Complete heart transplant; rethink your faith!

:hail:I bow to the docs, hands down, thats pure science! Inasikitisha sana mtu ana mgonjwa kwenye critical condition, daktari akiokoa maisha yake shukrani anapewa mungu, how does he even come into this?!!...:wacko:

Aliye create pure science ni Mungu, hata hao madaktari hawakujiumba wala kujizaa, that's the way God comes into picture dude..That super power that gives you breath, the.power that decides when you are going.to go deeper into earth.
 
Last edited by a moderator:
Kukubali nini mkuu?
Kuwa sio Mungu anaefanya niliyosema kwenye post yangu
Ni hivi hapa mimi niko neutral (sijui ni Mungu au si Mungu), mleta mada anasema si Mungu, wewe unasema ni Mungu.
Nilimpa sababu za mimi kusema ni Mungu na nikampa nafasi ya kuthibitisha kuwa sio Mungu anaefanya hayo na ameshindwa hadi sasa
Sasa wewe usemaye ni Mungu naomba uthibitishe, na mleta mada na yeye athibitishe (nafikiri umeshamuuliza swali).
Unataka uthibisho wa namna gani?
Leo nataka elimu tu, siko upande wowote.
Safi sana
Nisaidie kile unachotaka kujua kwa hilo swali hapo juu

By the way,habari ya siku?
 
Nasubiria hili jibu hapa ........
Ngoja huyu jamaa aje na jibu
Mkuu wa chuo kuna utam hapa Sangarara uko wapi mazee?
Kwa hilo swali naona jamaa mmempa kibano mpaka anaanza kuchepuka anaanza kuongea vitu ambavyo havipo kwenye swali Lakini Ishmael anamrudisha kwenye mstari tu, hebu ngojea niendelee kushuhudia...
 
Last edited by a moderator:
Kuwa sio Mungu anaefanya niliyosema kwenye post yangu

Kama nilivyokwambia mwanzo, siwezi kukubali au kukataa pasi na uthibitisho

Nilimpa sababu za mimi kusema ni Mungu na nikampa nafasi ya kuthibitisha kuwa sio Mungu anaefanya hayo na ameshindwa hadi sasa

Sababu zako ulizompa ndio zilinifanya nikuulize uthibitisho wa hizo sababu,

Mf. kuhusu Mungu kuwapa akili hao madaktari ni moja ya sababu ulizotoa, Je unaweza thibitisha ya kuwa Mungu ndo kawapa akili madaktari?

Unataka uthibisho wa namna gani?

Uthibitisho wowote ule ambao hautasababisha maswali zaidi.

Safi sana
Nisaidie kile unachotaka kujua kwa hilo swali hapo juu

Ninachotaka kujua hapa ni kuhusu usahihi wa mada hii, (je mleta mada yuko sahihi kusema kwamba madaktari ndio wanaostahili shukrani na si Mungu?)

Sasa hapa nimekutana na views mbili tofauti, ndo maana nataka uthibitisho.

By the way,habari ya siku?

Habari ya siku ni nzuri mkuu, sijui kwa upande wako
 
Labda Dreadnought anaweza kumsaidia
Huyo jamaa sijui ana matatizo gani!
Free ideas alileta mada wamempa kibano hajaonekana, sasa labda na huyu mwenzake sijui kama atahimili, hawa inawezekana wakawa wametoka kule kwa kina Gavana maana uwezo wao unatia shaka ngojea niendelee kumsoma CYBERTEQ labda anaweza akawa tofauti na mwenzake...
 
Last edited by a moderator:
Mm ninapoenda kumshukuru Mungu c kwamba cjui kuwa n juhudi za daktari zimesaidia natambua kwan najua kila mtu kapewa karama n Mungu na ndio maana daktar huyo huyo ukimpa boti aendeshe anaweza kuuwa watu wote. Kwa hyo shukran yangu kwa Mungu ni kuniwezesha kupona tatizo langu wakati mwingine kafa kwa tatizo hilo hilo n kingine n kumshukuru Mungu kwa ajili ya huyo daktari pia aweze kuhudumia n wengine
 
Aliye create pure science ni Mungu, hata hao madaktari hawakujiumba wala kujizaa, that's the way God comes into picture dude..That super power that gives you breath, the.power that decides when you are going.to go deeper into earth.

holly crp! mungu hayupo kabisa kwenye picha, ulishawahi kuskia mtu kafanyiwa operation kwa kutumia bible? nguvu gani unazoongelea, za mungu aliyekuwa anatishia uhai wa huyu jamaa aliyefanyiwa operation hapo juu wajanja wamembadilishia moyo na akaendelea na maisha? kwa ugonjwa aliokuwa nao hata angefunga miaka elfu saba na kumwomba huyo jamaa anayeitwamungu angekufa tu!
 
Labda Dreadnought anaweza kumsaidia
Huyo jamaa sijui ana matatizo gani!

Mkuu hili suala la wagonjwa wawili kutibiwa na daktari mmoja, mmoja akapona na mwingine asipone, linaweza jibika vizuri kama atapatikana daktari hapa,

Kunaweza kuwa na sababu mf. kuchelewa kuanza matibabu kwa mgonjwa wa pili n.k

Labda nimuombe mkuu Ishmael kama kuna case yoyote kama hiyo ambayo mgonjwa mmoja alikufa kati ya wawili walotibiwa na dakatari mmoja ikiwa all factors remained constant atuwekee reference hapa.
 
