Confession about wauza mihogo coco beach

Confession about wauza mihogo coco beach

Weka nyama za kueleweka ambia watu hata 3000 watanunua.
Sio utapeli ule wanaoufanya
Ila ndio hivyo kuna raia nao wanazo pesa za bure bure za kuchezea na kutapanya, kuna walimbukeni na washamba wanaoingia mjini kila siku kwa hiyo acha wajanja wapige pesa tu, hili ni soko huria, kufa kufaana.
 
Kwani mnakwenda beach kula ama kupata upepo wa Bahari?
 
Kama havifai achana navyo
Toka kwako umekula
Fika coco beach
Chezea mchanga na konokono wa baharini
Waruhusiwe wauza mihogo na wauza mishikaki wowote wafunge miamvuli hapo wafanye biashara, sio hao wauza mihogo wa TikTok na Instagram tu, beach ni mali ya umma.
 
Salaam wana jukwaa.

Nimepita sehemu moja nikakuta watu wanajadili kuhusu tabia ya upigaji ya wauza mihogo na mishikaki COCO BEACH.

Malalamiko yamekuwa mengi kuhusu tabia yao ya kuuza mishikaki kwa bei ya juu huku bidhaa hizo zikiwa sio za gharama hiyo kwa uhalisia.

Sasa kama wanajamvi naomba tusaidiane namna ya kukabiliana na wahuni hawa.

Tupatie mbinu ya kuhakikisha hauingii kwenye upigaji wa hawa jamaa.
Beba mihogo na mishkak yako kwenye kapu uende nayo, siyo lazima ununue kwetu
 
Wakienda mahotelini soda tu wanauziwa 2000 Hadi 3000 na hawalalamiki ila Coco Beach wanalalamika hovyo

Hawa lalamiki huko hotelini kuuziwa soda elfu2 kwasababu wanapata huduma inayoendana na mazingira. Coco Mazingira ya hovyo tu unawekewa zile meza za plastic za cocacola na viti vya plastic, unaletewa vimishkaki 15 kwenye sahani la plastic Kama la mama ntilie wa soko la mabibo muhudumu yuko hovyo tu kavaa mashat yake ya nyumbani halafu unatozwa elfu25 nyama haifiki hata robo!! Kwanza wahudumu wengi pale ni madalali tu mteja unakamatwa juu kwa juu unabamizwa mabei ya kishenzi Halafu watu wanaenda kugawana pesa zako!! Pale ukizubaa hata juice ya miwa glass utauziwa 5,000. Ningekuwa nina mamlaka ningepitisha greda nikavunja mabanda yote nikatomeza wale wahuni. Niliendaga na familia yangu coco zile bei nilizopigwa niliapa sitarudi tena kula ule ujinga pale. COCO WAACHE UTAPELI.
 
Back
Top Bottom