini wewe ukaona ipo.
To illustrate better this example, I will use the sun.
Tunapoangalia jua, hatulioni kama lilivyo sasa, bali kama lilivyokuwa dakika nane na sekunde ishirini zilizopita. Kwa maana huo ndio muda ambao mwanga unatumia kusafiri kutoka kwenye jua mpaka duniani kwenye macho yetu.
Kwa hiyo, jua likizimika ghafla sasa hivi, hatutajua kwamba jua limezimika mpaka zipite dakika nane na sekunde ishirini.
Hatuoni vitu kama vilivyo directly, tunaona effect ya vitu hivyo inavyotufikia kwa photons zinazosafiri kwa speed ya mwanga.
Basic relativity theory.
Nyota nyingine unazoziona usiku hazipo hapo zinapoonekana kuwapo. Zilishanyauka na kulipuka mamilioni ya miaka iliyopita.
Lakini unaziona hapo zilipo kwa sababu mwanga wake ndio kwanza unatufikia.
Hatuoni nyota, tunaona effect. Vivyo hivyo kila tunachokiona tunaona effect tu. Hakuna tunachokiona directly.