Last edited by a moderator:
Kama nilivyokwambia mwanzo, siwezi kukubali au kukataa pasi na uthibitisho
Sawa
Sababu zako ulizompa ndio zilinifanya nikuulize uthibitisho wa hizo sababu,

Mf. kuhusu Mungu kuwapa akili hao madaktari ni moja ya sababu ulizotoa, Je unaweza thibitisha ya kuwa Mungu ndo kawapa akili madaktari?
Mantiki inakana kuwepo kitu chenye mpangilio kama binadamu bila kuwepo muwekaji wake,hivyo mimi na mwingine yoyote anaetumia mantiki atakubali kuwa hata nyumba haiwezi kuibuka tu bali lazima kuna mjenzi

Kama ni hivyo basi na binadamu nae ana muwekaji na aliyempangilia awe kama alivyo,na huyu aliyepangilia haya ninamuita Mungu
Uthibitisho wowote ule ambao hautasababisha maswali zaidi.
Huo hapo juu
Ninachotaka kujua hapa ni kuhusu usahihi wa mada hii, (je mleta mada yuko sahihi kusema kwamba madaktari ndio wanaostahili shukrani na si Mungu?)
Hao madaktari wanamtibu binadamu kwa kufuata kanuni alizo nazo huyo binadamu,hawawezi kubadilisha mshipa unaoingiza damu kwenye moyo na kuuweka mahali pa unapotoa damu

Hakuna kipya wanachokifanya zaidi ya kufuata kanuni ambazo kama nilivyosema hapo juu ni LAZIMA ziwe na muwekaji
Sasa hapa nimekutana na views mbili tofauti, ndo maana nataka uthibitisho.
Habari ya siku ni nzuri mkuu, sijui kwa upande wako
Kama uko sawa namshukuru Mungu
Sijui wewe utamshukuru nani ...lol!
 
Mkuu labda ulirudie swali kisha ulisome upya!
 
Sijaona wa kujibu hapo

Labda anaweza kujaribu yule anaetumia ile list!
Kiranga anaweza akajaribu ila hawa wengine sijui wamekurupuka nashindwa kuelewa, mtu ana pewa logic anaanza kuzunguka zunguka tu, yule Free ideas ndio ameniacha hoi kabisa...
 
Last edited by a moderator:
Mantiki inakana kuwepo kitu chenye mpangilio kama binadamu bila kuwepo muwekaji wake

Sasa mkuu hii mantiki yako itamtaka Mungu na yeye awe na muwekaji, kwa sababu inakana uwepo wa kitu chenye mpangilio bila kuwa na muwekaji.

hivyo mimi na mwingine yoyote anaetumia mantiki atakubali kuwa hata nyumba haiwezi kuibuka tu bali lazima kuna mjenzi

Kwa hiyo unakubali kuwa Mungu na yeye ana muwekaji?

Kama ni hivyo basi na binadamu nae ana muwekaji na aliyempangilia awe kama alivyo,na huyu aliyepangilia haya ninamuita Mungu

Swali hilo hapo juu

Hao madaktari wanamtibu binadamu kwa kufuata kanuni alizo nazo huyo binadamu,hawawezi kubadilisha mshipa unaoingiza damu kwenye moyo na kuuweka mahali pa unapotoa damu

Hapana mkuu, madaktari muda fulani si lazima wafuate kanuni za muwekaji,

Mf. Mtu akiwekewa vyuma badala ya mifupa, hapa kanuni ya muwekaji haijafuatwa

Hakuna kipya wanachokifanya zaidi ya kufuata kanuni ambazo kama nilivyosema hapo juu ni LAZIMA ziwe na muwekaji

Nimekujibu hapo juu

Kama uko sawa namshukuru Mungu
Sijui wewe utamshukuru nani ...lol!

Wa kuwashukuru wako wengi mkuu ndugu, jamaa, marafiki n.k
 
There are so many of such cases and in fact, wakati mwingine anaye fariki ni mwenye afadhali.
1. Kutoka na jibu lako hapo juu, linakubaliana nami kuwa Dawa sio inayo ponya.
2. Kutokana na jibu lako hapo juu, linakubali kuwa Daktari anacho fanya ni kutibu tu.
3. Kutoka na jibu lako hapo juu, linakubali kuwa uponyaji wa mgonjwa si tegemezi katika Dawa.

Kumbe ndio maana tuna kuwa na vifo ingawa mgonjwa amepewa dawa. Uponyaji sasa unaanza kuonekana sio kutoka kwa madaktari wanao toa treatment na au kunywa dawa but upo kwa mwengine ambaye haonekani.

Tunaweza kuweka two cases za heart transplant na cha kushangaza.

1. Wote wanaweza kupona.
2. Wote wanaweza kuto kupona
3. Mmoja anaweza kupona

Ndio maana science bado inabakia tegemezi kwa asiye onekana.
 
Nakubaliana na wewe kuwa ili mgonjwa atibiwe na apone kabisa si dawa tu kuna factors nyingine nyingi mf. Muda wa kuanza matibabu, utayari wa mgonjwa kupokea matibabu n.k

Kumbe ndio maana tuna kuwa na vifo ingawa mgonjwa amepewa dawa. Uponyaji sasa unaanza kuonekana sio kutoka kwa madaktari wanao toa treatment na au kunywa dawa but upo kwa mwengine ambaye haonekani.

Kwa nini useme uponyaji uko kwa mwingine asiyeonekana?

Nimekupa sababu chache zinazoweza mfanya mtu asipone pamoja na kupata matibabu.

Tunaweza kuweka two cases za heart transplant na cha kushangaza.

1. Wote wanaweza kupona.
2. Wote wanaweza kuto kupona
3. Mmoja anaweza kupona

Ndio maana science bado inabakia tegemezi kwa asiye onekana.

Sababu zinazoweza sababisha hayo yote zipo, kwa nini useme kuna asiyeonekana?

Jee unaweza kuthibitisha kuwa asiyeonekana ndo anaponya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…