Ushirikina ni tofauti na ujambazi si kila kitu ni yabisi na kuna vingine havitupiki havichomekiHapo uliposema.umegawa vifaa vya kazi ndo unanipa ukakasi kiongozi.. Yaan ni sawa uamue kuacha ujambaz then ugawe zana za ujambaz kwa jambazi mwingine aendeleze ujambazi
Si ungetupa na kuchoma.vyote mkuu .... Huwez kuacha uovu kwa kuhamisha kuupeleka kwa mwingine aendelee...
Anafikiri ulozi ni kuchanganya kama mbege na konyagiUshirikina ni tofauti na ujambazi si kila kitu ni yabisi na kuna vingine havitupiki havichomeki
Nakushauri jishike na Yesu Kristo na uwe serious na jambo hilo la sivyo hukawii kutoweka ulimwengu huu na kwenda kutumikishwa kwenye mashimo ya uharibifu!Niliachana kabisa na mambo yote ya kishirikina miezi kadhaa iliyopita, na kuthibitisha hilo niliweka uzi rasmi hapa JF na kumrudia Mola wangu mazima. Na kuna hili ambao sikuwahi kulisema hapa lakini wale ambao niliwaumiza na roho ikaniongoza tusawazishe nilifanya hivyo. Na nikapata amani kubwa moyoni
Naamini nanyi ni mashuhuda wa hili kwakuwa nilipunguza mada za ushirikina kwa asilimia 80 ama 90 hivi. Na kila nilichomiliki chenye viashiria na viasili vya ushirikina ama niligawa au niliviharibu na kuviteketeza kwa moto kwa mikono yangu mwenyewe. Nilihakikisha naishi maisha ya ukamilifu na usafi wa kiroho
LAKINI wapendwa shetani ana nguvu sana sana. Unapokuwa umevaa koti jeupe la mshika dini na asiyependa mambo ya ulozo lakini ndani u mchafu kupitiliza wala sheatani hawezi kukusumbua kabisa lakini once unapomkataa kwa roho na kweli. VITA HUANZIA HAPO! atakujia na washirika wengine SABA kuhakikisha wanakurudisha kwenye himaya yao.
Juzi kati nilikuwa maeneo ya mikwambe Kigamboni kibada mpaka saa tatu usiku hivi wakati naondoka nikagundua kuna watu walikuwa wameniungia body na nilienda nao mpaka Tuangoma halafu wakapotea kusikojulikana
Tangu hapo nimejiwa na msisimko wa ajabu kabisa. Msisimko wa kutafuta zile nguvu za giza tena. Najitambua kiimani na kiroho niko vizuri mno. Lakini sasa naona viashiria vya kunirudisha kilingeni vinazidi kupata nguvu kila uchao.
Tafadhalini naomba msije mkanishangaa in case mkisikia nimerudi Msata Kilingeni penye shina langu. Lakini pia ukiweza na ukipenda kwa utashi wako pls niombee. Kuna shida nyingi huko vilingeni basi tuuu[emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
Mizimu itampa vingine uyo jamaa kaa mbali ni mtu hatar snSasa hivo vibuyu si ulivochoma moto , utavipataje vingine doctor na ule uchawi si uliugawa huko Sumbawanga! Utaufata huko?
Asomae na aelewe maandiko haya yani ukorudi huko ni kama kikirudia kifo soma sana Biblia fanya maombi ya kufunga hyo hali itaondoka chonde usirudi nyumaMathayo 12:43-45
Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.
Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.
Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Sio kosa lako ni tatizo la kisaikolojia.. Kuna baadhi hupenda kuwaita wazazi wao 'haka kazee...'!Hahahahaha haka kajamaa bane me ni mdau mkubwa wa thread zake but sijawahi kukaamini. Huwa nachukulia mizengwe2. (Sorry kutuamia kiambishi "ka")
Hahahahahaha raia wanakukaribisha![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Dah[emoji31][emoji38]
@Mshana Jr Kuna Ukweli hapa?Dawa ya wachawi pombe tu na kitimoto. Hawasogei nyumbani kwako. Kula mdudu nyumbani baadhi ya mifupa weka karibu na kwako umemaliza kazi
Hapa Mnamaanisha Kula Nyama Kabisa? Au Limekaa Kimafumbo hili Jambo la Kula Nyama Ya MtuNyama ya binadam ni tamu sana ndo maana tunakazwa tusionje, hata Simba huko porin akionja nyama ya binadam huwa anatafutwa Hadi auwawe hata wawe Simba 10 Ni lazma wauwawe ukionja nyama ya binadam huwez kuacha.
@Mshana Jr Chukua Huu Ushauri mkuu. Naamini upo katika Kusaidia watu waepukane na Wajikinge na Ulozi na UshirikinaJipe moyo mkuu, watu wengi wanatoka kwenye ushikina wanakuja nuruni wewe unatamani kurudi huko? Unajua kwenda mbinguni ni vita lakini Mungu ni mwaminifu hachelewi kufungua mlango wa kutokea. Bora uteseke ukifa uende pema kuliko pabaya. Nakushauri komaa tu mkuu!