Confession about wauza mihogo coco beach

Wauza mihogo na mishikaki wa uswahilini wanaruhusiwa kuleta mihogo na mishikaki yao hapo kwenye ndoo kuwauzia walalahoi ??
Swali zuri
 
Ni wajanja kabla hujaagizia Jua bei kwanza, ukila alafu uulize bei wanajua lazima utalipa ndio maaana wanapandisha bei. Sio coco tu asilimia kubwa ya boda boda biashara za rejareja wanafanya hivyo ni uhuni tu
 

Kuna viwanja vya maeneo ya beach kibao tu tena sehem nzuri huwez kuta unauziwa mishkaki bei ya kijinga kama wanavyotapeli hapo coco. Serikali iliacha lile eneo wazi ili walala hoi waweze nao kuja beach kuchezea maji na kula vyakula Kama mihogo. Serikali ikaona iwaruhusu raia wa hali ya chini wajenge hayo mabanda ili wawahudumie walala hoi wenzao!! Kumbe mambo yako tofauti. Wauza mihogo wana bei Kama za hotelini, malala hoi hakanyagi coco.
 
Wakienda mahotelini soda tu wanauziwa 2000 Hadi 3000 na hawalalamiki ila Coco Beach wanalalamika hovyo
Kachumbari yao wanavyoimiksi,hunikumbusha zamani tukienda fua nguo mtoni, kachumbari ile maradhi tupu,kama ya yule nani bonge sijui pale kinondoni,sharti uharishe
 
Where is the CONFESSION?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…