Confession: The hurting truth -- natamani kurudi kwenye ushirikina

Confession: The hurting truth -- natamani kurudi kwenye ushirikina

Hapo uliposema.umegawa vifaa vya kazi ndo unanipa ukakasi kiongozi.. Yaan ni sawa uamue kuacha ujambaz then ugawe zana za ujambaz kwa jambazi mwingine aendeleze ujambazi

Si ungetupa na kuchoma.vyote mkuu .... Huwez kuacha uovu kwa kuhamisha kuupeleka kwa mwingine aendelee...
Ushirikina ni tofauti na ujambazi si kila kitu ni yabisi na kuna vingine havitupiki havichomeki
 
Niliachana kabisa na mambo yote ya kishirikina miezi kadhaa iliyopita, na kuthibitisha hilo niliweka uzi rasmi hapa JF na kumrudia Mola wangu mazima. Na kuna hili ambao sikuwahi kulisema hapa lakini wale ambao niliwaumiza na roho ikaniongoza tusawazishe nilifanya hivyo. Na nikapata amani kubwa moyoni

Naamini nanyi ni mashuhuda wa hili kwakuwa nilipunguza mada za ushirikina kwa asilimia 80 ama 90 hivi. Na kila nilichomiliki chenye viashiria na viasili vya ushirikina ama niligawa au niliviharibu na kuviteketeza kwa moto kwa mikono yangu mwenyewe. Nilihakikisha naishi maisha ya ukamilifu na usafi wa kiroho

LAKINI wapendwa shetani ana nguvu sana sana. Unapokuwa umevaa koti jeupe la mshika dini na asiyependa mambo ya ulozo lakini ndani u mchafu kupitiliza wala sheatani hawezi kukusumbua kabisa lakini once unapomkataa kwa roho na kweli. VITA HUANZIA HAPO! atakujia na washirika wengine SABA kuhakikisha wanakurudisha kwenye himaya yao.

Juzi kati nilikuwa maeneo ya mikwambe Kigamboni kibada mpaka saa tatu usiku hivi wakati naondoka nikagundua kuna watu walikuwa wameniungia body na nilienda nao mpaka Tuangoma halafu wakapotea kusikojulikana

Tangu hapo nimejiwa na msisimko wa ajabu kabisa. Msisimko wa kutafuta zile nguvu za giza tena. Najitambua kiimani na kiroho niko vizuri mno. Lakini sasa naona viashiria vya kunirudisha kilingeni vinazidi kupata nguvu kila uchao.

Tafadhalini naomba msije mkanishangaa in case mkisikia nimerudi Msata Kilingeni penye shina langu. Lakini pia ukiweza na ukipenda kwa utashi wako pls niombee. Kuna shida nyingi huko vilingeni basi tuuu[emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
Nakushauri jishike na Yesu Kristo na uwe serious na jambo hilo la sivyo hukawii kutoweka ulimwengu huu na kwenda kutumikishwa kwenye mashimo ya uharibifu!
 
Mathayo 12:43-45

Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Asomae na aelewe maandiko haya yani ukorudi huko ni kama kikirudia kifo soma sana Biblia fanya maombi ya kufunga hyo hali itaondoka chonde usirudi nyuma
 
Hahahahaha haka kajamaa bane me ni mdau mkubwa wa thread zake but sijawahi kukaamini. Huwa nachukulia mizengwe2. (Sorry kutuamia kiambishi "ka")
 
Hahahahaha haka kajamaa bane me ni mdau mkubwa wa thread zake but sijawahi kukaamini. Huwa nachukulia mizengwe2. (Sorry kutuamia kiambishi "ka")
Sio kosa lako ni tatizo la kisaikolojia.. Kuna baadhi hupenda kuwaita wazazi wao 'haka kazee...'!
 
Mimi nakushauri kuwa ukiona hiyo hali inakujia ya kuoenda kurudi uliko toka penda kufanya mambo yafuatayo.
1.Sikiliza sana nyimbo za kuabudu /tenzi hizo hushusha uwepo wa Mungu na nguvu zake hukujilia kwa upya.

2.Soma sana Biblia humo utapata ushindi wa kila jambo.

3.Naamini una Roho Mtakatifu mshirikishe huyo kabla hujafanya maamuzi
 
Nyama ya binadam ni tamu sana ndo maana tunakazwa tusionje, hata Simba huko porin akionja nyama ya binadam huwa anatafutwa Hadi auwawe hata wawe Simba 10 Ni lazma wauwawe ukionja nyama ya binadam huwez kuacha.
Hapa Mnamaanisha Kula Nyama Kabisa? Au Limekaa Kimafumbo hili Jambo la Kula Nyama Ya Mtu
 
Jipe moyo mkuu, watu wengi wanatoka kwenye ushikina wanakuja nuruni wewe unatamani kurudi huko? Unajua kwenda mbinguni ni vita lakini Mungu ni mwaminifu hachelewi kufungua mlango wa kutokea. Bora uteseke ukifa uende pema kuliko pabaya. Nakushauri komaa tu mkuu!
@Mshana Jr Chukua Huu Ushauri mkuu. Naamini upo katika Kusaidia watu waepukane na Wajikinge na Ulozi na Ushirikina

Wachawi,Majini,Mashetani Ni Vitu Vibaya Hasa Vikishampa Mtu. Nikuombe Usirudi huko ila Jikite katika kutoa Elimu ya Kuwaepusha Watu na Wabaya Hao na Watumie Nini ili Kujikinga Navyo pamoja Na Nguvu za Mungu Muumba
 
Back
Top Bottom