Waalimu hawapendi slow learner na wakorofi hata mara moja.
Soma neno kwa meno utagundua Waalimu walikuwa wanamwambia utafeli.
Sababu kuna kitu hakikuwa sawa.
Kwanini madam alikuwa anamtetea?....
Kuna kitu kimejificha...huwezi kutetea kama huna makosa
Hao ambao hawapendi slow learner hawana hadhi ya kuitwa waalimu,
Unajua kazi mojawapo ya mwalimu ni kumjengea mwanafunzi saikolojia ya uwezo wa kufanya vizuri ktk masomo!!
Saikolojia ni kitu muhimu sana kwa kila mtu ambae yupo hai, kuwa slow learner haimanishi kuwa ndio hafai kuwa mwanafunzi na kujifunza,
Nikupe mfano unaonihusu mm,
Wakati nasoma mm nilikuwa nalichukia sana somo la hesabu sababu nilikua nafeli sana alafu nilikua naumia sana nikifeli...
Nakumbuka alitokea mwalimu mmoja kijana kijana aliniita ofisini akaniuliza kwann ninafeli hesabu wakati uwezo wa kufaulu nnao, kama nimeweza kufaulu masomo mengi yote inakuaje nifeli hesabu..!!!
Mwanzoni niliona yule mwalimu kama ananikejeli...akawa rafiki yangu sana na hata nikifeli alikua ananiambia wewe HESABU UNAJUA ILA TU HAUTAKI KUFAULU,
Sio siri yale maneno yake hadi leo bado nayasikia akilini mwangu na jinsi alivyokua ananiambia kirafiki....
Tangu awe ananiambia hivyo nilianza kulipenda somo la hesabu na kualifanyia kazi...nikikwama namfata, mwisho hadi nilikua napanda grades na mwalimu alikua anafurahi na kuniambia si nilikwambia mm![emoji1][emoji1]
Kwahiyo ile hali ikanifanya niwe mtu nnae jichukulia kuweza ila tu ni kuamua...
Kwakweli hesabu nilikua naziogopa sana lkn baada ya kukutana na yule mwalimua mbona nilitafuta hata CSBM kama ulikua mtu wa hesabu hicho kitabu utakua unakijua vizuri...kina maswali magumu lkn nilikua nafanya kila siku hadi nikawa nakiona hamna kitu,
Kuna haja sana ya wizara kuliangalia hili swala la waalimu wanaotufundishia watt wetu....wangekuwa wanapata na elimu ya saikolojia ingependeza sana.