Comrade Peter Magoti afunga pingu za maisha

Dr Restart

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
4,949
Reaction score
24,046
Leo tar 04 Septemba 2021, kada kindakindaki wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg Petro Magoti amefunga pingu za maisha na mchumba wake wa muda mrefu, mrembo Joyce Mvungi.


Kada huyu ambaye anafanya kama Ofisa Makao Makuu ya Chama. Alikuwa msaidizi wa karibu sana kwa aliyekuwa Katibu wa NEC, Siasa na uenezi, Ndg Humphrey Polepole.

Mkewe ni wakala wa Ulimbwende wa kampuni maarufu ya Black Fox Models Africa.

Harusi hiyo imefanyika katika viunga vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Tuwatakie ndoa njema na yenye furaha.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…